Cameroon vs Chile live TV1

africa tuna vitu vya kujifunza sana kutoka kwa wenzetu. Wenzetu wakiwa uwanjani wanajua kitu kimojatu ni ushindi lakini sisi ni misifa na kukosa umakini.
 
nimalizie kwa shukrani kwa wenzangu wote tuliokua tunafatilia mpira huu kupitia TV1 na kuwapongeza kwa dhati kabisa TV1 wazee wa "toroka uje" kwa kutuletea burudani majumbani yetu.

Jamaa zetu wachina wa Startimes walipanga kutufyatua michuzi ili kuona matangazo haya lakini ninyi kwa uzalendo mkubwa mmetuletea Bure kabisa Asanteni Sana.
 
Mbona ipo poa tu...timu nyingi zilikuwa zikionewa kwa kukosekana uamuzi makinifu...

Sheria ya ajabu niliyopata kuiona na bora ilifutwa haraka ni ile ya goli la dhahabu daaah...(ingawaje niliipenda wakati mmoja tu ambapo Senegal ilimtwanga Denmark na kuichukia zaidi hatua iliyofuata kwa Turkey kuitoa Senegal...)
Mkuu ile sheria ya goli la dhabu ilikua inang'ata kotekote mkuu.Ingawa iliwahi kunitoa machozi mwaka 1997!!dakika 30 za nyongeza jamaa wakamaliza game dk ya 8 tuu!
 
Aise poleni sana Cameroon,,haikuwa bahati yenu. Pamoja na kubebwa kote huko lakini mmeshindwa hata kifuta machozi tu!!!!!!!
 
Back
Top Bottom