CAG office, Audit zao halmashauri zina quality kufichua kila kitu?

shaurimbaya

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
1,915
2,329
Habari wadau?

Kuna kitu najiuliza mnaojua mnisaidie..

Je, audotors wa cag wana nguvu ya kufichua makosa na ufisadi wote nchini kwa uhuru bila kuhofia maisha yao??

Maana nikifikiria audit kama ile ya EPA iliyofichuliwa na ernst and young UK nazani ilikuwa rahisi kufichuliwa sababu auditors wengi waliofanya kazi sio wazawa. So wakaandika kila kitu kwa uhuru na hata wakati ripoti inatoka wao wameshasepa kurudi makwao.Hakuna wa kuwatisha, kuwadhuru au kuwaonga sababu huwajui??

Na hata kwa mwajiri wangu kumekuwa na mchezo wa kuleta watu wa secondment wa kpmg, ernst and young au pwc kuja kugagua sehem wanapohisi kuna magumashi.. ili kuepusha usalama wa maisha ya wakaguzi au kuwaonga.

Na wanafanikiwa sana maana wageni wanaandika kila kitu walichogundua bila hofu na ripoti inatoka wao wameshasepa makwao huwaoni tena.


Huwa nawaza ikatokea siku audit zote halmashauri au ofisi za uma zikakaguliwa na watu tusiowajua na walio huru itakuwaje?

Scandal kama Lugumi ile au escrow wapewe kazi watu huru itakuwaje hiyo ripoti.


Au halmashauri ili iende deep audit ya independence auditors itakuwaje?

Nina imani kuna vitu watu wa CAG hawavisemi kuhofia maisha yao na rushwa wanazopozwa maana asingepona mtu.
 
Soma kisa cha Arthur Anderson katika ukaguzi, utagundua independence ni tatizo kubwa si kwa CAG tuu ni duani kote....
 
Nikupongeze tu kwa mada uliyoianzisha ya kubainisha hatari waliyonayo wakaguzi wetu wengi na mwishowe huishia kupokea rushwa kutokana na hofu ile.
Mimi binafsi nitasema muda itakapowadia!
 
CAG Apewe rungu la papo kwa papo kila anapogundua MAKOSA awakabidhi POLICE kama hivi sawa WAKUU WA WILAYA wanavyofanya kila wanapohisi figisufigisu.Hata mwanzoni wa miaka baada ya kupata UHURU kila MKAGUZI Anapifika kumkagua BWANA FEDHA akikuta hata senti Tano imekosekana Hamwambii Bwana Fedha arejeshe badala yake anawakabidhi POLISI Na mida hiyo hiyo analetwa BWANA FEDHA Mwingine Hilo ndiyo DAWA Ima hawa watu wataendelea kucheza vivyo hivi kila kukicha Na CAG Kuendelea kuandika vitabu na vitabu TUTAFAKARI
 
Kumbuka Tegeta escrow ilifanywa na CAG.
Ila ni shida kufanya audit kwenye mazingira haya.MUNGU awajalie wakaguzi wanaotenda haki.
 
ripoti ya escrow ilikuwa mbovu sana.. hata ripoti ilishindwa kueleza fedha za uma au za watu binafsi.. haikuwa ripoti nzuri kama ya epa and the like.. very straight report.. ila escrow ilikuwa na uoga mwingi hata waliochota hela stanbic hawakutajwa mpaka leo...

ingekuwa wageni au watu wasio waoga wamekagua na kuandika ripoti ya escrow tungekimbiana nchini humu... hakuna ambacho kingefunikwa

Kumbuka Tegeta escrow ilifanywa na CAG.
Ila ni shida kufanya audit kwenye mazingira haya.MUNGU awajalie wakaguzi wanaotenda haki.
 
Back
Top Bottom