CAG abaini ufisadi wa Sh50 bilioni serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CAG abaini ufisadi wa Sh50 bilioni serikalini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Apr 30, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,623
  Likes Received: 419,794
  Trophy Points: 280
  CAG abaini ufisadi wa Sh50 bilioni serikalini Send to a friend Saturday, 30 April 2011 10:00

  [​IMG]Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Ludovick Utouh

  Boniface Meena
  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amebaini ufisadi wa Sh50.6 bilioni serikalini ukiwamo wa malipo yanayotia shaka ya Sh15.7 bilioni katika kipindi cha mwaka wa fedha 2009/2010.

  Katika ripoti yake ya ukaguzi iliyoishia Juni, 30, 2010, CAG amesema fedha nyingi zilitumika kufanya ununuzi bila kufuata taratibu.

  Katika ripoti yake, amesema wizara, idara, wakala na sekretarieti za mikoa, zilitumia fedha katika kipindi cha mwaka 2009/2010 kufanya ununuzi ambao haukuwa kwenye mpango wa mwaka.

  Alisema matumizi hayo ni kinyume cha kifungu cha 45 cha Sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004 kinachozitaka taasisi za ununuzi kuweka mpango wa mwaka kwa lengo la kuepuka ununuzi wa dharura, kupata thamani ya fedha, kupunguza gharama za matumizi na kufanya ununuzi sahihi kwa njia ya kandarasi.

  "Ukaguzi umebainisha kwamba katika mwaka wa fedha 2009/2010, taasisi zilizoonyeshwa hapa chini zilifanya ununuzi yenye thamani ya Sh50.6 bila kufuata kifungu cha sheria," imeeleza sehemu ya ripoti hiyo.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kati ya fedha hizo, Sh650.7 milioni zilitumika katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, kununulia samani kwa maofisa wanaoishi katika nyumba binafsi

  Wizara nyingine ni Nishati na Madini, Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Maliasili na Utalii, Habari, Vijana na Michezo na Tume ya kurekebisha Sheria.

  "Ununuzi wa samani kwa maofisa hao ulikuwa si sawa kwa kuwa hawana stahili ya kununuliwa vitu hivyo na ni kinyume cha waraka wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Utumishi) Na. C/CA/134/213/01/G/69 wa Januari 30, 2006, unaohusu malipo ya posho ya nyumba na ununuzi wa samani kwa nyumba za Serikali kwa maofisa wenye stahili," imesema ripoti hiyo.

  CAG ameeleza pia kuwa eneo jingine ambalo fedha hizo zimetumika vibaya ni matengenezo ya magari ya serikali na taasisi zake ambako Jumla ya Sh176.7 milioni zimeliwa.

  Alisema wakati kanuni ya 5 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma (mali, kazi, huduma zisizo za ushauri na uuzaji wa mali ya umma kwa zabuni) ya mwaka 2005, ikitaka wizara, idara, wakala na sekretarieti za mikoa kutengeneza magari yake Temesa (Wakala wa Ufundi na Umeme), au kupeleka katika karakana zilizoidhinishwa na wakala huyo, magari mengi yalikuwa yanatengenezwa kwenye karakana binafsi.

  "Magari hayo yametengezwa kwenye karakana hizo bila kuwa na kibali kutoka Temesa kama sheria inavyotaka."

  CAG amebaini pia kuwa serikali na taasisi zake imetumia Sh13.8 bilioni kulipia mali na vifaa ambavyo hata hivyo, havikupokewa au vilipokewa pungufu.

  "Hii ni kinyume na kanuni ya 122 ya kanuni za Ununuzi ya Umma (mali, kazi, huduma zisizo za ushauri na uuzaji wa mali ya umma kwa zabuni) ya mwaka 2005," alisema.

  Taarifa hiyo ilisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2009/2010, wizara, idara, sekretarieti za mikoa mitatu zilifanya malipo yenye shaka yanayofikia Sh15.7 bilioni.

  Malipo hayo yalikosa viambatanisho ambavyo vingeonyesha taarifa za kina pasipo kuacha shaka yoyote kuhusiana na usahihi wa malipo hayo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,623
  Likes Received: 419,794
  Trophy Points: 280
  Tatizo la CAG nikuwa baada ya kubaini wizi na ubadhirifu...........what follows next
   
 3. k

  kabindi JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Fikiria Kwamba hiyo ni report ya 2009/2010! 50 blns! ukijumlisha na miaka iliyopita ambapo udhibiti ulikuwa ni kidogo utagundua kwa nini Tanzania tumekuwa Masikini! Ingawa Raisi Kikwete hajui kwa nini Tz tunakuwa masikini!..
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndo maana sasa hivi ajira serekalini ina soko kubwa licha ya mishahara kuwa ya hovyo, watu wana uhakika wa kutengeneza zaidi ya 100X wakipata penyo! Hatari na giza nene huko mbele.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Hatuna culture ya kuwajibishana...tunaona fahari kuanika haya mambo hadharani, ili iweje sasa?
   
Loading...