Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 31,139
- 88,800
Wakuu, leo tudiscuss kuhusu mfumo mzima wa suspension.
Kwa uzoefu wangu, wengi tukisikia suspension tunachojua ni “shocks” peke yake, kumbe ni mfumo mkubwa unaojumuisha vitu zaidi ya kumi vinavyofanya gari lisitetemeke, liwe stable barabarani na kuzuia vibration isiingie ndani ya cabin.
Kwahiyo hii system ni moja ya sehemu muhimu zaidi katika comfort, handling, na usalama kwa gari na abiria.
KAZI KUU ZA SUSPENSION SYSTEM
Kama tulivyoainisha hapo juu, kazi kuu ya hii system ni pamoja na:
• Kupunguza vibration na mitikisiko kutoka barabarani especially zenye mashimo au rough.
• Kuhakikisha tyres zipo in contact na barabara wakati wote (for better traction).
• Kubeba uzito wa gari (body weight + abiria + mizigo).
• Kumaintain wheels alignment.
• Kufanya gari kua stable kwenye kona na breki (handling na balance).
COMPONENTS KUU ZA SUSPENSION SYSTEM
Bushes (Rubber Bushings)
Bushes ni vipande vya mpira vinavyotenganisha sehemu za chuma kama control arms, stabilizer bars, na mountings.
Zinachukua vibration na kuruhusu movement kidogo bila kugonga chuma kwa chuma.
Dalili za Bushes kuchakaa:
Suspension system ni tofauti na vitu vingine kwenye gari, ambavyo unabadirisha baada ya kilometa kadhaa. Mara nyingi components za suspension tunabadirisha baada ya kuona dalili za uchakavu.
Kwa bushes baadhi ya dalili ni:
• Kelele za kugongana vyuma unapopita kwenye mashimo au barabara isio smooth.
• Gari linavuta upande mmoja ata kwenye rami smooth.
• Steering inatetemeka ukiwa kwenye mwendo
• Uneven tire wear, either upande wa nje au wa ndani.
Bei za bushes ni ndogo sana. Huna haja ya kuvumilia mateso ya gari inayogonga gonga. Mifano:
• Magari madogo madogo (Vitz, IST, Fit, Axio): Tsh 10k–25k kila moja.
• SUV (Harrier, Rav4, Forester): 25k–50k
• German (BMW, Benz): 60k–120k (mfano kwenye picha chini ya BMW E46)
Brands sio case sana, ila zipo nyingi mfano RBI, CTR, Sankei, Lemforder (Germany) ambazo zitadumu zaidi. Ingawa sahivi zipo zisio na majina ila hazitakaa muda mrefu.
Tips unavyobadirisha:
Jitahidi ubadirishe kwa pair (kushoto na kulia) kwasababu ukibadilisha moja tu, balance inapotea, gari inakua kama imelalia kule kusikobadirishwa.
Shock Absorbers / Struts
Kwa leo tutaongelea hydraulic shock absorbers, hatutagusa kabisa air suspension za kishua, kwasababu ni magari ya kitajiri na machache yanakuja nazo.
Kwahiyo struts ndio zinacontrol “kuruka” kwa gari. Kwa ndani, zinakua na mafuta (hydraulic fluid) yanayozuia movement kubwa za spring.
Dalili za Uchakavu:
• Gari “linacheza” au “kuruka” likipita kwenye barabara isio smooth.
• Kelele kali uwa zinatoka (squeaky sound) esp ukipita barabara rough.
• Maji/mafuta kuvuja kwenye shock. Hii ni rahisi kuona ukiwa na tabia ya kufanya inspection.
• Tire kuisha vibaya, either upande au unakuta tyre la kushoto linaisha chap kuliko la kulia.
Bei za pair ya shocks itategemea na brand, aina ya gari na ni shocks za mbele au nyuma. Kwa mfano:
• Front shocks: 120k–250k (Japanese cars nyingi)
• Rear shocks: 90k–180k
• German: 250k–400k
Bei inaweza ikawa tofauti pia kutegemea na duka. Hii ni reference tu.
Brands famous hapa Bongo ni pamoja na KYB (Japan ambayo original ya Toyota), Monroe, Sachs, Tokico
Tips wakati unabadirisha:
Badilisha shocks kwa axle moja (zote mbili mbele au zote nyuma), sio moja moja.
Control Arms (Wishbones)
Control arms ni mikono ya chuma inayoshikilia magurudumu kwenye chassis.
Kazi yake ni kucontrol direction na movement ya wheel.
Dalili za Uchakavu:
• Gari halikai sawa kwenye alignment.
• Steering inavuta upande mmoja especially kwenye barabara flat.
• Kelele za kugonga chini ya gari.
Bei zake:
• Magari madogo madogo: 70k–120k
• SUV: 150k–300k
• German: 300k–500k
Ball Joints
Ball joints zinafanya kazi kama “kiwiko” (joint) kati ya control arm na wheel hub, kwa kusaidia magurudumu kuzunguka wakati unageuza.
Dalili za uchakavu:
• Kelele unapokata kona au unapopanda/kushuka tuta.
• Gari linaweza “kupoteza control” ghafla ambayo ni hatari ukiwa kwenye mwendo mkali.
Bei zake:
• 20k–60k kwa magari madogo.
• 70k–150k kwa SUV
• 200k+ kwa German
Ni vizuri kucheki ball joints kila 20,000km, kwasababu zinaweza zisioneshe dalili pindi zikiisha ukaishia kusababisha ajali.
Stabilizer Links / Sway Bar Links
Hizi uunganisha stabilizer bar na suspension ili kupunguza “kuyumba” kwa gari (tunaita body roll).
Dalili za uchakavu:
• Kelele za kugonga kwenye kona
• Gari kuyumba upande wa pili unapogeuka
Bei zake:
• 20k–50k (Japanese small cars)
• 80k–150k (SUV)
• 200k+ (BMW, Benz)
Mountings (Engine, Shock, Suspension Mounts)
Mounts zina absorb vibration kati ya engine, body na suspension.
Dalili za uchakavu:
• Vibration nyingi ndani ya gari
• Kelele wakati wa kuanza au ku-hold brake
• Engine inatikisika sana
Bei zake:
• Engine mount: 60k–150k
• Shock mount: 40k–100k
• German: 150k–300k
Tips kwa ujumla kuhusu Suspension service:
• Angalia kama bolts zote zimekazwa sawasawa wengine wanaacha lose.
• Usikubali kufungiwa shocks fake (za China) zenye rangi kali zinadumu miezi 3 tu tatizo linarudi.
• Ukibadilisha bushes au joints, fanya alignment kabisa.
• Kwa hizi barabara zetu, hakikisha unakagua suspension kila 20,000–30,000 km, au mara moja kwa mwaka.
• Kama unasikia milio ya ajabu ajabu kama “kukukuku” au “gogogo”, usipuuzie suspension ikifeli, inaweza kuharibu tires, axle, au hata kusababisha ajali.
• FWD cars (mfano Vitz, Fit, Axio suspension zake bei rahisi, mfano MacPherson Strut system.
• SUV na AWD cars (RAV4, Harrier, CR-V, Forester) zenyewe suspension zake ni complex (multi-link), gharama kubwa kidogo.
• BMW, Benz, Audi wao suspension zao ni za “comfort” sana lakini fragile kwenye barabara mbovu na engineering yake iko very complex, ndio maana bei za moto.
Kwenye suspension wakuu vitu ni vingi, mwingine anaweza kuongezea ila nimeona nigusie ivyo. Pamoja.