CCM Arusha kwazidi kuchafuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Arusha kwazidi kuchafuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by baraka boki, Jun 4, 2011.

 1. b

  baraka boki Senior Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  na David Frank, Arusha
  MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Arusha (UV-CCM), James Millya, ni miongoni mwa watakaohojiwa leo na Kamati ya Usalama na Maadili ya Mkoa kufuatia mgogoro unaofukuta kati ya makundi mawili ya vijana hao kuhusu falsafa mpya ya Kujivua Gamba kwa wanachama wa ngazi ya juu wa CCM.

  Wakati kundi jingine likitaka wanachama hao ambao ni aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa; Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge; na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, wajivue gamba kundi jingine linapinga uamuzi huo.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana ndani ya chama hicho mkoa na kuthibitishwa na Katibu wa CCM Mkoa, Mary Chatanda, zinaeleza kuwa mbali na mwenyekiti huyo pia wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya UV-CCM mkoa nao watahojiwa sambamba na wanachama walioshiriki katika maandamano yaliyofanyika hivi karibuni.

  Katika madai yao waandamanaji hao kutoka wilaya zote mkoani hapa ambazo ni pamoja na Arusha Mjini, Monduli, Arumeru, Longido, Ngorongoro na Karatu, walikuwa wakishinikiza katibu huyo aachie ngazi kwa madai ya kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kusababisha majimbo mawili ya uchaguzi ya Arusha Mjini na Karatu kuchukuliwa na wapinzani.

  Mbali na majmbo hayo pia walidai kuwa kushindwa uchaguzi katika baadhi ya maeneo kulisababishwa na katibu huyo, wakimtuhumu kufanya kazi kibabe na zaidi ya hayo anaingilia kazi za jumuia hiyo.

  Katika kikao hicho kitakachokuwa chini ya Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole, baadhi ya watakaohojiwa walidai kuwa kina lengo la kuwatisha kufukuzwa uanachama.

  Wakizungumza na gazeti hili, miongoni mwa watakohojiwa leo walilalamika na kuhoji ni vipi wao wawekwe kiti moto huku kundi lingine la vijana hao waliofanya maandamano kama hayo likiachwa.

  “Nashindwa kuelewa ni vipi kundi lililoandamana na kutoa matamko mazito dhidi ya viongozi wa ngazi za juu liachwe bila kuwekwa kiti moto na kuwataka vijana wa upande mmoja kuhojiwa peke yao.

  “Tunajua lengo la kikao cha leo ni kututisha tuache dhamira yetu ambayo tutaendelea nayo hadi kieleweke,” alisema mmoja wa vijana hao.

  Katika siku za hivi karibuni makundi mawili ya vijana mkoani hapa yamekuwa yakisigana na kulumbana huku kila moja likielezea hisia zake juu ya mustakabali wa falsafa mpya ya Kuvua Gamba.

  Wakati moja likipinga hatua hiyo na lingine linasisitiza watuhumiwa wote wanaodaiwa kuhusika na tuhuma za ufisadi wang’olewa kwa lengo la kusafisha chama.

  Kadhalika ilidaiwa kuwa watuhumiwa wa ufisadi walikifanya Chama cha Mapinduzi kukosa mvuto mbele ya Watanzania katika uchaguzi mkuu uliopita na kusababisha majimbo mengi nchini kunyakuliwa na wapinzani katika nafasi ya ubunge na udiwani.
   
 2. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Wacha wamalizane, CDM zidi kuwapelekea moto,wakishindwa huko waje kwenye chama cha ukombozi wa Mtanzania CHADEMA!!! Mwenye macho haambiwi tazama!!!!!
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Waache wamalizane wenyewe kwa wenyewe na kusemana fulani kakosa maadili fulani ni mtovu wa nidhamu wakimaliza kugombana mambo yashakuwa mengiene
  Ila si hawa hawa waliteteana kuwa kila kitu kipo shwari hapa arusha au imekuwaje tena
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Watapasuana mpaka watamalizana na hata kwetu hatuwataki! Mimi kama mkazi wa Arusha nawashangaa eti vijana wanajiita ni wa ccm. Wanasema kwenye tv na magazeti tu. Mtaani hakuna kijana anayeweza kusema kwa akili timamu kabisa kuwa ni ccm. Maana ndani ya muda mfupi atakuwa ICU ametundikiwa drip na madaktari wanamfanyia operation ya ubongo baada ya kufikishwa huko na wasamaria wema wakiwa na ushahidi kuwa ana mtindio wa ubongo kwa kunukuu maneno yake! Kwa kuwa madaktari nao wapo Arusha wataamini na watajaribu kumwondolea hiyo hali maana kwa Arusha ya sasa haiwezekeani mkazi wa hapa huwezi kuwa ccm!.
   
 5. A

  Abunuas JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 8,730
  Likes Received: 420
  Trophy Points: 180
  Time for ccm to die. Good. JK ataondoka na ccm yake 2015. Thanks god.
   
 6. Abbasy

  Abbasy Senior Member

  #6
  Jun 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ndo dalili za mgonjwa kukata roho CCM bye bye
   
 7. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Jamani tuwaache wafu wazike wafu wao
   
 8. T

  Twasila JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,913
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  je Chatanda ambaye anatuhumiwa na uvccm naye ni moja wa wajumbe wa kamati ya maadili? Tujuzeni vijana.
   
Loading...