Calabar, Nigeria: Wanajeshi wakichoma moto kituo cha polisi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
ba9f0e75c206d8b24478831f03bd58d0.jpg
Ripoti kutoka nchini Nigeria zinasema Maafisa wa Jeshi la Wanamaji wamevamia na kuchoma moto kituo cha polisi mjini Calabar kusini mwa nchi hiyo

Maafisa wa polisi watatu wanaripotiwa kuuawa ingawa bado haijafahamika vifo hivyo vimetokeaje

Tukio hilo limetokea kufuatia mabishano yaliyotokea kati ya wanajeshi hao wa majini na maafisa wa polisi

Ripoti zaidi zinasema maafisa hao wa jeshi la maji walirudi tena katika eneo hilo wakiwa wamejiimarisha zaidi na kuanza kushambulia kituo cha polisi, na kuchoma moto

Chanzo: BBC
 
Akili kukosekana kichwani, ukiona kazi ngumu acha tafuta fursa nyingine, sasa askari mnapigana wenyewe kwa wenyewe sindo kukosa akili huko.
Askari wote ni muhimu sio polisi wala jeshi la wananchi, kila mmoja anaplay role muhimu katika eneo lake.
Tatizo kuna wenye vichwa vya kuku jeshini/polisi ambao hudhani nafasi zao ni muhimu kuliko wenzao
 
Ushauri wangu.. Na wao polisi waende wakachome kambi ya jeshi walau moja ili kubalance tukio!
 
Back
Top Bottom