CAG Mfano wa Kuigwa kwa Wasomi

CAG Mfano wa Kuigwa kwa Wasomi

Kabla ya kualikwa mezani wanakuwa timamu, wakialikwa tu na ufahamu unapotea.

Kama yule aliyekuwa na Zito wakipambana, mara ghafla naye kachomoka na kufuata MKUMBO.
 
Una hoja ya msingi. Lakini wasomi kuna wakati wakati wanatakiwa kuchagua kati ya kutunza taaluma zao au kuwa watumwa wa matumbo yao.

Tijiulize, ni yeye tu ndiye mwenye kinga? Vipi kuhusu jaji mkuu? Vipi kuhusu majaji?
Naamini hawa majaji wanalindwa na katiba kinachobaki ni utashi wa kila mmoja. Kama unakumbuka Tundu Lissu aliongelea matatizo yaliyokuwepo kwenye kuchagua majaji, kama mtu akipewa cheo hicho kwa style aliyosema TL usishangae akawa anarudisha fadhila kwa ku abuse offisi zao, lakini yule anaepata kwa kustahili anaweza akafanya kazi kama huyu CAG.
Hawa wengine wenzangu mimi ukikataa uteuzi ujue utashughulikiwa tu, ukikubali uteuzi unajua unatakiwa ufunike kombe, hapo lazima uwe na jeuri kusimamia unacho amini. Lakini pia wako wale ambao wao wanasaka hizo nafasi kwa udi na uvumba na kundi hili ni hatari kabisa.
 
Jaji mkuu naye tatizo ni nini?
Huenda anafunika kombe ili mwanaharamu apite au anarudisha fadhila. Huyu alitegemewa au tunamtegemea ajiweke mbali afanye kazi zake kimya kimya.
 
Back
Top Bottom