CAG: NHIF ilitoa mkopo kwa Serikali bila nyaraka wala dhamana ya mkopo

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg

Hii kitu ilisemwa sana Bunge la bajeti 2015,kwamba mifuko ya jamii pamoja na mfuko wa Afya wa Taifa.Taasisi hizi zimekuwa kama "zinatapanya" michango ya wanachama wake bila taarifa rasmi kwa wadau.

Mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa inatumia pesa kujenga miradi mikubwa na faida yake haionekani kwa wachangiaji,matokeo yake kwa sasa mifuko mingi imekuwa na ukata mkubwa sababu serikali baada ya kukopa imeshindwa kulipa deni.

Kwa sasa baadhi ya hospitali za binafsi zinagoma kupokea kadi za NHIF sababu wanacheleweshewa malipo yao na hivyo kuwa na malimbikizo ya deni,hali hii inatokana na NHIF kukabiliwa na ukata sbb ya kuikopesha serikali.

NHIF extend loan to UDOM without proper documentation

National Health Insurance Fund (NHIF) advanced a loan of Sh44.29 billion to the University of Dodoma (UDOM) to construct a Medical Centre without a written documents, the Controller and Auditor General (CAG) has found out.

It was established in an audit for the year which ended June 2015/16 that there were neither written agreement between the two institutions nor a Government guarantee for the said loan

. NHIF extend loan to UDOM without proper documentation

Chanzo:Gazeti la The Citizen
 
Yaani kweli unatoa bilioni 44 bila mkataba? Hata mwendokasi Tsh 650 wanatoaga tiketi!!

Kila mwaka wa uchaguzi huja na lake jambo,kipindi kile ulikuwa EPA

Mbaya zaidi sasa hela ziko benki kuu,sijui usalama wake ukoje,napendekeza mifuko ya pensheni iwe inatoa taarifa ya hali yake kifedha kwa wanachama,kila mwezi.

PSPF ni de facto bankrupt,chanzo ni serikali kuikopa usiku na mchana,inadaiwa kwamba PSPF huchelewesha malipo mpaka inabidi siku ya kulipa wamlipe mtumishi na mishahara ya kipindi walichomcheleweshea malipo

Hela za haya mashirika zisikae Benki kuu, hizo sio hela za serikali,ni hela za wachangiaji,zitolewe Mara moja kabla hazijaanza kudokolewa wakalipwa wajenzi wa reli
 
[HASHTAG]#okoamifukoyapensheni[/HASHTAG]
[HASHTAG]#fukuzamchwa[/HASHTAG]
 
Tatizo la hii inchi kila kitu ni siasa ata visivyohitaji siasa.
Mbaya zaidi siku hizi ata watu wenye taaluma zao wanafikili kwa kutumia matumbo.

Tanzania bado tuna safari ndefu Sana ata 2020 hakuna tutakachokibadilisha.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kaka hi kitu serikali inachofanya kwa hii mifuko ya jamii na hata hii mifuko ya bima ya afya ambapo serikali inajua kabisa hii mifuko ni kwa faida ya wachangiaji, ina tufanya wanachama na wachangiaji wa hii mifuko kuhuzunika sana

Hebu fikiria mfuko wa WCF (Workers compensation Fund) inakuwaje wachangiwaji ambao ni waajiriwa wa makampuni yanayochangia hawana number ya uwanachama hii ni kama bima, WCF wangetoa kard kwa kila mchangiwaji ili ikitokake kaumia kazini kusiwe na usumbufu wa kupata huduma iliyokusudiwa na mfuko huu. Hii WCF nayo siku za usoni utasikia nao wanafanya mambo kama yanayofanywa na hii mifuko ya hifadhi ya jamii.
 
Kaka hi kitu serikali inachofanya kwa hii mifuko ya jamii na hata hii mifuko ya bima ya afya ambapo serikali inajua kabisa hii mifuko ni kwa faida ya wachangiaji, ina tufanya wanachama na wachangiaji wa hii mifuko kuhuzunika sana

Hebu fikiria mfuko wa WCF (Workers compensation Fund) inakuwaje wachangiwaji ambao ni waajiriwa wa makampuni yanayochangia hawana number ya uwanachama hii ni kama bima, WCF wangetoa kard kwa kila mchangiwaji ili ikitokake kaumia kazini kusiwe na usumbufu wa kupata huduma iliyokusudiwa na mfuko huu. Hii WCF nayo siku za usoni utasikia nao wanafanya mambo kama yanayofanywa na hii mifuko ya hifadhi ya jamii.
Mfuko wa Bima ya Afya wao wanaweza kukukata hata miaka kumi,hawahangaiki kujiuliza mteja wao fulani mbona hana kitambulisho/hatujawahi kumpa?

Nadhani hawana hata database ya watu waliowahi kuwa na vitambulisho wakawatambua,na baadae wakawajua watu ambao hawajawahi kuchukua kitambulisho ili watu wa customer care wawa trace,ofisi zao za mikoani nyingi ni kama mapagala tu,hovyohovyo,hazijitegemei kila kitu mpaka wakwambie wanawasiliana na makao makuu
 
Tuna bunge ambalo ni kibogoyo kwa msingi ya Katiba ya nchi yetu. Hata kama wabunge wana nia ya kuibana Serikali Katiba inawawekea munda. Kwanza kipengere kinacholazimisha Mbunge kupoteza ubunge wake akitofautiana na chama chake Kifutwe, halafu tuone kama madudu haya yataendelea kujirudia!!
 
Back
Top Bottom