CAG: Huu ndio ufisadi Halmashauri ya Serengeti

don-oba

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
1,387
677
Kutokana na ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, madudu na ufisadi mkubwa umegundulika katika Halmashauri yetu ya Serengeti. Hamashauri yetu imewekwa katika orodha ya Halmashauri zenye makosa katika uandaaji wa taarifa za hesabu. Halmashauri imetoa malipo yasiyothibitishwa na stakabadhi ya mil 67, 475, 085/- kutoka katika akaunti ya amana. Vilevile katika ukurasa wa 277 wa ripoti hii kwa mwaka wa fedha 2014/15 Halmashauri imepata HATI YENYE SHAKA. Ikumbukwe kwamba mwaka wa fedha 2011/12, 2012 /13 na 2013/14 miaka yote hiyo halmashauri yetu ilikuwa ikipata HATI SAFI.

Kwahiyo Halmashauri yetu imeporomoka kutoka kwenye hati safi hadi hati yenye shaka! Mkaguzi Mkuu anasema hii nikwasababu thamani ya ardhi haikuoneshwa kwenye taarifa za hesabu, hivyo kufanya thamani ya malengo, mitambo na vifaa vilivyooneshwa kwenye taarifa za hesabu kuwa pungufu kwa thamani ya ardhi ambayo haikuthamanishwa. Mapendekezo ya ukaguzi katika miaka ya nyuma kwenye halmashauri yetu yalikuwa 32, yaliyotekelezwa 10, yanayoendelea na utekelezaji 19 na yasiyotekelezwa 1. Makisio yaliyoidhinishwa yalikuwa 1, 849, 055, 000/- lakini makusanyo halisi yalikuwa 2, 089, 863, 000/- Makusanyo ya ndani yalikuwa 2, 089, 863, 000 /- na matumizi halisi yalikuwa 21, 078, 528, 000/-.

Jambo la ajabu kabisa, kuna fedha 21, 580, 787, 000/- zilitumwa na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri kwa ajili ya ruzuku na matumizi ya kawaida lakini zilitumika 21, 078, 528, 000/- na kuacha bakaa ya mil 502, 259, 000 /- zisijulikane zilipokwenda! Halmashauri ilitumia takribani mil 132, 930, 000/- kwenye ujenzi wa maabara shughuli ambayo haikuwa na idhini ya bajeti. Lakini Halmashauri ilifanya ujenzi huo bila makadirio yaliyopitishwa. Ripoti inatuambia Halmashauri ilifanya malipo ya mil 74, 212, 648/- bila stakabadhi za kielekroniki.

Kuhusu elimu upande wa shule za sekondari kuna upungufu wa nyumba 474, zilizopo 110. Mabweni yaliyopo ni 21, upungufu 69. Maabara zilizozo ni 26, upungufu 37. Vilevile Ripoti imeonesha ubadhirifu katika miradi ya NMSF, SEDP na mradi as mfuko wa jimbo (CDCF)ambao haujaonesha matumizi yoyote. Kuna mil 32, 459, 491/- ambazo inasemekana zilikopesha mtu bado hazijarudishwa. Kwa machache hayo, naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom