Mwakajana mbunge Msukuma aliwahi kueleza Bungeni kuwa mambo makubwa katika nchi hii yamefanywa na watu wasio wasomi, watu walioshia darasa la 7 ukilinganisha ba wanaojiita wasomi. Aliyaongea hayo wakati akipigania watendaji wa vijiji walioishia darasa la saba warudishwe kazini.
Pamoja na ukweli kuwa Mbunge Musukuma mara nyingi kauli zake hukosa weledi lakini katika hili kwa kiwango fulani alikuwa sahihi.
Kati ya watu ambao hawana mchango mkubwa katika Taifa hili ni hawa wanaoitwa 'wasomi', hapa ndiyo tunawapata wale wenye titles za Dr. na Prof.
Tumeshuhudia, mara kadhaa, hawa wanaoitwa wasomi, wakiteuliwa kwenye nafasi za uongozi katika serikali. Wengi wao walipoingia huko waliishia kuwa walamba viatu vya wale waliowateua na hakuna chochote kipya walichokipeleka badala ya baadhi yao kwenda kudhihirisha unafiki, woga, ukigeugeu na kukosa misimamo hata katika mambo ambayo waliwahi kuyanena kwa vinywa vyao wenyewe.
Sifa kubwa ya msomi wa kweli ni kujitambua, kujiamini na kusimama katika yale unayoyaamini.
Leo hii tujiulize, ni Doctor (PhD) na Professor (ukimwacha Musa Assad) gani ambaye daima amewahi kusimama katika yale anayoyaamini bila kugeuka na kuyakana yale aliyokuwa akiyanena kabla ya kuteuliwa kwenye nafasi za uongozi? Ni msomi gani ambaye alipoteuliwa, utendaji wake ulidhihirisha utofauti wa yeye aliye msomi na viongozi wengine wenye elimu ya kawaida? Je, ni Bashiru au Kabudi?
Sidhani kama kuna awamu ya utawala iliyojaza madokta na maprofesa kama awamu ya 5. Lakini ni awamu hii ndiyo imekuwa na sera mbaya za uchumi zinazofukuza uwekezaji, kupalilia umaskini, kuongeza shida ya ajira, kupunguza mauzo ya ndani na nje, na kuua mzunguko wa fedha.
Ni awamu hii ndiyo yenye mfumo wa utawala holela. Mkuu wa wilaya, Mkoa au Waziri anaweza kusimamisha uzalishaji wa kiwanda au mgodi wakati hana mamlaka ya kisheria, anaweza kumweka ndani mtu yeyote hata kwa masuala ambayo yangeweza kufikishwa mahakamani kwa mfumo wa kisheria wa kawaida.
Ni awamu hii, watawala wanaamini kuwa wananchi ni kama wanyama, wanaweza kuwaswaga kadiri wao wanavyotaka bila ya kuzingatia sheria na katiba.
Ni awamu hii matamko ya Rais yanageuzwa kuwa ni sheria hata kama yapo kinyume na katiba. Lakini ndani ya serikali kuna madokta na maprofesa kibao ambao badala ya kumshauri, kumrekebisha na hata kumuonya Rais na viongozi wengine pale ambapo utendaji wao ni kinyume na katiba, ni kinyume na kanuni za uchumi au kinyume na utawala bora, wao ndio wamekuwa vinara wa kushangilia kila linalonenwa na watawala.
Watanzania, yawezekana kwa mara ya kwanza, wanaoneshwa na Prof. Musa Assad, namna wasomi wanavyotakiwa kuwa.
Prof. Musa Assad, tunampongeza kwa mambo yafuatayo:
1) Kuzingatia mamlaka ya kazi yake kwa mujibu wa katiba na siyo matakwa ya mtu au kikundi fulani
2) Kujiamini kwake katika yale ambayo yupo sahihi
3) Kuongea ukweli kwa kile anachokiamini
4) Kutokuwa na papara na kuwa mropokaji
5) Kuwa mwadilifu na mkweli kwa nafsi yake na Mungu anayemwamini
Tunahitaji wasomi wa namna hii. Wanaofanya kazi kwa mujibu wa sheria na katiba lakini walio jasiri kuyanena yaliyo sahihi hata kama kuna watu hayawapendezi.
Kwa upande mwingine, tuna aibu ya Taifa. Mheshimiwa Ndugai na Bunge ni aibu ya Taifa letu. Mtu asiyejua kuwa kila mtu na kila taasisi yoyote ina weaknesses na strengths zake, na ndiyo maana kunakuwa na improvements programs. Ndugai hajui hayo. Bunge halijui hayo. Kama kweli Bunge letu na speaker, hawayajui haya, basi wana udhaifu wa hali ya juu, au sasa wameanza kuwa zaidi ya DHAIFU.