CCM Acheni Kugombana, Fuateni Katiba Kupiga Kura

Demokrasia ipi unataka ifwatwe labda ya jecha lakini hii tunayo ijua sahau
 
Kama utamaduni huo ungekuwa umo katika katiba watu wazito kama Bulembo wasingetoa vitisho vya kufukuzana hadharani.
Katiba inataka Uchaguzi na kuna wanaoogopa uchaguzi
Haya na nyie mmelipwa buku ngapi kuandika haya yasiyowahusu? Maana wakiandika wenzenu buku saba na wewe umelipw kiasi gani?
 
Wacha wachapeni Mkuu labda hili linaweza likawa chanzo cha kuleta ahueni kwenye nchi yetu ili huyu nanihii apunguze unanihii wake. Sasa sijui polisiccm kwenye mnyukano huu watakuwa kipande ipi au ndiyo watabaki wakitumbua mimacho tu

Chama cha zamani sana nchi hii kipo kwenye mtifuano. Sio siri tena hali ni tete na viongozi, wanachama na washabiki wa chama hicho kwa mara ya kwanza wako kwenye ugomvi mkubwa wa maneno na hila na sababu kubwa ni uchaguzi wa Mwenyekiti mpya.
Wapo wanao mtaka huyu mpya na wapo ambao sio tuu hawamtaki bali wanaona hana uwezo wa kukiongoza chama chao hivyo hayo mambo ya utamaduni weka pembeni.
CCM ndio chama kinacho unda serikali, wakitifuana ni hatari kwa nchi tofauti na vyama vingine.

Ni vyema wakaheshimu katiba yao na kuwapa uhuru wanachama uhuru wa kuchagua mwrnyekiti wao badala ya VITISHO kuwa asiyemtaka mgombea huyu afukuzwe au watu kuchafuana eti fulani ndio adui nk nk

Hivi uchaguzi wa wajumbe 3000 tu imekuwaje unawashinda? Au Demokrasia sio utamaduni wa chama.

Kwa mara ya kwanza ccm mtajenga picha kuwa na mwenyekiti ambaye ni kama kashikishwa usukani kwa nguvu.
ACHENI WANACHAMA WAPIGE KURA
 
Nadhani wale waliokuwa upande wa Mzee Mkubwa ndio hao wanaoshikwa na mchecheto, JPM ni jembe na mpini wake linakuja kulima ndani ya CCM na wengi watapotelea kusikojulikana, kwa sasa nataka nianze kuvaa Tshirt yangu ya chama niliyoinunua kwa pesa yangu mwenyewe, mafisadi yalikuwa yanatutia aibu hata tusiohusika na kutushusha morali, CCM inarudi kwenye misingi yake kama ilivyoasisiwa.
 
Back
Top Bottom