CAG - Ufisadi mamilioni wa kutisha Chuo cha Mabaharia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CAG - Ufisadi mamilioni wa kutisha Chuo cha Mabaharia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Apr 26, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  CAG, Ludovick Utouh

  Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG), Ludovick Utouh, amebaini matumizi mabaya katika Chuo cha Mabaharia cha Dar es Salaam (DMI) ambapo Mwenyekiti wa baraza la chuo alijilipa Sh milioni 51.8, kama malipo ya kazi, mafuta na posho za mwezi bila kuidhinishwa na bodi.
  Aidha, Sh. milioni 12 zimelipwa kama posho kwa maofisa wa Wizara ya Uchukuzi bila bodi ya chuo hicho kuidhinisha.

  Kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni mwaka jana, iliyotolewa CAG, jumla ya Sh. milioni 83.96 zimetumiwa na chuo hicho kama malipo ya kazi na posho nyingine bila kuidhinishwa na bodi. Licha ya mwenyekiti kulipwa mamilioni hayo, Sh. milioni 2.6 zililipwa kama posho ya kikao kwa wahasibu wa chuo hicho ingawa hawakuhudhuria mkutano.


  Alisema Sh. milioni 10.4 kati ya fedha hizo zililipwa kama posho kwa wafanyakazi wa chuo hicho katika kikosi kazi kilichoundwa kwa ajili ya kupandisha na kutengeneza mtaala wa chuo hicho Juni, 2009. Watumishi hao hawakuwa sehemu ya timu waliohusika katika zoezi hilo.


  Aidha, Sh. milioni 6.95 zililipwa kwa watumishi wa chuo hicho kwa kutumia viwango ambavyo havikudhibitishwa na bodi na hawakuwa sehemu ya timu iliyoandaa mikutano kati ya Machi 9 mwaka jana na 11 Machi mwaka 2011 kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za mahafali ya saba ya chuo hicho. Kadhalika, Sh. milioni 385 zilitolewa Wizara ya Uchukuzi kwa ajili ya kulipa madeni hazikutumika ipasavyo. Hata hivyo, alisema katika ukaguzi walibaini Sh. milioni 205.8 ndio zilitumika kukamilisha ulipaji wa madeni huku fedha zilizobakia Sh. milioni 179.3 zikitumika katika shughuli nyingine ya chuo kinyume na madhumuni ya ufadhili huo.


  Utouh alielezea malipo ya viwango vya mishahara kwa watumishi wa chuo hicho ambao hawakudhibitishwa na baraza la chuo. Alisema malipo ya mishahara kwa watumishi 12 wa chuo hicho katika kiwango cha PDSS 5 na zaidi yalilipwa bila kuthibitishwa na baraza . Hata hivyo, alisema haikueleweka kama watumishi hao walipandishwa vyeo kwa viwango vya mishahara hiyo.


  Utouh pia alisema katika ukaguzi huo walibaini Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (DFA) wa chuo hicho kulipwa kinyume na viwango vya mishahara ya utumishi wa chuo hicho. Alisema analipwa PHTS badala ya PGSS kama ilivyoainishwa katika viwango vya malipo vya chuo hicho. Katika muamala huo, DFA amelipwa malipo ya ziada ya jumla ya Sh. milioni 16 katika kipindi cha kati ya Julai 2009 na Januari, 2012.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kila mahala ni ufisadi tu? Nani atapona sasa?

  CAG nenda kaangazie idara kama PCCB tuone nako kuna nini huko.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Asiiruke Magogoni, lazima pale kuna shimo kubwa lililotokeza baharini, kama mnakumbuka pale kuna bomba kubwa limetokeza baharini eti la maji taka, huenda linapitisha madudu hadi ufichoni baharini.
   
Loading...