CCK ije na jipya katika siasa za Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCK ije na jipya katika siasa za Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kalunguine, Feb 20, 2012.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  [TABLE="align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody, align: left"]CHAMA Cha Kijamii (CCK), kipya, kimeingia kwenye ulingo wa siasa mara baada ya kupata usajili wa kudumu mwanzoni mwa mwaka huu, na kufanya orodha ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu kufikia 19.

  Chama hicho ni kipya katika ulingo wa siasa na kwamba hakijafufuka wala kurithi mikoba ya Chama Cha Jamii (CCJ) ambacho Msajili wa Vyama, John Tendwa alikifuta kabla hata hakijapata usajili wa kudumu kwa kukosa sifa ya kuwa chama cha siasa nchini.

  CCK, ni sawa na mtoto aliyezaliwa wakati usio wake, lakini ana umuhimu wake kisiasa kutokana hali ya siasa iliyopo nchini, hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, lakini pia kutokana na Watanzania wengi kutokuwa kwenye vyama vya siasa.

  “Ni mwaka mmoja na nusu umepita tangu tuwakabidhi cheti cha muda CCK, na sasa Januari 27, mwaka huu tunawakabidhi cheti cha kudumu baada ya kutimiza masharti ya kuwa chama cha siasa nchini,” anasema Tendwa.

  Chama hicho, kimepata usajili baada ya kupata wanachama 200 katika kila mikoa 10 kwenye jamhuri ya Muungano; minane ikiwa ya Tanzania Bara na miwili ya Zanzibar, lakini mmoja lazima uwe wa kisiwa cha Pemba na mwingine uwe wa Unguja, katika hali ya kujenga muungano.

  Msajili wa vyama Tendwa anasema, sheria ya vyama inasema hakuna chama cha siasa kinachoruhusiwa kupewa usajili wa kudumu kama hakikupewa usajili wa muda, hivyo, CCK wanastahili kupewa usajili huo kutokana na kuwa Julai 23, mwaka jana, kilipewa usajili wa muda.

  Kutokana na hilo, Tendwa anasema kuanzia sasa CCK ni chama halali kina haki zote za kimsingi kama vyama vingine 18 vya siasa nchini kusimamisha mgombea kwenye uchaguzi mdogo katika majimbo yote yaliyo wazi nchini, likiwamo la Arumeru Mashariki baada ya mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Jeremiah Sumari kutangulia mbele ya haki.

  Mlezi wa vyama vya siasa, Tendwa amewakumbusha wajibu viongozi wa chama hicho na wanachama wa chama hicho pindi watakapokuwa katika kazi zao, kujali na kuheshimu misingi ya kuendeleza amani na utulivu nchini.

  “Viongozi wa siasa wenye dhamana kwa jamii wasiwe na sifa ya upandaji mbegu ya chuki kwa jamii, bali wajenge na kusimamia hoja na kuipa jamii nafasi ya kuchangia hoja hiyo, wasipende vurugu, watambue kuwa amani na utulivu ni rasilimali ya jamii,” anasema.

  Mwenyekiti wa CCK, Costantine Akitanda, alisema uamuzi wa kuanzisha chama hicho unatokana na kutokuwapo chama kingine cha upinzani nchini chenye itikadi na msimamo kama wa chama hicho. Anasema itikadi ya CCK ni “Uhafidhina wa kijamii na kiuchumi.”

  Mwenyekiti wa chama hicho, anaona kuwa kuanzishwa kwa chama chake ndio wakati wa harakati za ukombozi kuanza nchini Tanzania. Akitanda, ndiye mwenyekiti wa kwanza kukiongoza chama hicho ambacho kinaingia kwenye orodha ya vyama vyingi vya siasa, kuanzia chama tawala hadi vyama vya upinzani kuna mitafaruku inayoashiria baadhi ya wanachama kuvihama vyama vyao.

  Chama hicho kina Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar, Hamad Abushir, ambaye atakiongoza chama hicho na kusaka wanachama wake visiwani humo na kujiweka tayari kushiriki katika uchaguzi mdogo na mkuu ujao.

