Cabinet CHADEMA naomba msome hapa

STIDE

JF-Expert Member
Sep 1, 2011
997
349
Peopleee's Power!! Naomba niwape pongezi uongozi mzima wa CHADEMA kwa mafanikio mliofikia huko Igunga, binafsi nayaita "mafanio," maana kuanzia 0 hadi maelfu ya kura ni jambo la kujivunia!

Ninayo mengi ya kuomba yafanyike kabla ya uchaguzi mkuu 2015, ila baadhi ni haya chini na mengine wadau wenye uchungu na nchi hii(mawazo endelevu) wataniongezea.

(A) Mkitumia sera zenu safi mlizo nazo, jitahidini kwa khari na mali kutoa elimu vijijini kwa kasi, maana vijiji vingi Tz bado wamelala, hawajajua maana halisi ya ukombozi! (e.g, fanya tathimini kati ya kura za Igunga mjini na vijijini).

(B) Taftieni ufumbuzi wa SUMU ya UDINI iliyoenezwa na mafisadi ktk kampeini za Igunga! Mimi nadhani kwa hili muwaite viongozi wa dini mzungumze nao na mfanye nao mihadhara ili kuondoa habari za udini ktk watu.

(C)Watembeleeni mara kwa mara na kuwashukuru wapiga kura wenu maana ndo mtaji wetu ktk ukombozi wa taifa hili.

(D) Fungueni ofisi za matawi nyingi hususani vijijini maana 2015 mtakabidhiwa nchi hivyo mpate pa kuanzia, (kiufupi mjipange kuongoza nchi).

(E) Boresheni mshikamano ndani ya chama, msimamo thabiti, maana ni dhahiri mnawindwa na mafisadi ili chama kififie(e.g, wamewaonga CUF chopa ili kuidhoofisha cdm)

"Nawatakieni kila la kheri Mungu yu pamoja nasi CHADEMA."

PEOPLEEEE's .....!
Nawasilisha.
 
AZIMIO

Senior Member
Jun 15, 2011
188
48
Ni kweli kabisa kwa kura ambazo wamepata chadema hawana budi kupongezwa makamanda kwa kazi nzuri,
ushauri umetoa mzuri sana natumaini utafika kwa walengwa nna kufanyiwa kazi.
people's...................................... power
 
Mtuflani

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
323
74
Kweli mkuu,ila suala la katiba mpya lianze kudaiwa sasa hivi tusisubiri baadae,chadema mkomae nalo hilo.
 
MPAMBANAJI.COM

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
713
331
HATIMAYE CCM imekiri ya kuwa imeshindwa kwa zaidi y asilimia 53 na hawana haya ja kujisifu, kwani uchambuzi wa kweli unaonesha wazi kuwa mbunge wao atakua anaongoza watu wanaompinga kuliko wale wanaomuunga mkono.

Hukuna haja yeyoye ya kujisifu na matokeo haya, ukweli ni kwamba tumeshindwa vibaya sana na tunakubalika kwa asilimia 47 achilia mbali mizengwe na takrima tulizotumia kwa watu wa Igunga.Mfano ugawaji wa mahindi siku mbil kabla ya uchaguzi, ugawaji wa maji vijijini, BAKWATA mbinu na mkakati mingine isiyokua rafiki wa demokrasia.

Ukweli hawa jamaa wa CHADEMA wanakubalika sana na hatuna sababu ya kujigamba.Hatukubaliki na tunapoteza mwelekeo.
 
GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,319
305

Tunajua mtakuja na sababu nyingi sana kuhusu kushindwa kwenu kwani mliyotegemea sivyo. Mmetumia hela nyingi sana zipatazo tshs 1.345bn kwenye uchaguzi huo, na kwa taarifa yako chama kwenye akaunti zake hakina kitu kimeishiwa ' kimefilisika'.
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Ni kweli kabisa kwa kura ambazo wamepata chadema hawana budi kupongezwa makamanda kwa kazi nzuri,
ushauri umetoa mzuri sana natumaini utafika kwa walengwa nna kufanyiwa kazi.
people's...................................... power

Hivi ndicho walichokuwa wanakihitaji kwenye uchaguzi huu?
 
mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,285
7,303
Ww hata kiswahili hujui ndio wataka kutupa ushauri gani sasa ? Craaaaaaaaaaaaaaaaaaaap !
Ujumbe umefika mbona Wasukuma hawajui kiswahili na wamepiga kura huko Igunga,hata kama kiswahili kibovu ujumbe umefika
 
kamakak

Member
Sep 22, 2010
60
9
Mimi nijuacho kwa CHADEMA kule Igunga Kilikuwa kinataka kuthibitisha kuwa uchaguzi wa 2010 waliibiwa kura.Ndiyo maana walipeleka pesa nyingi sana ili washinde alafu waanze kulalamikia uchaguzi wa 2010.
 
mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
554
Hivi ndicho walichokuwa wanakihitaji kwenye uchaguzi huu?

