CAG ashauri Serikali ivunje ATCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CAG ashauri Serikali ivunje ATCL

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wwww, Apr 15, 2012.

 1. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 351
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 60
  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema, Serikali inavyoendesha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa sasa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

  Utouh amependekeza ATCL ivunjwe na liundwe shirika jipya lenye mtaji, menejimenti nzuri na mikakakati madhubuti ili kumudu ushindani.

  “Ni mapendekezo yangu kwamba kama shirika hili litaundwa upya, likapewa mtaji wa kutosha na likawa na uongozi bora, hakika litafanya kazi vizuri,” alisema Utouh.

  CAG Utouh alitoa pendekezo hilo mjini Dodoma juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasilisha bungeni Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2011.

  Alisema ATCL kwa sasa haina ndege hata moja inayofanya kazi baada ya iliyokuwepo, kuanguka huko Kigoma wiki iliyopita wakati ikiruka.

  Utouh pia amerejea pendekezo lake la kutaka wabunge wasiwe wajumbe wa bodi za wakurugenzi wa mashirika ya umma, kwani kwa kufanya hivyo watashindwa kuyasimamia.

  “Serikali ichukue hatua kama alizochukua gavana wa Benki Kuu za kuwaondoa wabunge kwenye taasisi za fedha za umma ambazo ni mabenki na mifuko ya pensheni,” alisisitiza Utouh

  Historia ya ATCL
  ATCL ilianzishwa baada ya Shirika la Ndege la Tanzania ATC kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mwaka 2002.

  Hili ni moja ya mashirika ya ndege yaliyoonyesha kukua kwa kasi miaka ya 1980 na 1990 lakini lilianza kuyumba kutokana na uendeshaji mbovu na hali ikawa mbaya zaidi baada ya kuingia ubia na SAA.

  Serikali iliingia ubia na SAA mwaka 2002 kwa matumaini ya kuifanya ATCL moja ya mashirika makubwa ya ndege Afrika lakini hali ikawa kinyume.

  Kwenye mkataba huo, Serikali ilibaki na hisa 49 huku SAA ikimiliki hisa 51, ambazo zilimfanya mbia huyo kuwa na nguvu katika maamuzi mengi.

  Septemba 2006, Serikali ilivunja mkataba na SAA baada ya kubaini kuzidi kudorora ATCL huku ikiandamwa na madeni makubwa.

  Baada ya kuvunja mkataba huo, ATCL ilirejeshwa chini ya menejimenti ya wazalendo iliyokuwa inakabiliwa na changamoto nyingi yakiwemo madeni makubwa, ukosefu wa fedha, mishahara ya wafanyakazi na kutokuwa na ndege zinazofanya kazi.

  Ndege mbili ilizokuwa nazo, zote zilikuwa za kukodi na zilifanya kazi kwa kusuasua kiasi cha kulifanya shirika hilo kusitisha safari kutokana na idadi ndogo ya abiria pamoja na ndege hizo kuwa na matatizo mara kwa mara.

  Miaka mitatu iliyopita Serikali ilikuwa kwenye mkakati wa kuingia ubia mwingine na China lakini mpango huo baadae uliyeyuka.

  Hivi sikio la kufa linasikia dawa kweli? Nampongeza sana Ndugu Utuoh kwa ushauri ambao hata hivyo hautasikika kwani wanasiasa wananufaika na hali iliyopo pale ATCL, hivyo kuwaambia walivunje shirika hilo maana yake unawanyang'anya tonge mdomoni.

  Lile shirika lina watu wamejipanga kuchuma kutoka pale. Watu wanaofaidika pale ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Eng. Omary Chambo, David Mattaka - Ex. CEO, Eliasaph Mathew - Ex- CFO sasa IA - Galileo, William Haji- Ex-IA na Balozi Mstapha Nyang'anyi Ex- Board Chairman. Hawa ndiyo wamelifiksha shirika hili hapo lilipo.

