Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,427
Abiria 36 wametekwa nyara na watu wenye silaha kwenye barabara kuu kati ya Buea na Kumba, kusini magharibi mwa Cameroon katika eneo ambalo wakaazi wake wanazungumza lugha ya Kiingereza.
Walioshuhudia wanasema katika tukio hilo la Jumanne, mabasi mawili yaliondoka Kumba na kwenda Buea na kuzuiliwa na watu wenye silaha kwenye kijiji cha Ediki. Abiria wote walilazimishwa kushuka kwenye basi na kukabidhi vitambulisho vyao, na kupelekwa msituni na sehemu isiyojulikana
Wakuu wa eneo hilo wanasema usafiri kwenye barabara hiyo umesimamishwa, na kazi ya kuwatafuta mateka hao imeanza.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na uasi katika eneo la watu wanaozungumza Kiingereza nchini Cameron. Waasi wanaotaka kujitenga wanalalamikia ubaguzi unaotendwa na serikali ya Rais Paul Biya wa nchi hiyo ambayo lugha yake rasmi ni Kifaransa.
Rais Paul Biya wa Cameroon
Harakati za kutaka kujitenga eneo linalozungumza Kiingereza nchini Cameroon zilianza mwaka 2017 baada ya serikali kukandamiza maandamano ya amani.
Wazungumzaji wa Kiingereza wanaunda karibu asilimia 20 ya wakazi wote milioni 20 wa Cameroon.
Wazungumzaji hao wa Kiingereza wanalalamika kuwa wananyanyaswa na kutengwa na serikali kuu na wananyimwa haki zao kama raia wa Cameroon hivyo wanaona ni vyema wapiganie kujitenga