  Chama hicho kinaungana na vyama vingine vyenye usajili wa kudumu vya CCM, Chadema, CUF, TLP, UDP, UPDP, NCCR-Mageuzi, Jahazi Asilia, DP, NLD, Sau, NRA, Chausta, UMD, Tadea, Demokrasia-Makini, APPT-Maendeleo na Ford ambacho hakipo hai kisiasa.

  Usajili wa kudumu umetolewa kwa CCK baada ya chama hicho kutimiza masharti yaliyomo kwenye sheria namba tano ya uanzishwaji vyama vya siasa. Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Tendwa, amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha vyama hivi vinatenda siasa ili kuwapa Watanzania nafasi ya kutumia demokrasis ya vyama vingi.

  Pamoja na kuongeza idadi ya vyama vya siasa nchini, bado Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Tendwa, ametishia kuvifuta vyama vyenye usajili wa kudumu vilivyoanza kukiuka masharti na sheria zinazovipa uhalali wa kuwa vyama vya siasa.

  “Mpaka sasa kuna vyama vya siasa 19 nchini, lakini vilivyo vingi havifuati mashati na sheria ya kuwa vyama vya siasa. Vingi ni vya mashaka mashaka na hivi karibuni tutaanza kuhakiki kama vipo na tukivibaini tutavifuta,” alisema Tendwa.

  Tendwa anasema sheria inataka chama kiwe cha pande zote mbili za Muungano, lakini vingi havijatimiza sheria hiyo, hivyo atafanya ukaguzi kuona vyama gani havizingatii sheria na hivyo vitafutwa.

  Mwenyekiti wa Chama cha APPT-Maendeleo, Peter Mziray alipoulizwa anasemaje kuhusu kuingia kwa chama kingine katika ulingo wa siasa, anasema, hicho ni chama kama vyama vingine vichanga, wala si tishio kwa vyama vya siasa vilivyomo kwenye ulingo huo kwa zaidi ya miaka 15.

  Anasema, chama hicho kitakuwa na kazi kubwa kujijenga kuanzia kwenye mashina, matawi, kata, tarafa, wilaya, mikoa hadi taifani, hivyo hakitakuwa sawa na vyama vingine ambavyo vimeshiriki uchaguzi wa vyama vingi 1995, 2000, 2005 na 2010.

  Mziray ambaye alikuwa mgombea urais kwati tiketi ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha 2010, anasema CCK ni chama kipya ambacho hakina hata uhusiano wa karibu na CCJ, kwani waanzilishi wa CCJ wametawanyika na wengine wamerudi CCM na kwenye vyama vingine wanaendelea na majukumu yao kisiasa.

  Abdallah Kidenye, Mkazi wa Magomeni, alipoulizwa kama amesikia kuhusu kuongezeka kwa chama kingine kwenye ulingo wa siasa kinachoitwa CCK, amesema Watanzania wa sasa hawataki uwingi wa vyama wanachotaka ni kuboreshewa maisha yao ambayo yamekuwa magumu kila uchao.

  “Watanzania wanataka maisha bora, lakini hawataki idadi kubwa ya vyama vya siasa nchini, jambo ambalo ni muhimu katika kuhakikisha wanapata maendeleo na maisha yenye nafuu, badala ya kusajili vyama vya siasa.

  Mtazamo wa wachambuzi wa siasa nchini wanaona kuwa CCK, kimeanzishwa wakati mzuri kitakuwa na wakati mwingi wa kujiandaa kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa vyama vingi nchini, ambao ni wa tano ifikapo mwaka 2015.

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text, align: left"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text, align: left"] [TABLE]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody, align: right"] [/TD]
  [TD="class: kaziBody, align: center"] [/TD]
  [TD="class: kaziBody, align: left"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hicho chama kitakuwa bomba ikiwa SITTA hatakuwemo
   
 3. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hapa hakuna cha sita wala saba
   
 4. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  viva cck
   
 5. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Tupatie list ya Viongozi pls. Gari tumjue na Driver pls :plane:
   
 6. TASLIMU

  TASLIMU Senior Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nasubiri hiko chama,nigombee urais2020
   
Loading...