CCM Acheni Kugombana, Fuateni Katiba Kupiga Kura

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,830
2,000
Chama cha zamani sana nchi hii kipo kwenye mtifuano. Sio siri tena hali ni tete na viongozi, wanachama na washabiki wa chama hicho kwa mara ya kwanza wako kwenye ugomvi mkubwa wa maneno na hila na sababu kubwa ni uchaguzi wa Mwenyekiti mpya.
Wapo wanao mtaka huyu mpya na wapo ambao sio tuu hawamtaki bali wanaona hana uwezo wa kukiongoza chama chao hivyo hayo mambo ya utamaduni weka pembeni.
CCM ndio chama kinacho unda serikali, wakitifuana ni hatari kwa nchi tofauti na vyama vingine.

Ni vyema wakaheshimu katiba yao na kuwapa uhuru wanachama uhuru wa kuchagua mwrnyekiti wao badala ya VITISHO kuwa asiyemtaka mgombea huyu afukuzwe au watu kuchafuana eti fulani ndio adui nk nk

Hivi uchaguzi wa wajumbe 3000 tu imekuwaje unawashinda? Au Demokrasia sio utamaduni wa chama.

Kwa mara ya kwanza ccm mtajenga picha kuwa na mwenyekiti ambaye ni kama kashikishwa usukani kwa nguvu.
ACHENI WANACHAMA WAPIGE KURA
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,462

Wapo wanao mtaka huyu mpya na wapo ambao sio tuu jawamtaki bali wanaona hana uwezo wa kukiongoza chama chao hivyo hayo mambo ya utamaduni weka pembeni.
CCM ndio chama kinacho unda serikali, wakitifuana ni hatari kwa nchi tofauti na vyama vingine.
Ni vyema wakaheshimu katiba yao na kuwapa uhuru wanachama uhuru wa kuchagua mwrnyekiti wao badala ya VITISHO kuwa asiyemtaka mgombea huyu afukuzwe au watu kuchafuana eti fulani ndio adui nk nk
Hivi uchaguzi wa wajumbe 3000 tu imekuwaje unawashinda? Au Demokrasia sio utamaduni wa chama.
Kwa mara ya kwanza ccm mtajenga picha kuwa na mwenyekiti ambaye ni kama kashikishwa usukani kwa nguvu.
ACHENI WANACHAMA WAPIGE KURA
Sijui uzoefu, sijui nini sijui hayo yote ni maneno tu.... kilichojificha nyuma ya hayo maneno ni woga wa kutumbuliwa. Nakuhakikishia CCM wengi wanajuta kwa sasa. Walidhani bwana mkubwa atakuwa ''mwenzao'' lakini mambo yameenda wasivyotegenea...

Na uenyekiti ndo rungu la mwisho atakalokabidhiwa bwana mkubwa ili auwe kabisa...

Huo utamaduni uliwezekanaje wakati uliopita na ushindikane leo..??

chama kina majibu makubwa makubwa sana ndiyo maana wanaogopa... kimsingi majipu ndo yanamkataa
 
Magimbi

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
1,419

Lakini hakunaga shida kama CCM tutafuata katiba yetu hapo maramoja au tuibadili ifuate utamduni. Tukifanikiwa kufuata katiba basi hata majirani nao watakuwa waumini wa katiba..
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,830
2,000
Uchaguzi wa mwenyekiti si ulishapita ile siku jina la mgombea lilipopatikana au?
Kama utamaduni huo ungekuwa umo katika katiba watu wazito kama Bulembo wasingetoa vitisho vya kufukuzana hadharani.
Katiba inataka Uchaguzi na kuna wanaoogopa uchaguzi
 