Nadhani sicho tu walichohitaji, walihitaji/tarajia ushindi. Lkn pamoja na hayo mafanikio waliyopata nazungumzia kuungwa mkono na raia zaidi ya 23000 wa Igunga still ni jambo la kujivunia ukizingatia hawakuwa na base kali sana before pale. Proves wananchi wengi wanachoshwa na ccm na wanaiamini CDM. Big up kwa mtoa thread na observation yake. Cabinet lichukulieni hili kwa umakini
 
buyegiboseba

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
535
145
Pia CHADEMA nawaomba muwe mnaupdate website Yenu kwani haiendi na kasi ya habari zilivyo,wekeni watu full time kuapdate taarifa kwenye tovuti yenu ili iendendane na hadhi ya Tovuti ya chama imara chenye kujiandaa kushika dola hakuna shaka 2015 ikulu njia nyeupe hata kama Shekhe Yahya akifufuka kutabiri.
 
Hakuna hela pesa yote imeishia igunga Tshs 1.345bn unadhani mchezo !
 
MALI YA BABA

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
459
119
Ni kweli kabisa mkuu sasa chadema waanze kujikita vijijini na kufungua matawi itawasaidia sana
 
Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,888
1,190
Ni kweli kabisa mkuu sasa chadema waanze kujikita vijijini na kufungua matawi itawasaidia sana
Nadhani mkuu pamoja na kujikita vijijini, wafanye jitihada za makusudi kuwahimiza watu kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura pindi kunapotokea nafasi ya maboresho. Ni kweli vijana wengi watakuwa hawakujiandikisha hapo awali kwa kukata tamaa, lakini kwa sasa wamehamasika sana na wanahitaji mabadiliko ya kweli.
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Nadhani sicho tu walichohitaji, walihitaji/tarajia ushindi. Lkn pamoja na hayo mafanikio waliyopata nazungumzia kuungwa mkono na raia zaidi ya 23000 wa Igunga still ni jambo la kujivunia ukizingatia hawakuwa na base kali sana before pale. Proves wananchi wengi wanachoshwa na ccm na wanaiamini CDM. Big up kwa mtoa thread na observation yake. Cabinet lichukulieni hili kwa umakini

Linganisha hizo na resources (human na financial) walizotumia halafu utumabie kama viko commensurate.
 
mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
554
Linganisha hizo na resources (human na financial) walizotumia halafu utumabie kama viko commensurate.

Sahihi kabisa mkuu, lkn bado tukilinganisha na walizotumia ccm (human and financial) kwa jimbo tu la Igunga ambazo kimsingi zimetoka serikalini still inanipa fursa kuona CDM wamepiga hatua kubwa sana, wamewakaba vilivo that proves watu wana mwamko mkubwa sana sasa wa mabadiliko.
 
Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
Ni mawazo mazuri sana. Naamini chama chetu sikivu kimekusikia hivi karibuni utaona matokeo yake kwa vitendo. Siku zote hatufanyi ajizi na masuala ya mabadiliko mpaka kielewekeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Igunga CCM imelazimika kutumia bilioni 2.5 na ndio bado wakapelekeshwa mchaka mchaka nguo kuchanika katika jimbo moja tu, je watalazimika kuiba kiasi gani cha fedha leo hii ili nao wabakie kwenye ramani 2015
 
kiloni

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
575
75
Tunajua mtakuja na sababu nyingi sana kuhusu kushindwa kwenu kwani mliyotegemea sivyo. Mmetumia hela nyingi sana zipatazo tshs 1.345bn kwenye uchaguzi huo, na kwa taarifa yako chama kwenye akaunti zake hakina kitu kimeishiwa ' kimefilisika'.
Wewe ni chama cha watu makini kufilisika mwiko. Mwaka 2005 mliona chopa mkaogopa mkaenda kuiba Benki kuu (EPA). Mwaka huu kwa Igunga tutawakamata mlikoiba tu nyie chama cha vibaka na majambazi>
 
OMEGA

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
693
300
Pia CHADEMA jitahidini muwe na ofisi zenye hadhi angalau ya wastani kwa kila wilaya,haya mabanda yaliyopo mawilayani yanawaangusha sana,hakikisheni ofisi zenu ziko wazi muda wote na zinafanya kazi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

6 Reactions
Reply
Top Bottom