Naiomba kampuni ya simu ya Tigo iwe makini sana inapompatia mteja wake caller tone hasa zile za imani. maana unaomba caller tone ya kiisilamu unawekewa kwaya ya kanisa au unaomba nyimbo ya kanisa unawekewa qur an sasa tunawaomba muwe makini sana hasa kwenye hizi huduma zenu musituudhi wateja wenu tutawakimbia kwa uzembe wenu
Mimi hawa jamaa wanaboa!unawekewa caller tone!ukitaka kujitoa hakuna option!je hiyo ni sawa?hivi ukitaka kujitoa unafanyaje?manake inakua kero mwenyewe ninayo caller tone ya quran hapa hadi aibu!mwenyewe nilikua sijui ila kuna mtu aliniambia mbona simu yako inasoma aya za quran?lol sasa sijui unatoaje!nikaweka ingine sasa hv zinapokezana!
Ni kawaida yao hiyo huduma unailipia. Kila call inakuja na tone yake. Ipo ile ya duuum duum ya tangazo lao Tigo inakera sana.
Huduma hiyo peke yake inattosha kuchangia madawati au kupeleka walimu school za ward.
Wateja 2m zidisha kwa 27 tshs. Kila siku. Unafikiriaje hapo?
Hata mie nilipigiwa simu na prospective employer akaniambia hivi wewe watu wote ni wapenzi wako, kwani tone ilikuwa inaimba ''fall in love'' Hawa jamaa wanaweza kukubadilishia caller tone wanavyotaka. wanaboa kweli
Wakati mwingine hata hujaomba wanakuwekea, hasa unapokuwa hauko kwenye mtandao, aliyekupigia anawekewa tangazo kisha tone zao. Mie ni mteja tangu 2001 kwa namba ileile, nawaomba wasinichefue, la sivyo nitahama