Carrier Background ya JK na matatizo ya nchi yetu

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,485
14,353
Wana JF, ifuatayo ni Career Background ya JK, Kuanzia mwaka 1988-2011 na kuendelea nimejaribu kuangalia baadhi ya majanga ya kitaifa yaliyosababishwa na raisi Kikwete katika kipindi chote ambacho amekua ni mtumishi wa serikali mpaka sasa alipo kama raisi wanchi hii..

CAREER BACKGROUND
2005-UP TO DATE The president of United Republic of Tanzania
1995-2005Minister for Foreign Affairs and International Cooperation
1995-2005Member of Parliament for Chalinze Constituency
1994-1995 Minister for Finance
1990-1995 Member of Parliament for Bagamoyo Constituency
1990-1994 Minister for Energy, Minerals and Water Development
1988-1990Deputy Minister for Energy and Minerals

Minister for energy and minerals -JK akaingiza nchini mikataba mibovu hasa ule wa IPTL ambao unaigharimu TANESCO na serikali kiasi cha millioni 300 kwa siku na uzalishaji wa umeme ni Megawati 60 tu, vilevile akaingiza mkataba tata na kinyonyaji wa bulyanghulu kule Kahama mkoani Shinyanga na inasemekana ndugu zetu wengi walipoteza maisha pale ( Mheshimiwa Tundu Lissu anao ule mkataba na aliuonyesha live siku ya uzinduzi wa kampeni za CHADEMA pale Jangwani mwaka jana) na mkataba huu utawanyonya watanzania kwa miaka 200 ijayo na kuacha wananchi wakiwa viziwi kutokana na kelele za mitambo, wagonjwa kutokana na sumu zinazotililika kutoka kiwandani mpaka kwenye vyanzo vya maji na mito kwa ujumla, magonjwa kutokana na kemikali na hewa chafu itokayo kiwandani, mashimo bila barabara nzuri, maji, vyuo, zahanati nk..

Minister for foreing affairs and cooperation -hapo ndipo mikataba mingi mibovu ilipoingia inchini inayosababisha wananchi wa taifa kuendelea kuiona nchi hii kama kiama, mikataba hiyo ni pamoja n KIWILA,DEEP GREEN, MEREMETA,TANGOLD

Member of Parliament –wananchi wa Chalinze na bagamoyo wameendelea kuishi katika umasikini uliopitiliza na wamekosa tumaini la kuja kuwa na maisha bora, hali halisi tunaiona kwa watu tunaopita pale Chalinze, vijana na wakinamama hawana ajira ya kueleweka wamekuwa ni wauza korosho, karanga, pipi, maji nk barabarani kwa abiria wanosafiri, wazee nao kazi yao ni kucheza bao na kunywa kahawa tu….

Minister of finance, alikaa mwaka mmoja tu siwezi kujua alileta positive au negative effect gani lakini naamini bado hakufanya chochote katika hiyo wizara maana tunashuhudia leo hii thamani ya fedha yetu imezidi kushuka dhidi ya fedha nyingine za kigeni….

The President of United republic of Tanzania, hapa madudu ndio hayasemeki mambo mengi sana yametokea kwa kipindi nadhani wengi wetu tunayajua.. RICHMOND mpaka DOWANS, EPA, Ugumu wa maisha, mfumko wa bei, kukosekana kwa umeme wa uhakika, milipuko ya mabomu katika kambi za kijeshi Mbagala na Gongolamboto...yapo mengi sana ambayo siwezi kuyaorodhesha na kumaliza yote hapa

Kwa kifupi tu hii ndio Career background ya JK, tangu amekuwa kiongozi serikalini yapo mazuri aliyoyafanya lakini kwa haya niliyoyaandika hapa ni mateso na maumivu makali kwa watanzania karibu wote, namalizia kusema kwamba sisi waajiri wake (mimi sikumpa kura yangu) tukiyaangalia yote haya aliyoyafanya huyu jamaa tumchukulie hatua gani au ni adhabu ipi itakayomfaa?
NAWASILISHA
 
Wana JF, ifuatayo ni Carrier Background ya JK, Kuanzia mwaka 1988-2011 na kuendelea nimejaribu kuangalia baadhi ya majanga ya kitaifa yaliyosababishwa na raisi Kikwete katika kipindi chote ambacho amekua ni mtumishi wa serikali mpaka sasa alipo kama raisi wanchi hii..

