CCM Acheni Kugombana, Fuateni Katiba Kupiga Kura

Lakini kwani chama cha siasa huwa ni ubabe au ni ushawishi na hoja? Ubabe kama utakuwepo kwa vyama vichanga sio jambo la ajabu sana, lakini ubabe katika vyama vikongwe hapa Afrika kama CCM ni jambo la aibu sana na lisilotegemewa.
Mbona ANC inaweza kuruhusu demokrasia ndani ya chama chao lakini CCM inaogopa?
Chakaza kama nchi inaendeshwa ki ubabe sembuse chama? Si waliipenda wenyewe waache waendelee kuisoma namba!
 
Chama cha zamani sana nchi hii kipo kwenye mtifuano. Sio siri tena hali ni tete na viongozi, wanachama na washabiki wa chama hicho kwa mara ya kwanza wako kwenye ugomvi mkubwa wa maneno na hila na sababu kubwa ni uchaguzi wa Mwenyekiti mpya.
Wapo wanao mtaka huyu mpya na wapo ambao sio tuu hawamtaki bali wanaona hana uwezo wa kukiongoza chama chao hivyo hayo mambo ya utamaduni weka pembeni.
CCM ndio chama kinacho unda serikali, wakitifuana ni hatari kwa nchi tofauti na vyama vingine.
Ni vyema wakaheshimu katiba yao na kuwapa uhuru wanachama uhuru wa kuchagua mwrnyekiti wao badala ya VITISHO kuwa asiyemtaka mgombea huyu afukuzwe au watu kuchafuana eti fulani ndio adui nk nk
Hivi uchaguzi wa wajumbe 3000 tu imekuwaje unawashinda? Au Demokrasia sio utamaduni wa chama.
Kwa mara ya kwanza ccm mtajenga picha kuwa na mwenyekiti ambaye ni kama kashikishwa usukani kwa nguvu.
ACHENI WANACHAMA WAPIGE KURA
Huo ushauri wape Chadema
 
moto utawaka tu kwenye ukumbi,wana ccm hatukubali kulazimishiwa mwenyekiti asiye na ozefu kwenye chama atatuharibia chama ni mtu wa visasi hajui siasa,
 
Kwa unafki uliojaa ccm, na Rais ameshamuhakikishia ulinzi JK basi hana budi kukabidhi uenyekiti kwa ngosha.

Ila jambo hili si zuri sana tukirudi kwenye fact, kazi ya chama ni kuisimamia serikali yake kutimiza ilani ya chama, sasa Rais anapokuwa ndio mwenyekiti wa chama moja kwa moja chama hakina tena uwezo wa kuisimamia na kuihoji serikali.

Ndio maana mtu kama Obama hana cheo chochote kwenye lakini mambo yanakwenda bila muingiliano.

Tatizo kubwa la ngozi nyeusi ni unafki.
 
Ya ccm waachie ccm
Katika hilo hatuwezi kuwaachia maana ccm ndio imeunda serikali na wakiendelea kugombana kwa hila na ubabe ugomvi huo unaingia serikalini na nchi inakosa mwelekeo. Huoni hata polisi wanawalinda huko Dodoma?
Kama wanataka kugombana watuachie serikali wagombanie uenyekiti wao kwanza.
Kuna dalili kubwa kuwa wanachama wengi hawakuridhika tokea awali na uteuzi wake kuwa mgombea
 
wewe siburi bifu la Lowasa na Mbowe wakati Lowasa atakapo taka akabidhiwe chama chake.

Chonga tu ya CCM, Chadema wanaharakati na Chadema wanasiasa watakapo nyukana, chadema masilahi na chadema asilia watakapo tifuana nani awe mwenyekiti, subira yatosha
 
ANC haijawahi ruhusu demokrasia hivyo unavyotaka kutuaminisha
Mfano mzuri anzia kisa cha MALEMA kufukuzwa uanachama
Lakini kwani chama cha siasa huwa ni ubabe au ni ushawishi na hoja? Ubabe kama utakuwepo kwa vyama vichanga sio jambo la ajabu sana, lakini ubabe katika vyama vikongwe hapa Afrika kama CCM ni jambo la aibu sana na lisilotegemewa.
Mbona ANC inaweza kuruhusu demokrasia ndani ya chama chao lakini CCM inaogopa?
 
ANC haijawahi ruhusu demokrasia hivyo unavyotaka kutuaminisha
Mfano mzuri anzia kisa cha MALEMA kufukuzwa uanachama
Wewe huna unalolijuwa, Rais Thabo mbeki pia ndio alikuwa Rais wa ANC muda wa uchaguzi ulipofika ndani ya ANC Jacob Zuma pia alichukuwa fomu kugombea na akamshinda Thabo Mbeki.

Thabo Mbeki akabaki na Urais wa nchi na Jacob Zuma akawa Rais wa chama. Hiyo ndio demokrasia.

Kama issue ni kumpa tu mezani Magufuli uenyekiti ni bora wangeokowa hizo billioni 4 wangeitana tu Lumumba kukabidhiana madaraka simple n clear.
 
ANC haijawahi ruhusu demokrasia hivyo unavyotaka kutuaminisha
Mfano mzuri anzia kisa cha MALEMA kufukuzwa uanachama
Suala la Malema kama unalijua vizuri yakikuwa masuala ya kinidhamu lakini kwenye mambo ya kisemokrasia ya kiuongozi hawana longolongo kama ccm ndio maana waliwahi kumng'oa Mbeki na akapoteza urais wa nchi kabla ya wakati. Kufukuzwa mtu kwenye chama kwa kukiuka maadili sio kukosa demokrasia
 
UCHAGUZI WA KUMPATA MWENYEKITI HAUPO .UTAMADUNI WETU NI KUPOKEZANA KIJITI.KWA HILI HATUHITAJI DEMOKRASIA.HAPA KAZI TU SIASA HADI 2020
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom