VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali,almaarufu kama CAG, imetoa kali za mwaka. Ripoti hiyo ya CAG Prof. Assad imeanika ufisadi wa kutosha na kutisha katika idara,taasisi na nyanja mbalimbali za kiserikali.
CAG amewaambia watanzania na walimwengu wote jana kuwa fedha za umma,za wananchi wengi waliotopea kwenye umaskini wa kuogofya,zinaendelea kufisadiwa na walioaminiwa kuongoza Serikali. Viongozi wameanikwa kama wasaliti kupitia ufisadi wao.
Rais na Serikali yake wameongezewa majipu na matambazi ya wazi ya kuyafanyia kazi. CAG amekivua nguo kiaina Chama cha Mapinduzi kwakuwa makada wake ndiyo waongozao Serikali. Ufisadi hauwezi kujitenga nao wala chama chetu-CCM.
CAG amekuja muda mbaya. Amekuja muda ambao watanzania maskini walikuwa wametingwa na kupiga makofi na kushangilia ziara za kushtukiza na kutumbuliwa wafanyakazi papo kwa papo hata kama ni kwenye ufunguzi wa Daraja la haja. Kwa Ripoti ya CAG,makofi na vicheko vitapungua. Huzuni na hasira za kuliwa hela zitatawala tena anga la siasa na maisha ya watanzania!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam