CCM bado tupo imara!

CCM bado tupo imara!

Ingawa tumebwagwa vibaya katika uchaguzi wa Udiwani Arusha Jumapili iliyopita, bado CCM tupo imara. Ni wazi kuwa kuanzia uchaguzi mkuu wa 2010,hasa katika chaguzi ndogo mbalimbali,kura zetu zinaendelea kuserereka kuelekea chini pamoja na kushinda sehemu nyingi nchini kwa kipindi hicho.Bado tuna nafasi ya kujirekebisha.

Chaguzi hizi ndogo ni kama mechi za kisoka. Viongozi wetu (makocha wetu) wameshauona udhaifu unaojitokeza chamani na hata kwenye kampeni.Ni watu waonaji na wasikivu.Watafanya jambo. Watakirekebisha vyema chama kuelekea 2015. CCM yetu bado imara na iko tayari kwa uchaguzi wowote mahali popote. Yeyote atakayestahili adhabu ya kichama atapewa;wa kutunukiwa atatunukiwa.

Lakini,kama chama kikomavu,tunatambua kuimarika kwa chama kikuu cha upoinzani nchini CHADEMA SIKU HADI SIKU. Tunatambua kuwa siasa za nchi hizi naimarika na kunoga. Zinaelekea pazuri. Zitafikia mahali ambapo wapigakura watachagua maendeleo hasa. CCM tunajiandaa kwa hilo. Tunajiimarisha kwa siasa za kihoja za haja. Tupo tayari haswa!

CHADEMA,CUF,NCCR-Mageuzi,TLP na wengineo kaeni chonjo.CCM inaimarishwa na siasa za sasa za kidijitali. Bado tupo imara!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
mko imara kweli kwani uongo tunaona hapo chini na vikosi vyenu vya green rebels
998861_490081497742516_1206258209_n.jpg
 
mko imara kweli naamini hii mamluki ya cdm haiwatishi
998696_695792413780878_1609746419_n.jpg
 
Back
Top Bottom