CAG ni Mkaguzi tu, si MDHIBITI

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
7,435
7,105
Kwa ripoti yako kila mwaka kugubikwa na madudu huko Halmashauri na taasisi za Serikali na hakuna kinachofanyika baada ya hapo mpaka uje na ripoti nyingine (mwaka unaofuata) ya madudu yale yale ama kuzidi! Ni sahihi kukuita wewe ni MDHIBITI? kwa lipi? Nafikiri ungebaki na AUDITOR GENERAL (AG) tu ingekuwa poa mno.
 
nakubaliana na mtoa mada, CAG ni Auditor tu hadhibiti chochote madudu yale yale ya miaka yoooote, hatua sifurii. Pengine iwepo CONTROLLER of BUDGET (independent office/institution) ili twende sawa.
 
Huyu si ndio anawawadhibiti wahasibu?
Kwa nini hawafukuzwi kazi hao wahasibu ili wawekwe wengine waangaliwe kama kuna mabadiliko na endapo nao watafanya madudu nao wapigwe kibuti?
Waliofuja pesa ni wale wale wa tangu awamu ya tatu mpaka leo!
Nani anawabeba?
 
CAG ameanza lini kudhibiti wahasibu serikalini? mwenye hizi updates atujuze.


Nimeuliza tu mana maauditor mara nyingi wanakagua vitabu vya wahasibu.

Mahesabu ya serikali bila shaka ni pesa . Na pesa zinawahusu wahasibu!

Tuelimishane hapo mkuu.
 
1000 digits mimi kitaaluma si mhasibu ila ninachoelewa mhasibu anawajibika kwa mwajiri wake tu. Ingawa pia najua wana chombo cha NBAA amabacho hakina uhusiano wa moja kwa moja na CAG
 
yaani mpaka raha likiisha hili itakuja ishu ya bajeti nalo littapita basi maisha yanaendelea
 
Immigration wanaingiza Dola za kutosha kwa siku kwa malipo ya PERMIT (Residence), Visa on Arrival. Patajwe ni kiasi gani kinaingia ili tujue wananchi. Kama Polisi wanatangaza wameingia ngapi kwa mwezi kwenye faini, iweje immigration wao wanapiga kimya?
 
Back
Top Bottom