‘’CCM ‘’ A Purposefully Scavenger | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘’CCM ‘’ A Purposefully Scavenger

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Jul 13, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  ‘’CCM ‘’ A Purposefully Scavenger

  Huwezi kuamini katikati ya Harakati za Wabunge wa Upinzani kuendeleza jitihada za kuikaba koo serikali. Ghafla CCM inachomoa turufu yake tata kufumba macho watanzania mpaka wachangiaji hapa JF.

  Kwa mwezi mzima habari itakuwa hii huku shauku, udadisi na tetesi zikimulika kundi la mapacha wawili waliosalia itakuwaje.

  Wakati haya yakiendelea, Agenda ya Umeme itasahaulika, Agenda ya kuunda Tume kuchunguza ubadhilifu katika Jeshi la Wananchi Tanzania litasahaulika, maneno ya kejeli ya Sitta yasahaulika na turufu nyingine nyingi za ukombozi wa Tanzania ambazo zimesikumwa tangu Bunge lilipoanza awamu hii.

  Lets get focused People
   
 2. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kaka utadhani tumefundishwa na mwalimu mmoja, na lecture ya leo ndio hii kwani nilikuwa nafikiria hivi hivi.

  Kwanza walidandia ujio wa tiba ya Babu wa Loliondo wakati UMMA umewasha moto kupinga malipo ya DOWANS. Matokeo yake mpaka leo hakuna watu waliohoji tena kuhusu hatma ya malipo yale. Kilichosikika ni SYMBION pekee. Na hii ya leo ni fursa by design ili kuzima moto unaotakiwa kuwaka bungeni kuhusu Mgao wa Umeme na utendaji mbovu.

  Ili kuwasahaulisha watu mambo ya misingi, basi tunatengenezewa HOJA za kujadili. Ni vizuri RA kaachia ngazi na tumeshajua hilo sasa turudi kwenye hoja zetu za msingi
   
 3. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Suprising na Vijana wa Magamba wamepost thread za kutosha zenye agenda moja na hundred of forum members wote wamenaswa kwenye hiyo thread...Woote wamesahau Agenda ya Msingi kirahisi kabisa
   
Loading...