CCM 2015 wajiandae kukabidhi nchi kwa UKAWA

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,904
4,050
NI habari njema kwa watanzania kwa kuzaliwa UKAWA kwani kwa hofu ya CCM kuanguka imekuwa kubwa mpaka wameanza kuweweseka.Ni kutokana na namna UKAWA walivojitambua na kukabiliana na propaganda za CCM, mfano CCM waliimaliza CUF kwa kusema ni chama cha waislamu na wakatumia staili ile ile kwa CHADEMA kuwa ni chma cha wakirsto.

Sasa UKAWA kudai watamsimamisha mgombea mmoja 2015, hiyo imekuwa shubiri kali kwa sisi kuimeza.

Ni ukweli huo tunawaomba CCM kukabidhi nchi hii kwa amani kwa UKAWA kwani wananchi hatutakubali tena wizi wa kura kwani miaka 50 ya mateso na shida sasa imetosha na sisi tunasema basi.
 
Unazungumzia ukawa gani ni chama cha siasa au genge fulani la wahuni unazungumzia kitu ambacho hakijulikani kinafanya kazi kwa usajili gani.
 
Jumuisha kura za wagombea wote wa upinzani mwaka 2010 halafu uone kama zitafika hata nusu ya mgombea wa ccm.
 
mjepo, we uko nchi gani? Iyani hujui UKAWA imekuja kuishika CCM? Pole sana unakuwa kma Maden?
 
Habari wana Jamii Forums.......

Kwa hali ya kisiasa inavyoendelea hapa nchini wakati huu inaashiria kabisa CCM imeshikwa pabaya na huenda wakakabidhi nchi kwa UKAWA kabla ya 2015.

Nayasema haya kutokana na CCM wenyewe kugawanyika katika makundi ya kuwania Urais hivyo kukosa mshikamano.

Kwa kuwa UKAWA ni kundi moja la Upinzani basi lina nguvu na ushawishi kwa wananchi baada ya CCM kuchokwa baada ya kushindwa kutimiza majukumu waliyopewa na Wananchi.

Kwa hali hii ya udhaifu wa CCM basi UKAWA kilichobaki sasa ni kuboresha daftari la kudumu la mpiga kura na kuhakikisha kanuni zote za uchaguzi zinazingatiwa ili kusiwepo na uchakachuaji wa aina yoyote unatokea.

Baada ya hayo machache basi Watanzania ni wakati wetu sasa kuwaunga mkono UKAWA ili tupate ukombozi wa kweli tuachane na mkoloni mweusi CCM.
 
Haya ni mawazo dhahania. Ndani ya UKAWA hakuna mtu wa kuweza kuisambaratisha CCM
 
Gongo ni mbaya sana. Ukichanganya na bangi ndo kabisaaaaa! Maana wale wavuta bangi wakipata stim wanakuwa na ndoto za kwenda ulaya. Ndo kama huyu mleta uzi
 
Jumuisha kura za wagombea wote wa upinzani mwaka 2010 halafu uone kama zitafika hata nusu ya mgombea wa ccm.

Kumbuka kura za ccm zilikuwa ni za kuchakachua,maana bwana mkubwa hakushinda,akapewa hisani na usalama wa taifa kwamba ni aibu kukaa kipindi kimoja tu madarakani wskati wenzake wamekaa vipindi viwili,hivyo basi wakamsaidia
 
Poleni sana! Jipeni moyo ila chadema haina mvuto tena ndiyo maana imejificha ktk koti la ukawa, nitasikitika sana baada ya uchaguzi wengi hamtaonekana jukwaani.
 
UKAWA watasambaratika kabla mwaka huu haujaisha.
Nchi haikabidhiwi kwa wahuni kirahisi rahisi hivyo.
 
Ukawa mnaweweseka saana, hata mapekezi mliyoyapata ktk ziara za ukawa bado inaonesha hoja ya ukawa dhidi ya serikali bado halijawa chachu ya kupata waungaji mkono wengi. Mmeunganisha vyama vinne pamoja na shura ya maimamu ila bado watu wanahudhuria ni sawa kabisa na mkutano wa cdm tu, wakati Kinana peke yake unaoneka kuimarisha chama kwa nguvu sana.
 
Upinzani wa CCM utatoka ndani ya CCM.


Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
CCM watajitahidi kutumia mbinu nyingi kujaribu kuusambaratisha umoja huu.
1. Kutumia Dola kujaribu kuzuia UKAWA wasifikishe ujumbe wa katiba kwa wananchi - mnaona wenyewe yanayotokea kule Kigoma
2. Kutumia mbinu ya kupenyeza Rupia.

Kama mbinu hizi zitashindikana, basi ni kweli anachotabiri mtoa hoja kwamba CCM iwe tayari kukabidhi nchi kabla ya 2015.

Sioni dalili ya DR. Slaa, Lipumba, Mbowe na Mbatia kuusaliti umoja huu, sioni dalili kabisa na kurudi nyuma. Watanzania tuwe tayari kwa mabadiliko 2015.
 
ccm ni chama cha wahuni na washenzi wakubwa hawawezi kuzuia nguvu ya ukawa
 
Gongo ni mbaya sana. Ukichanganya na bangi ndo kabisaaaaa! Maana wale wavuta bangi wakipata stim wanakuwa na ndoto za kwenda ulaya. Ndo kama huyu mleta uzi

Kama Nape na KINANA wakiinywa wanapata stimu kuwa Ccm bado inapendwa na watanzania kumbe sivyo.
 
Back
Top Bottom