mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Kwa siku za karibuni CCM na serikali yake wamekuwa wakitumia sana hoja ya umaskini wa watanzania kuhalalisha hoja zao mbalimbali.Ukiongea la bunge live utasikia hatuwezi kutumia mabilioni kuonesha bunge huku wananchi hawana madawa hosp. sijui madawati n.k. Utawasikia kwenye majukwaa wakisema eti hali ya watanzania imekuwa duni kwa miaka mingi huku watu wachache wakijinufaisha na rasilimali za nchi.
Mtu mgeni akiwasikia wanavyozungumza anaweza kudhani CCM ni chama cha upinzani ambacho ndio kwanza kimechukua madaraka kuongoza nchi.
Eti leo ndio wamegundua kuwa maskini wa nchi hiii wamekuwa km wageni au wakimbizi kwenye nchi yao wenyewe. CCM na serikali yake wanalaumu tawala zilizopita kwa kuifanya nchi hii shamba la bibi wakati wote hao walikuwa sehemu ya tawala zilizopita na hatujawahi kuwaona wakilalamika au kuonesha nia ya kujiuzulu. Badala yake wamekuwa wakisifia sana viongozi na tawala hizo walizokuwa wanazitumikia.
Kama kweli CCM na serikali yake ya awamu ya tano inaamini kwa dhati na inamaanisha wakisemacho kwamba hii nchi ilifikishwa pabaya na viongozi waliopita, ilikuwa shamba la bibi basi na tuone viongozi wote walioshiriki kuifikisha nchi hapa wakiwajibishwa! Ina maana gani kulalamika kwamba nchi imekuwa shamba la bibi huku viongozi waliohusika wapo na hawafanywi lolote?
Je, hii si dhihaka kwa maskini walioteseka sana kwa ssbabu ya ubovu wa awamu zilizopita za serikali hii hii ya CCM? Hii nchi ilishaongozwa na chama kingine zaidi ya CCM?
Natoa wito kwa CCM na serikali yake iache kuwadhihski maskini kwa kuwatumia kipropaganda! Kuna watu wengi wamekufa kwa sababu ya umskini, wengine wamekuwa vilema, wengine wameshindwa kusoma, watu wanaishi kama mashetani kwa sababu ya hiki chama ambacho kimeshindwa kuwajali kws zaidi ya miaka 40. Leo eti mnajifanys mnawahurumia maskini? Eti mnawajali?
Acheni kuwatumia maskini kama mtaji wa kisiasa. Wajibisheni viongozi wote waliotufikisha hapa na kuahidi kuwa hakuna mtanzania atakayeishi tena kama shetani! La sivyo tutajua hizo sympathy zenu mnazojifanya kuonesha leo kwa maskini ni geresha tu ya kujipa political milleage.
Na hakika nawaambieni, km mnawakebehi maskini wa nchi hii wanaoishi kama mashetani, hamtaamini watakapowageuka watakapoona hali zao za maisha haziwi bora!!!!