  Hivyo nina uhakikika ushauri huu utapuuzwa kabisa, tena akiendelea kutoa ushauri huo ajiandaye kufanywa kama Mwakyembe.

   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Utouh janga la kitaifa,alishawahi kusema jairo hana kosa!
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  HIVI MTU AKIKUAMBIA UVUNJE KITU AMBACHO KIMESHAVUNJIKA SI SAWA NA KUKUAMBIA HUNA AKILI?
  HILO SHIRIKA ANALOSHAURI LIVUNJWE LIKO WAPI?
  NA HUO MTAJI ANAOSEMA UWEKWE KWENYE SHIRIKA JIPYA UTAPATIKANA WAPI?WAKATI AMETUAMBIA MISAMAHA IMESABABISHA NCHI KUFILISIKA?

  MIMI NINGEMWONA ANA AKILI KAMA ANGESHAURI LIUZWE HIYO HELA SERIKALI IFUNGUE KIWANDA CHA VIROBA HUYO MATAKA AWE MKURUGENZI MKUU.maana ndiyo kazi tunayoiweza.
   
 4. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  [/QUOTE] Utouh pia amerejea pendekezo lake la kutaka wabunge wasiwe wajumbe wa bodi za wakurugenzi wa mashirika ya umma, kwani kwa kufanya hivyo watashindwa kuyasimamia.

  “Serikali ichukue hatua kama alizochukua gavana wa Benki Kuu za kuwaondoa wabunge kwenye taasisi za fedha za umma ambazo ni mabenki na mifuko ya pensheni,” alisisitiza Utouh [/QUOTE]

  Huyu asiwe ANADANGANYA UMMA kama vile yatendekayo yako kuzimu. Mbunge Kirigini ambaye ni mjumbe wa bodi ya PPF mbona anaendelea kama kawaida?

  Ataachaje kipato hiki: Annual fees about Tshs. 3,000,000.00, sitting allowance Tshs 600,000 na kuna vikao 8 (ordinary) kwa mwaka (Tshs 4,800,000), Per diems za ndani akiwa kwenye kikao, Tshs 600,000 per day. na hulipwa siku tatu kwa kila kikao (600,000X8X3days) 14,400,000. Per diem nje ya nchi training siku 15 mara mbili kwa kila mwaka (USD 800X15daysX2tripsX1600) Tshs. 38,400,000.

  Mapato haya kila mwaka yanayokaribia milioni 60, ukiacha vikao viitwavyo extra ordinary, per diem za kutembelea vitega uchumi mikoani, mikutano ya kila mwaka ya Arusha.

  Wakati wanachama wastaafu waliochangia kwa umri wao wote wakiambulia Tshs. 600,000 (12X50,000) kwa mwaka hali huyu mbunge na bodi members wenzie wanalipwa Tshs 600,000 kwa siku.

  Haya sio kwamba Utouh hayaoni ila anazibwa na pesa za PPF kupitia kwa Bw. William Erio Mkapa.

   
 5. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Utoh, haeleweki anafanya kazi gani
   
 6. J

  John W. Mlacha Verified User

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  hakuna mwenye uchungu na nchi watu wana uchungu na matumbo yao
   
 7. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Kuna uhakika gani kama hilo shirika jipya litakaloundwa kutofisidi kodi ya wananchi? Suala ni kutibu tatizo la kutofanya vyema kwa shirika. Menejimenti ya Net Group solution kwa Tanesco haikuwa mwarobaini wa kulifufua shirika hilo! Nashauri apendekeze pia Tanesco nayo ivunjwe kwasababu haina tija na kodi zetu zinapotea kama ATCL.
   
 8. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  -Aje Mkapa atueleze mafanikio ya shirika hili tangu alipolibinafsisha kijinga.
  -Utatoa wapi fedha za kuunda shirika jingine wakati mali zote za shirika zimeshafisidiwa, hata likiuzwa unapata bei ya hasara.
  -Hilo shirika jingine lisimamiwe na serikali ipi wakati tayari serikali hiyohiyo imesha prove failure katika hilo.
  Kweli hii ni Jamhuri ya Maigizo ya Tz.
   
 9. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tujifunzekutoka ethiopia

  Tatizo la watoto wa vigogo kuhusika ktk hisa kama ilivyo kapunga mbeya
   
 10. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #10
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa utawala huu uliopo chini ya CCM hakuna kampuni au taasisi yoyote ya serikali na umma itakayofanya vizuri"MIPANGO MIZURI KATIKA MAKARATASI AMBAPO NYUMA YAKE IMEJIFICHA MIPANGO YA KUCHOTA PESA NA RASILIMALI NA KODI ZA WALALAHOI.KILA TAASISI NA SHIRIKA LA UMMA KATIKA NCHI YETU IMEKUA DEAL YA WAJANJA WACHACHE KUJITAJIRISHA,AMBAPO KATIKA MFUMO AU SYSTEM AU CIRCLE NA MFUMO WA CHAMA TAWALA CCM NA UTAWALA HAKUNA WA KUMWAJIBISHA MWENZI KUANZIA RAIS JK KWANI WOTE WANACHEZA MCHEZO MMOJA UFISADI!!!!!!!"MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 11. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Tatizo la kuvunja taratibu za kuwachagua wabunge kuwa wajumbe wa bodi mwanzo wake ni mawaziri ambao wanawateua wenzi wao; si ulisikia bungeni juzi wakati wanachangia muswada wa mifuko ya pensheni wabunge wakiomba ujumbe kiujanjaujanja wakati wa kuchangia . Ni conflict of interest kwa wabunge kuwa wajumbe wa bodi za mashirika ya umma na ni jukumu la waziri mkuu kama kiongozi wa shuhuri za serikali bungeni kuhakikisha kuwa wabunge hawawi wajumbe wa bodi hizi otherwiise inakuwa embarrassment kwake swala hili linapojadiliwa mara kwa mara bungeni! Mifano ya wabunge kwenye bodi ni kama huyo Kirigini PPF na Mwambalaswa TANESCO[ ingawa yuko kwenye kampuni ya kuzalisha umeme wa upepeo]!!
   
 12. Jamani mbona si poa

  Jamani mbona si poa Member

  #12
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kama wataanzisha shirika jipya si kweli kuwa ndo litakuwa na tija. Cha muhimu ni serikali iamue kwa ukweli kwamba sasa wanalifufua shirika hilo kwa kugharamia mahitaji yake yote ya mtaji mpya wote unaohitajika na madeni yake yote yalipwe. kuwepo na usimamizi na ufuatiliaji wa karibu wa utendaji kazi wa shirika. kama TRA ni chombo cha umma na kinasimamiwa kwa nini ATCL ishindwe kusimamiwa na ikawa na tija? Naamini kinachohitajika ni serikali kuwa na dhamira za dhati kabisa za kulifufua shirika hili kama ilivyo kwa TRC ambalo nalo limekwama kabisa. Namlaumu sana Ben aliyefanya maamuzi ya haraka kubinafsisha mashirika haya badala ya kuyasimamia na kurudisha heshima yake kama ilivyokuwa awali kwani kwa namna moja au nyengine yamechangia kuleta hali ngumu ya maisha kwa bidhaa kupanda bei kutokana na kutokuwepo kwa usafirishaji wa reli ndani ya nchi na hatimaye kutegemea usafiri wa bidhaa kupitia kwa magari ya watu binafsi.
   
 13. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Uganda, Malawi, Rwanda wote wamefufua mashirika yao ya ndege kutumia wataalamu wa ATCL
   
 14. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  previously: Mattaka alifanikiwa kudesign logo ya kampuni.
  currently: Mh. Nundu + Chizi, anasema shirika sio lazima kumiliki ndege bali kuna vitu kama Routes, (sijui na nini - nilimsikia akisema nikashangaa)!

  Nashindwa kuamini kuwa jina la mtu linaweza reflect matendo/akili yake
   
Loading...