CARRIER BACKGROUND
2005-UP TO DATE The president of United Republic of Tanzania
1995-2005Minister for Foreign Affairs and International Cooperation
1995-2005Member of Parliament for Chalinze Constituency
1994-1995 Minister for Finance
1990-1995 Member of Parliament for Bagamoyo Constituency
1990-1994 Minister for Energy, Minerals and Water Development
1988-1990Deputy Minister for Energy and Minerals

Minister for energy and minerals -JK akaingiza nchini mikataba mibovu hasa ule wa IPTL ambao unaigharimu TANESCO na serikali kiasi cha millioni 300 kwa siku na uzalishaji wa umeme ni Megawati 60 tu, vilevile akaingiza mkataba tata na kinyonyaji wa bulyanghulu kule Kahama mkoani Shinyanga na inasemekana ndugu zetu wengi walipoteza maisha pale ( Mheshimiwa Tundu Lissu anao ule mkataba na aliuonyesha live siku ya uzinduzi wa kampeni za CHADEMA pale Jangwani mwaka jana) na mkataba huu utawanyonya watanzania kwa miaka 200 ijayo na kuacha wananchi wakiwa viziwi kutokana na kelele za mitambo, wagonjwa kutokana na sumu zinazotililika kutoka kiwandani mpaka kwenye vyanzo vya maji na mito kwa ujumla, magonjwa kutokana na kemikali na hewa chafu itokayo kiwandani, mashimo bila barabara nzuri, maji, vyuo, zahanati nk..

Minister for foreing affairs and cooperation -hapo ndipo mikataba mingi mibovu ilipoingia inchini inayosababisha wananchi wa taifa kuendelea kuiona nchi hii kama kiama, mikataba hiyo ni pamoja n KIWILA,DEEP GREEN, MEREMETA,TANGOLD

Member of Parliament –wananchi wa Chalinze na bagamoyo wameendelea kuishi katika umasikini uliopitiliza na wamekosa tumaini la kuja kuwa na maisha bora, hali halisi tunaiona kwa watu tunaopita pale Chalinze, vijana na wakinamama hawana ajira ya kueleweka wamekuwa ni wauza korosho, karanga, pipi, maji nk barabarani kwa abiria wanosafiri, wazee nao kazi yao ni kucheza bao na kunywa kahawa tu….

Minister of finance, alikaa mwaka mmoja tu siwezi kujua alileta positive au negative effect gani lakini naamini bado hakufanya chochote katika hiyo wizara maana tunashuhudia leo hii thamani ya fedha yetu imezidi kushuka dhidi ya fedha nyingine za kigeni….
The President of United republic of Tanzania, hapa madudu ndio hayasemeki mambo mengi sana yametokea kwa kipindi nadhani wengi wetu tunayajua.. RICHMOND mpaka DOWANS, EPA, Ugumu wa maisha, mfumko wa bei, kukosekana kwa umeme wa uhakika,yapo mengi sana ambayo siwezi kuyaorodhesha na kumaliza yote hapa
Kwa kifupi tu hii ndio Carrier background ya JK, tangu amekuwa kiongozi serikalini yapo mazuri aliyoyafanya lakini kwa haya niliyoyaandika hapa ni mateso na maumivu makali kwa watanzania karibu wote, namalizia kusema kwamba sisi waajiri wake (mimi sikumpa kura yangu) tukiyaangalia yote haya aliyoyafanya huyu jamaa tumchukulie hatua gani au ni adhabu ipi itakayomfaa?
NAWASILISHA

hapo kwenye red mkuu... hope ni career.

Ongea tusubiri achievements zake kutoka kwa wanazi... bila ushabiki.
 
Achievements:
  • kaitoa tz kutoka kule kuja huku tuliko
  • kaleta mauaji tz kule arusha na mbalali
  • kaleta mgao mkubwa wa umeme tz ambao haujawahi kutokea
  • kaahidi ahadi nyingi kwa watz wkt wa kampeni ambazo hazitekelezeki
  • kaonyesha kwamba huwa hasomi anavyopelekewa zaidi ya kusaini
  • kashindwa kukontrol mfumuko wa bei
  • .....
 
Back
Top Bottom