CAG ‘alalamika kupuuzwa’ na Serikali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CAG ‘alalamika kupuuzwa’ na Serikali.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Apr 14, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  CAG ‘alalamika kupuuzwa’ na Serikali.

  Imeandikwa na Na Shadrack Sagati; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 21; Jumla ya maoni: 0
  SERIKALI haikutekeleza mapendekezo yote 15 yaliyotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) mwaka 2010, hali aliyoieleza kuwa inakwamisha ufanisi serikalini na katika mashirika ya umma.

  CAG amelalamikia hatua hiyo ya Serikali katika ripoti yake ya mwaka 2010, iliyotolewa wiki hii na kuorodhesha mapendekezo yote aliyotoa huku akionya kuwa kudharauliwa kwake, kutasababisha kukwama kwa shughuli za maendeleo.

  Baadhi ya mapendekezo aliyosema hayakufanyiwa kazi ni pamoja na ushauri wa kuitaka Serikali ipunguze ununuzi wa magari ya kifahari na kupunguza gharama za warsha, ili mapato yanayokusanywa yatumike kwenye shughuli za maendeleo.

  Pia alilalamikia kutotekelezwa kwa mapendekezo ya kuondoa wabunge kuwa wajumbe wa bodi za wakurugenzi wa mashirika ya umma, ili kuepuka mgongano wa maslahi kwa kuwa ni wabunge hao hao wanaosimamia utendaji kazi za mashirika hayo kupitia Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).

  Mapendekezo mengine aliyolalamikia kutotekelezwa na Serikali ni kuboresha ukusanyaji mapato kutoka vyanzo mbalimbali, kuziba mianya ya ukwepaji kodi hususani kwenye mafuta ya magari na mitambo, kupunguza misamaha ya kodi na kupanua wigo wa kodi.

  CAG alisema katika ripoti hiyo, kuwa hata alipoomba maelezo ya kina kuhusu uhalali wa malipo ya dola milioni 4.8 za Marekani kwa kampuni ya M/s Dowans kwa ajili ya kukodisha ndege maalumu, Serikali haikumpa majibu yoyote sasa yapata mwaka.

  Mbali na maombi ya kupata taarifa za Dowans ambayo hayajatekelezwa, CAG alilalamikia pia ushauri wake wa Serikali kuligawa mara mbili Shirika la Maendeleo ya Petroli la Tanzania (TPDC); shirika moja lishughulikie biashara na lingine litoe leseni, ukaguzi na kufanya kazi za udhibiti, ili kuleta ufanisi katika biashara ya mafuta, haukutekelezwa.

  Mapendekezo mengine aliyosema yalipuuzwa ni kuruhusu Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), kusimamia hesabu za mashirika na kampuni zote ambazo Serikali ina hisa.

  Mkaguzi huyo pia alipendekeza bodi za wakurugenzi za mashirika ya umma kuhakikisha watendaji wakuu wa mashirika hayo wanawajibika zaidi kwa matokeo ya utendaji kazi wao, lakini alieleza kuwa ushauri huo haujatekelezwa.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  JK analala,ika na wateule wake nao ni malalamiko......kama hamridhiki si muachie ngazi ijulikane moja......................kukinga pesa zetu hatuwasikii mkilalamika lakini yanapokuja majukumu ni malalamiko yasiyo na ukomo.....................................
   
Loading...