Carl ANCELOTTI Kaingizwa mkenge?

Unafananisha Tende na Mende...
Carlo Ancelotti amebeba pia hilo kombe akiwa kama mchezaji wa AC Milan dume kupata kutokea akiwa na manguli wenzie kama Mauro Tasotti, Paolo Madini, Alesandro Billy Costacurta, Franco Baresi, Colombo, Roberto Donadoni, Frank Rhiijkard, Marco Van Barstern, ruud Gullit na yeye Carlo Ancelotti...

Hakuna na hapatatokea kikosi kama hicho na pia hakuna na hakutatokea kocha kama Ancelotti.

Forza Milan
Numero uno Carlo

Nakubaliana na wewe kuhusu Carlo. Mengine nakuachia.

Carlo angepata clubs kama Man U au Arsenal ambazo zina falsafa ya ku-sustain technical bench kwa miongo kadhaa, angeweza kubeba idadi ya mataji waliyobeba Ferguson na Wenger combined. It is a FACT!
 
Gang Choba..kuwa na heshima kidogo..mi nijasema Carlo Ancelotti hafai..Carlo amekuwa kocha wa Chelsea, timu ninayoipenda. Nimesema inategemea unapenda nini..kwa takwimu wote sawa..Carlo kafanya yote hayo akiwa na timu moja tu! Ni sawa tu na Pep Guardiola..

Mourinho ameta katika nchi zaidi ya moja. Hata ingawa Carlo amechukua ubingwa wa ligi Uingereza na Ufaransa..kusema kwamba "Unafananisha Tende na Mende" si kauli unayopaswa kutoa "senior" kama wewe! Penda utakacho but respect my views!
 
Tukubaliane kutofautiana bila kugombana..hili ni jukwaa la wastaarabu au vipi mkuu?



:)
 
Huyu jamaa Madrid wamemuingiza mkenge?
alikuwa na uhakika wa kazi Madrid akatagaza kuacha PSG
sasa Madrid wanamchukua kocha wa Beyern naona
najiuliza huyu mzee ndo atakuwa kaingizwa mjini?


Hivi ukiisoma hii thread yako unajisikiaje?
Je unajuwa kuwa hakuna dhambi mbaya hapa JF kama Dhambi ya kukurupuka?
Je na wewe ni Great Thinker?
Unaonaje nikikununulia Kanga zilizoandikwa ''USIGEUZE SIKIO KUSIKILIZA YA WENZIO'' au nikununulie inayosema ''KUSHADADIA USILOLIJUWA NI SAWA NA KUINGIZA VOCHA BILA KUIKWANGUA''...?
 
Back
Top Bottom