Salary Slip ,
..tishio nambari moja kwa ccm ni KIZAZI KIPYA.
..habari ya vyama vingi ilikuja wakati mimi sijafikia umri wa kupiga kura.
..na mimi kipindi hicho nilikuwa napinga mfumo wa vyama vingi.
..by the time vyama vingi vinaanzishwa nikaanza kuunga mkono nccr ile ya kina marando, tengambwage, mashaka nindi chimoto, bagenda, etc.
..alipoingia mrema nikawa-disappointed kwasababu niliamini alikuwa mtu wa hovyo-hovyo tangu alivyokuwa ccm.
..sasa tangu wakati huo mimi nimeamini ktk demokrasia ya vyama vingi.
..matamanio yangu ni kuwa chama kimoja kikiharibu basi kiondolewe kupitia sanduku la kura.
..hiyo ni experience yangu mimi niliyekuliwa wakati wa chama kimoja na " chama kushika hatamu . "
..vijana wa KIZAZI KIPYA ambao ni watoto wetu experience na makuzi yao yamejikita siasa za ushindani. Huwezi kuwalazimisha tu siasa za chama kimoja.
..pia kizazi kipya wanakuwa influenced na wanachoona ktk mataifa mengine. Sidhani kama watashawishika kirahisi kuuwawa kwa demokrasia ya vyama vingi.
..Kwa hiyo, kwa maoni yangu mfumo wa vyama vingi ni kama gurudumu nililoloko ktk mteremko. Wanachoweza kufanya CCM ni kupunguza spidi yake. Kubadilisha muelekeo wa gurudumu hilo sidhani kama ni busara.