CAG: Kampuni zote za madini hazijawahi kulipa kodi kutokana na faida, hapa kuna tatizo

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
April 13, 2017 - Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad amewasilisha ripoti ya mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2016.

Katika vitu alivyoelezea ni pamoja tatizo kitendo cha makampuni ya madini nchini kutolipa kodi zitokanazo na faida kwa miaka yote.

Prof. Assad amesema…
Kampuni za madini zimekuwa zikitengeneza hasara kwa nchi, kampuni zote za madini hazijawahi kulipa kodi kutokana na faida kwa miaka yote

Inawezekana vipi watu wakawa wanaendesha miradi ya madini kwa miaka 10,15 wanapata hasara na hawaondoki? Sasa tunafikiri hapa kuna tatizo.

Full video ya CAG akielezea nimekuwekea hapa chini tayari…

April 13, 2017 Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad amewasilisha ripoti ya mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2016. Katika vitu alivyoelezea ni pamoja tatizo kitendo cha makampuni ya madini nchini kutolipa kodi zitokanazo na faida kwa miaka yote.

Prof. Assad amesema…>>>‘Kampuni za madini zimekuwa zikitengeneza hasara kwa nchi, kampuni zote za madini hazijawahi kulipa kodi kutokana na faida kwa miaka yote

Inawezekana vipi watu wakawa wanaendesha miradi ya madini kwa miaka 10,15 wanapata hasara na hawaondoki? Sasa tunafikiri hapa kuna tatizo’ –CAG Prof. Mussa Assad

Anachokisema CAG kuhusu sekta ya madini ni sahihi na serikali inabidi ifanyie kazi mapendekezo hayo.

Kuna ulaghai mwingi sana kwenye mikataba ya madini, kila siku serikali inapoteza mapato huku baadhi ya watanzania wachache wakinufaika kupitia madhaifu ya mikataba hiyo.

Ni vyema pia CAG akaangalia mkataba walioingia serikali kupitia taasisi yake ya TPDC na kampuni ya Pan - Africa, maana kila sehemu kumeoza.

Na hii ilikuwa chini ya MARAIS wa zamani, nasikitika Rais Magufuli kusema atawalinda. Hawa lazima wamefaidika na mikataba hii mibovu. Kwa kitu kidogo wameyauza maisha ya Watanzania kwa bei ya kutupa. Ndiyo maana kila kitu kilikuwa siri.
 
April 13, 2017 Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad amewasilisha ripoti ya mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2016. Katika vitu alivyoelezea ni pamoja tatizo kitendo cha makampuni ya madini nchini kutolipa kodi zitokanazo na faida kwa miaka yote.

Prof. Assad amesema…>>>‘Kampuni za madini zimekuwa zikitengeneza hasara kwa nchi, kampuni zote za madini hazijawahi kulipa kodi kutokana na faida kwa miaka yote

Inawezekana vipi watu wakawa wanaendesha miradi ya madini kwa miaka 10,15 wanapata hasara na hawaondoki? Sasa tunafikiri hapa kuna tatizo’ –CAG Prof. Mussa Assad

Full video ya CAG akielezea nimekuwekea hapa chini tayari…

Tunamini raisi wetu atafuatilia
 
Hakuna sehemu tuliyofanya ujinga watanzania kama sekta ya madini ktk miaka ambayo tuliingia mikataba mibovu kabisa duniani na makampuni ya uchimbaji wa madini Tanzania.

Na hii itatugharimu sisi na vizazi vyetu kwa kupata mapato kidogo sana toka sekta ya madini huku kwenye migodi wakinufaika na madini na kutuachia mashimo tu.

Rais Magufuli ameunda Kamati mbili kutaka kujua ukweli ya sekta hii kiuhakika toka tulipoanza kuwapa wawekezaji wakubwa mikataba ya kuchimba madini.
 
Hii ndiyo Tanzania. Wafanya biashara wa kawaida unapoanza biashara tu unakadiriwa kodi yako haijalishi umepata hasara au faida. Wafanyakazi wote hawajawahi pewa mda wa kuri cover cost za uanzaji wa kazi emediately unaajiriwa unaanza lips kodi but haya makampuni hadi 10 years hayalipi kodi.
 
April 13, 2017 Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad amewasilisha ripoti ya mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2016. Katika vitu alivyoelezea ni pamoja tatizo kitendo cha makampuni ya madini nchini kutolipa kodi zitokanazo na faida kwa miaka yote.

Prof. Assad amesema…>>>‘Kampuni za madini zimekuwa zikitengeneza hasara kwa nchi, kampuni zote za madini hazijawahi kulipa kodi kutokana na faida kwa miaka yote

Inawezekana vipi watu wakawa wanaendesha miradi ya madini kwa miaka 10,15 wanapata hasara na hawaondoki? Sasa tunafikiri hapa kuna tatizo’ –CAG Prof. Mussa Assad

Full video ya CAG akielezea nimekuwekea hapa chini tayari…

Yaani mawaziri wa madini na wa fedha wakati wa hii mikataba walilidanganya bunge,serikali na wananchi kwamba kwenye madini serikali it's pata corporation tax Kati ya 30% mpaka 40% na pia PAYE , VAT na other indirect tax na pia Kutoka ajira , kumbe hiyo corporation tax ya 30% mpaka 40% hakuna kitu, inabidi kamati maalumu au CAG wafuatilie zaidi suala hili na mawaziri husika wawekwe chini ya uangali nahasa Hasa mali zao na wote waliohusika kwa namna moja au nyingine
 
Hii ndiyo Tanzania. Wafanya biashara wa kawaida unapoanza biashara tu unakadiriwa kodi yako haijalishi umepata hasara au faida. Wafanyakazi wote hawajawahi pewa mda wa kuri cover cost za uanzaji wa kazi emediately unaajiriwa unaanza lips kodi but haya makampuni hadi 10 years hayalipi kodi.
Sio hayalipi kodi bali hayalipi inayotokana na faida.
 
Shida sio kampuni za madini. Shida ni sheria zetu wenyewe. Ni vizuri CAG pia akawa mkweli kuwa kisheria na kanuni za kodi na za kihasibu upo uwezekano wa kampuni kupata faida (kihasibu) lakini ikawa na hasara(kikodi) na hivyo kutolipa kodi ya mapato. So argument kwamba kama hawalipi kodi kwa sababu ya kupata hasara (ya kikodi) wangekuwa wameondoka may not be valid (with due respect kwa Prof).
 
Back
Top Bottom