Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,634
- 1,770
Doh! Kwa hiyo GDP yetu ni kama dola 47.6 bilioni tu, ji nchi lote hili! Pato la Taifa tuko nchi ya 10 hivi Afrika, lakini kwa pesa za kila mtu mfukoni tunapitwa hata na Lesotho, Swaziland, Zambia, Zimbabwe na usiseme Botswana au Namibia.....wako mbali sana. Rwanda na Comoro wanatufukuza! Loh, jamani tuko maskini wa kutupwa, halafu hawa ma dead brain kazi kukimbizana na upinzani na kutumia mapesa kwenye uchaguzi wa kupanga! Wana huruma kweli hawa na wananchi?