Kila mtu ana habari zake za ajabu ambazo watu wakizisikia kila wamwonapo usoni,hupatwa na mitazamo fulani kumhusu mtu huyo.Binafsi kila nimwonapo mtu huyu nacheka sana na kusema hao walio chini yake huko aliko "kazi wanayo".
Bila shaka wale wakimbizi wa Kagera wanayo ya kusimulia kuhusu huyu bwana.
Sitasahau siku alipomfuata headmaster wa Azania na kumlalamikia kuwa wanafunzi wa Azania wakiwa vituo vya mabasi na barabarani,wanawapiga sana wanafunzi wa kike wa Jitegemee baada ya kutokea ugomvi baina ya wanafunzi wa shule hizo mbili,ugomvi uliodumu takriban wiki nzima hadi serikali ilipoingilia kati.
Mnaamka asubuhi vituo vya Posta,kkoo na fire vimerembwa kwa chupi,madaftari,mabegi,sidiria za wadada wa Jitegemee waliokuwa wakienda shule asubuhi.Azania walikuwa na fujo sana kwa kweli!
Headmaster wa Azania akamjibu kuwa hawezi kufanya lolote kwa kuwa mambo hayo yanatokea nje ya shule,yeye hana uwezo nayo.
Massawe akamjibu "nashukuru bwana".
Akaitisha assemble ya wanafunzi wote wa Jite(walikuwa wengi sana),wote wakaondoka shift moja ya jioni.Jana yake aliwaambia waende shule wamejizatiti kivita,akawaamuru wabebe kila wanachoweza kubeba,panga,rungu,sime,nondo n.k
Kabla wanafunzi hawajatoka jioni,alituma kundi la askari waliovaa kiraia,wakaenda kukaa vituo vyote ambavyo wanafunzi wa Azania walipenda kukaa na kuvizia wadada wa Jitegemee na kuwapiga,kuwanyanyasa .
Ilikuwa rahisi kwa Azania kufanya hujuma maana walikuwa wakitoka mapema zaidi ya Jite na hivyo kujiandaa na kuweka mitego vituoni,wengine wakiwa wamevua uniform.
Halafu akawavisha askari wengine wa kike Jkt uniform za A level,wakatoka mapema na kufika vituo vya mjini wakionekana ni wanafunzi,Azania si wakaanzisha mambo yao,wasijue vituo vimejaa wajeda na sio abiria au wanafunzi pekee,mtitu ukalipuka,wakati ukiendelea madenti woote wa Jite wakaondoka kwa pamoja,wa kiume na kike wakitembea pamoja kuelekea destination zilizopangwa kiusalama kulingana na eneo mwanafunzi analokwenda,ambapo wengi walikuwa wakipita kkoo na posta,kama walivyoamrishwa na baba yao Massawe(huyu mtu alikuwa akisema neno tu,wanafunzi,walimu,askari wote wanalibeba zima zima,alikuwa kama mungu mtu pale Mgulani),wakazisimamisha daladala zinazopita nje ya shule yao,na kushusha abiria wote kwa nguvu,wakapanda na kuwapa makonda hela nyingi za nauli ya mtu mzima na zaidi,daladala kustukia mchongo zikawa zinaenda tupu hadi Jitegemee na kubeba wanafunzi,wakapelekwa mjini kwa makundi,wakakuta wajeda tayari wamemaliza kazi,wakakosa cha kufanya na kuanza kufanya fujo mjini,balaa likawa zito hadi shule zikafungiwa na wizara kwa muda.
Headmasters wote wakaitwa kujieleza,ndipo Massawe akatoa ya moyoni.
Tangu wakati huo sijasikia tena ugomvi mkubwa wa wanafunzi Dar kama enzi zile.
Serikali ikapata somo,nadhani na UMISETA ikapigwa stop manake inasemekana ugomvi ulianzia huko.
Ni mtu ambae ukimkabidhi kazi hakubali kushindwa,atatafuta namna ya kupata matokeo chanya kwa namna yoyote ile,jambo linalomfanya wengine wamuone jembe,wengine wamuone mjanja mjanja kupitiliza,wengine wamuone mpenda sifa,wengine wamuone opportunist,haijalishi unamwonaje,wewe jua tu kazi itafanyika kwa namna yoyote.
Pale Jitegemee alibuni miradi na kuwalipa walimu vizuri tu,hata wakati mwingine watu walijiuliza sana anatoa wapi uwezo wa kulipa walimu vizuri vile,wakawa suspicious nae ila angle moja tu aliwashinda mahasimu wake,kazi zilifanyika kwa mafanikio,aliendesha shule kwa mafanikio,na kila aliyekuwa chini yake alimfurahia na kumheshimu sana na kufanya kazi kwa bidii,hata wanafunzi na wajeda waliowahi kupishana nae na kukiona cha moto,leo ukiwauliza,watakwambia wanamheshimu na kumkumbuka sana.
Baadae alipandishwa cheo na kupelekwa makao makuu,huko nako akafanya vema tu,na kuanza safari ya kikazi iliyomfikisha hapa alipo.
Binafsi nilimjua zaidi akiwa Jitegemee na makao makuu kidogo.Sifahamu profile yake maeneo mengine nje ya hapo.
Tuliomjua huyu mtu,tulihisi mapema tu kuwa atafika mbali kikazi na kimaisha.
Ni mtoto wa mjini kweli,kamanda haswa,labda abadilike sasa,manake siasa hizi ngumu kweli.