Chifu Nsyepa

Senior Member
Jul 9, 2016
106
225
Chama cha zamani sana nchi hii kipo kwenye mtifuano. Sio siri tena hali ni tete na viongozi, wanachama na washabiki wa chama hicho kwa mara ya kwanza wako kwenye ugomvi mkubwa wa maneno na hila na sababu kubwa ni uchaguzi wa Mwenyekiti mpya.
Wapo wanao mtaka huyu mpya na wapo ambao sio tuu hawamtaki bali wanaona hana uwezo wa kukiongoza chama chao hivyo hayo mambo ya utamaduni weka pembeni.
CCM ndio chama kinacho unda serikali, wakitifuana ni hatari kwa nchi tofauti na vyama vingine.
Ni vyema wakaheshimu katiba yao na kuwapa uhuru wanachama uhuru wa kuchagua mwrnyekiti wao badala ya VITISHO kuwa asiyemtaka mgombea huyu afukuzwe au watu kuchafuana eti fulani ndio adui nk nk
Hivi uchaguzi wa wajumbe 3000 tu imekuwaje unawashinda? Au Demokrasia sio utamaduni wa chama.
Kwa mara ya kwanza ccm mtajenga picha kuwa na mwenyekiti ambaye ni kama kashikishwa usukani kwa nguvu.
ACHENI WANACHAMA WAPIGE KURA
Naam Chakaza maneno yako kuntu kabisa, katiba ipo basis ifuatwe. Lakini mh kama katiba ya nchi inafanyiwa mizengwe je ile ya kijani?
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,462
2,000
Lakini hakunaga shida kama CCM tutafuata katiba yetu hapo maramoja au tuibadili ifuate utamduni. Tukifanikiwa kufuata katiba basi hata majirani nao watakuwa waumini wa katiba..
1. Why now?
2. Kwani hiyo katiba imetungwa baada ya bwana mkubwa kuwa na nafasi hiyo..??
3. Umewahi kusikia malumbano kama hayo kabla ya bwana mkuwa..??
4. Katiba ni kivuli mnachotaka kukitumia kumnyima jamaa uenyekiti, hamna njia nyingine...

NB: woga wa kutumbiliwa ndo chanzo cha hayo yote
 
Chifu Nsyepa

Senior Member
Jul 9, 2016
106
225
1. Why now?
2. Kwani hiyo katiba imetungwa baada ya bwana mkubwa kuwa na nafasi hiyo..??
3. Umewahi kusikia malumbano kama hayo kabla ya bwana mkuwa..??
4. Katiba ni kivuli mnachotaka kukitumia kumnyima jamaa uenyekiti, hamna njia nyingine...

NB: woga wa kutumbiliwa ndo chanzo cha hayo yote
adui yako muombee njaa! Halafu kaa pembeni angalia chezo litakavyosanuka
 
Drifter

JF-Expert Member
Jan 4, 2010
3,017
2,000
Sitegemei makada wa CCM wawe na tatizo na JPM kuukwaa uenyekiti kwani, kwanza, ni jambo lisilo na mjadala tangu alipoteuliwa kuwa mgombea urais. Halafu, cha maana zaidi, anaimarisha utekelezaji wa sera nzuri za CCM kikwelii hadi "wapinzani wamekosa hoja" kama mnavyodai. Msiomtaka ndio mliojenga utawala wa unafiki nchini. Kazi kwenu kwani msiemtaka ndio keshafika hivyo. Na mnaohangaika kujikomba safari hii mkae upandeupande. Upepo hautabiriki. All the best chama tawala.
 
Ndalama

JF-Expert Member
Nov 22, 2011
8,793
2,000
1. Why now?
2. Kwani hiyo katiba imetungwa baada ya bwana mkubwa kuwa na nafasi hiyo..??
3. Umewahi kusikia malumbano kama hayo kabla ya bwana mkuwa..??
4. Katiba ni kivuli mnachotaka kukitumia kumnyima jamaa uenyekiti, hamna njia nyingine...

NB: woga wa kutumbiliwa ndo chanzo cha hayo yote
Wajaribu wamnyime waone timbwili lake watatamani wangekuwa washirika wa UKAWA, "atakayejaribu kutukwamisha tutambomoa..."
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,830
2,000
Wajalibu wamnyime waone timbwili lake watatamani wangekuwa washirika wa UKAWA, "atakayejaribu kutukwamisha tutambomoa..."

Lakini kwani chama cha siasa huwa ni ubabe au ni ushawishi na hoja? Ubabe kama utakuwepo kwa vyama vichanga sio jambo la ajabu sana, lakini ubabe katika vyama vikongwe hapa Afrika kama CCM ni jambo la aibu sana na lisilotegemewa.
Mbona ANC inaweza kuruhusu demokrasia ndani ya chama chao lakini CCM inaogopa?
 
Ndalama

JF-Expert Member
Nov 22, 2011
8,793
2,000
Lakini kwani chama cha siasa huwa ni ubabe au ni ushawishi na hoja? Ubabe kama utakuwepo kwa vyama vichanga sio jambo la ajabu sana, lakini ubabe katika vyama vikongwe hapa Afrika kama CCM ni jambo la aibu sana na lisilotegemewa.
Mbona ANC inaweza kuruhusu demokrasia ndani ya chama chao lakini CCM inaogopa?
Mkuu kuna ukongwe na uzee....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom