CAG Mfano wa Kuigwa kwa Wasomi

CAG Mfano wa Kuigwa kwa Wasomi

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,940
Mwakajana mbunge Msukuma aliwahi kueleza Bungeni kuwa mambo makubwa katika nchi hii yamefanywa na watu wasio wasomi, watu walioshia darasa la 7 ukilinganisha ba wanaojiita wasomi. Aliyaongea hayo wakati akipigania watendaji wa vijiji walioishia darasa la saba warudishwe kazini.

Pamoja na ukweli kuwa Mbunge Musukuma mara nyingi kauli zake hukosa weledi lakini katika hili kwa kiwango fulani alikuwa sahihi.

Kati ya watu ambao hawana mchango mkubwa katika Taifa hili ni hawa wanaoitwa 'wasomi', hapa ndiyo tunawapata wale wenye titles za Dr. na Prof.

Tumeshuhudia, mara kadhaa, hawa wanaoitwa wasomi, wakiteuliwa kwenye nafasi za uongozi katika serikali. Wengi wao walipoingia huko waliishia kuwa walamba viatu vya wale waliowateua na hakuna chochote kipya walichokipeleka badala ya baadhi yao kwenda kudhihirisha unafiki, woga, ukigeugeu na kukosa misimamo hata katika mambo ambayo waliwahi kuyanena kwa vinywa vyao wenyewe.

Sifa kubwa ya msomi wa kweli ni kujitambua, kujiamini na kusimama katika yale unayoyaamini.

Leo hii tujiulize, ni Doctor (PhD) na Professor (ukimwacha Musa Assad) gani ambaye daima amewahi kusimama katika yale anayoyaamini bila kugeuka na kuyakana yale aliyokuwa akiyanena kabla ya kuteuliwa kwenye nafasi za uongozi? Ni msomi gani ambaye alipoteuliwa, utendaji wake ulidhihirisha utofauti wa yeye aliye msomi na viongozi wengine wenye elimu ya kawaida? Je, ni Bashiru au Kabudi?

Sidhani kama kuna awamu ya utawala iliyojaza madokta na maprofesa kama awamu ya 5. Lakini ni awamu hii ndiyo imekuwa na sera mbaya za uchumi zinazofukuza uwekezaji, kupalilia umaskini, kuongeza shida ya ajira, kupunguza mauzo ya ndani na nje, na kuua mzunguko wa fedha.

Ni awamu hii ndiyo yenye mfumo wa utawala holela. Mkuu wa wilaya, Mkoa au Waziri anaweza kusimamisha uzalishaji wa kiwanda au mgodi wakati hana mamlaka ya kisheria, anaweza kumweka ndani mtu yeyote hata kwa masuala ambayo yangeweza kufikishwa mahakamani kwa mfumo wa kisheria wa kawaida.

Ni awamu hii, watawala wanaamini kuwa wananchi ni kama wanyama, wanaweza kuwaswaga kadiri wao wanavyotaka bila ya kuzingatia sheria na katiba.

Ni awamu hii matamko ya Rais yanageuzwa kuwa ni sheria hata kama yapo kinyume na katiba. Lakini ndani ya serikali kuna madokta na maprofesa kibao ambao badala ya kumshauri, kumrekebisha na hata kumuonya Rais na viongozi wengine pale ambapo utendaji wao ni kinyume na katiba, ni kinyume na kanuni za uchumi au kinyume na utawala bora, wao ndio wamekuwa vinara wa kushangilia kila linalonenwa na watawala.

Watanzania, yawezekana kwa mara ya kwanza, wanaoneshwa na Prof. Musa Assad, namna wasomi wanavyotakiwa kuwa.

Prof. Musa Assad, tunampongeza kwa mambo yafuatayo:

1) Kuzingatia mamlaka ya kazi yake kwa mujibu wa katiba na siyo matakwa ya mtu au kikundi fulani

2) Kujiamini kwake katika yale ambayo yupo sahihi

3) Kuongea ukweli kwa kile anachokiamini

4) Kutokuwa na papara na kuwa mropokaji

5) Kuwa mwadilifu na mkweli kwa nafsi yake na Mungu anayemwamini

Tunahitaji wasomi wa namna hii. Wanaofanya kazi kwa mujibu wa sheria na katiba lakini walio jasiri kuyanena yaliyo sahihi hata kama kuna watu hayawapendezi.

Kwa upande mwingine, tuna aibu ya Taifa. Mheshimiwa Ndugai na Bunge ni aibu ya Taifa letu. Mtu asiyejua kuwa kila mtu na kila taasisi yoyote ina weaknesses na strengths zake, na ndiyo maana kunakuwa na improvements programs. Ndugai hajui hayo. Bunge halijui hayo. Kama kweli Bunge letu na speaker, hawayajui haya, basi wana udhaifu wa hali ya juu, au sasa wameanza kuwa zaidi ya DHAIFU.
 
Kwa tabia aliyoionyesha CAG toka alipoanzisha vurugu hizi binafsi naungana na wachache wanaofikiria kuwa huyu CAG wa sasa hakustaili kujua baadhi ya fedha zimetumika kufanya nini. Nitakuwa nimewashangaza...lakini ukitumia milango yote ya fahamu na ile ya ziada utanielewa na utajishangaa kwa nini ulinishangaa.
 
CAG amedhihirisha unafiki wa hawa wanojiita wazalendo kumbe ni wezi wa fedha za umma.
CAG ni msomi na mzalendo wa kweli.
 
Inaonekana wengi mmechelewa kumfahamu Proffesa Assad, mwaka 2014 alishamuita jiwe political enterprenuer kwa kuuza nyumba za serikali.
Mbona alipotaka kubomoa jengo la Tanesco pale Ubungo makutano alizuiwa, ilikuwaje katika uuzwaji nyumba za serikali ambazo zilikuwa zimeisha depreciate mpaka negative value kiasi cha serikali kutumia gharama kubwa kuzitunza, Mh. Waziri mwenye zamana wakati huo kwa nini hakuzuiwa?
 
Kwa tabia aliyoionyesha CAG toka alipoanzisha vurugu hizi binafsi naungana na wachache wanaofikiria kuwa huyu CAG wa sasa hakustaili kujua baadhi ya fedha zimetumika kufanya nini. Nitakuwa nimewashangaza...lakini ukitumia milango yote ya fahamu na ile ya ziada utanielewa na utajishangaa kwa nini ulinishangaa.
Kiongozi wangu wa dini aliniambia kuwa,siku ukijiona kwamba wewe ni mkamilifu basi ujue kwamba sasa,umeanza kuugua ugonjwa wa akili ama tayari ushakuwa mgonjwa.

Kama unajiona una uwezo mkubwa wa akili basi ujue tayari una tatizo.

Kwa kawaida watu wanapima maongezi yako na matendo yako,na watakusifia kwamba huyu kweli ni kiona mbali.
Na kuna mfano mdogo tu hapa. Pr Assad hakuwahi hata mara moja kujisifia elimu yake wala cheo chake,lkn humu tumeangali,tumepima,na mwisho tumekubali kwamba HUYU NI PROFESA wa kweli wala hakugushi vyeti.

Kwanini mwenzetu unajisifia mwenyewe?
Mpaka sasa hujahisi kwamba kuna tatizo mahali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa tabia aliyoionyesha CAG toka alipoanzisha vurugu hizi binafsi naungana na wachache wanaofikiria kuwa huyu CAG wa sasa hakustaili kujua baadhi ya fedha zimetumika kufanya nini. Nitakuwa nimewashangaza...lakini ukitumia milango yote ya fahamu na ile ya ziada utanielewa na utajishangaa kwa nini ulinishangaa.
Hizi ndio akili za majizi ya ccm yakikwapuwa pesa za umma yanasingizia ni za kazi maalum wapumbavu wakubwa kabisa nyinyi tena mashetani kabisa.
 
Mbona alipotaka kubomoa jengo la Tanesco pale Ubungo makutano alizuiwa, ilikuwaje katika uuzwaji nyumba za serikali ambazo zilikuwa zimeisha depreciate mpaka negative value kiasi cha serikali kutumia gharama kubwa kuzitunza, Mh. Waziri mwenye zamana wakati huo kwa nini hakuzuiwa?
Unajuwa bei ya kiwanja tu Masaki na Oysterbay per squre meter ni bei gani na nyumba wameuziana kwa bei gani?

Nyinyi wazalendo wetu hata shetani anawaogopa.
 
Mbona alipotaka kubomoa jengo la Tanesco pale Ubungo makutano alizuiwa, ilikuwaje katika uuzwaji nyumba za serikali ambazo zilikuwa zimeisha depreciate mpaka negative value kiasi cha serikali kutumia gharama kubwa kuzitunza, Mh. Waziri mwenye zamana wakati huo kwa nini hakuzuiwa?
Tuwe wakweli wa nafsi zetu.

Mheshimiwa alikiuka maadili ya kazi. Nyumba zile, kabla ya kuuzwa viliwekwa vigezo vya nyumba za kuuzwa. Halafu baadaye viliwekwa vigezo vya watu wa kununua, na masharti ya kutimiza wakati wa kununua.

Kwa wanunuzi, sifa mojawapo ilikuwa mnunuzi lazima awe mtumishi wa umma, na nyingine mtumishi huyo ni lazima awe ni yule aliyekuwa akiishi ndani ya nyumba hiyo kwa muda mreru (kiliwekwa kipindi - sikumbuki ni miaka mingapi).

Yule Dada ambaye tunamjua kwa jina na sura, hakuwa mtumishi wa umma wala hakuwa anaishi kwenye nyumba aliyouziwa. Wakati ule yule Dada alikuwa anasoma UDSM, pale idara ya Hesabu. Na nyumba yenyewe aliuziwa kwa bei ya kutupwa.

Lakini pia ukumbuke na wale ndugu ambao hawakuwa watumishi wa serikali lakini nao wakaingizwa kwenye orodha, nao wakauziwa.

Hivi, hata kama wewe ungekuwa ni Rais au Waziri Mkuu, ungeweza kujua kila mmoja aliyewekwa katika orodha ya wanunuzi, alikuwa amekidhi vigezo au hakukidhi? Nadhani ni lazima ungewategemea watendaji wako wa Wizara, kumbe hao watendaji wako ndio waliofanya mambo kinyume cha vigezo vilivyokubaliwa.

Kwa hiyo siyo sahihi kulinganisha suala la ubomoaji wa jengo la TANESCO na watu waliouziwa nyumba pasipokuwa na sifa zilizokubaliwa.

Nadhani itoshe tu kusema kuwa Mh. alifanya kosa, na tuamue kusamehe maana wengi tuna makosa mbalimbali kama binadamu lakini tusiseme kuwa kila kitu kilifanyika kwa usahihi. Lakini angekuwa mmungwana japo angeamua kulipia tofauti ya bei ya soko na ile shilingi milioni 10 aliyolipa. Maana hata kama nyumba ingekuwa chakavu kiasi gani, lakini kwa shilingi milioni 10, eneo la Upanga, sijui kama kuna anayeweza kuelewa.
 
Kwa tabia aliyoionyesha CAG toka alipoanzisha vurugu hizi binafsi naungana na wachache wanaofikiria kuwa huyu CAG wa sasa hakustaili kujua baadhi ya fedha zimetumika kufanya nini. Nitakuwa nimewashangaza...lakini ukitumia milango yote ya fahamu na ile ya ziada utanielewa na utajishangaa kwa nini ulinishangaa.
University of kayumba
Bachelor of education in idiotness and evil honored

Mkuu soma hiyooo ulivyofauli
 
....
wakubwa kabisa nyinyi...
1. Ukichunguza vizuri, kuna uwezekano CAG alili 'provoke' Bunge na Spika kwa ujumla. Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu CAG alitoa kauli ya udhaufu wa Bunge muda kitambo kidogo, kabla Spika Ndungai hajaamua kutangaza kumuita CAG kwenye kamati ya maadili tena kwa maneno makali. Kwa maneno mengine, kuna uwezekano zilitumika juhudi za kidiplomasia kati ya Bunge na Ofisi ya CAG ili kumaliza tatizo hili lakini kwa tabia ambayo nimeielezea hapo awali ya CAG basi sieji akataka kuonyesha msuli tena sijui kwa mnaufaa ya nani. Ki urahisi ilitakiwa mbinu ya kushuka kwa upande mmoja ili ulingane na upande mwingine (CAG alikosa mbinu hii).

2. Katika suala lingine ningependa kujua ni utaratibu upi utumika kujiridhisha kuwa ripoti inayoandaliwa na CAG haina mapungufu na hakuna hila dhidi ya mkaguliwa?

3. Kwa nini majumuhisho ya ripoti ya CAG hayaanishi extreme best performance na extreme worst perfomance za wakaguliwa badala yake CAG anaonyesha worst performance za wakaguliwa tu. Baada ya ukaguzi, Ofisi ya CAG uchukua jukumu gani ili kuwasaidia wale waliopata hati chafu...ili waboreshe usimamizi wa fedha?

4. Je. tunaweza kuanza kufikiria kuwa CAG mara nyingi kwenye summary ya repoti yake husisitiza zaidi worst performance scenario ili kuifitinisha serikali iliyoko madarakani kwa wananchi ama huwa ana lengo gani hasa?
 
Rubbish, kwani Ludovick Uttoh alikuwa anatowa report za kuwalamba matako?
 
Back
Top Bottom