C++ programming

C++ programming

msakhara

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2019
Posts
297
Reaction score
405
Habari kwenu wataalamu, katika kujifunza C++

Nimejaribu kufanya mfano huu, lengo likiwa ni kuonesha maneno yanayojirudia knye sentensi, lakini sipati matokeo nnayoyahitaji.

Nnakosea wapi?

20220312_130629.jpg
 
Nadhani kuna brackets umeruka hapo, code hazionekani vizuri
 
Habari kwenu wataalamu, katika kujifunza C++

Nimejaribu kufanya mfano huu, lengo likiwa ni kuonesha maneno yanayojirudia knye sentensi, lakini sipati matokeo nnayoyahitaji.

Nnakosea wapi?

View attachment 2147837
Mkuu inamaana unataka kutafuta maneno yanayojirudia kwenye sentensi na si herufi kama ni maneno.

Kama kawaida unapoanza kutatua tatizo kupitia code kuna vitu inakubidi kuvibainisha kabla ya kuanza kuiandika code yenye.

Step 1:
What are the input to your program?
Hapa inakubidi kuangalia jee ni data gani unahitaji kuingia kama input ambapo kwenye Case yetu ni sentensi.
Mfano tutumie sentensi hii kama input
"Baba na mama wanakwenda dukani kununua vifaa vya shamba pamoja na chakula"

Step 2:
What are the output of the program?
Hapa tutaangalia tunategemea kupata nini kama output baada ya kuingiza input.
Kwa case yetu tunahitaji maneno yanayojirudia kwenye sentensi.
Kulingana na mfano wetu neno linalojirudia ni
"na"

Baada ya kuvitambua vitu hivyo ndipo sasa tuanze kudadavua namna tutavyoandika program yetu na itoe majibu tunayohitaji.

Kwanza kabisa kwa kuwa sentensi ina maneno mengi basi njia rahisi ya kuitunza sentensi ili tuifanyie kazi ni kwa kutumia array. Kwa hivyo tutapikea sentensi na kuitunza kwenye array.

Kisha baada ya kuwa na sentensi nzima sasa hapo ndipo tutaanza ku compare neno moja moja lilopo kwenye Kila index na index zingine na pale tutakapo baini kuwa neno limejirudia basi tutalitunza kwenye array nyingine ili baada ya hapo tutoe jibu Kwa pamoja ni neno gani limejirudia.

Sasa kutokana na hayo maelezo nikipata muda nitaandika code Kisha ntaipost hapa.
 
Mkuu sasa nimekuja na simple code kwa ajili ya kudemostrate nilichokisema.
Vitu unavyopaswa kujua kabla ya kuisoma hii code ni
  • Array in C++
  • Multi-dimensional array
  • function in c++
find_repeated_word_cpp.png

Tujaribu kuangalia kwa haraka haraka namna hizi function zetu mbili zinavyofanya kazi.

  • Function "splitSentence"
kwenye hiyo for loop kinachofanyika ni kwamba variable "x" inakuwa inachukuliwa na characters za sentensi.

kwenye if statement hapo tunajaribu kutafuta ni wakati gani "x" ni empty space kwa sababu empty space ndio hutumika kutenganisha neno na neno kwenye sentesnsi. Na tukiipata basi moja kwa moja hilo neno tunaliweka kwenye array kisha varible yetu "word" tunai assign empty string ili tuitumie tena kutafuta another word.
kwenye else hapo ni kwamba tumejua character sio empty space kwa hivyo hiyo character tui assign kwenye "word"

Baaba ya hapo tunakuwa tayari na array yetu iliyo na words na sio sentensi tena. Sasa tutatumia hiyo array kutafuta repeated word.

  • Funtion "searchRepeatedWord"
Baada ya kuwa na array yako sasa hapo ni juu yako kuchagua algorithm ya kutumia kufanya searching. Kwa hii case nimeamua kutumia tu simple searching algorith kwa ajili ya kutatua hiyo changamoto.
Nimetengeneza for loop mbili, moja itakuwa ina hold array index ya neno kisha nyingine ya pili yenyewe kazi yake ni kuwa na kuchukua array index kuanzia inayofuata kutokea ile tuliyo nayo.
kisha baada ya hapo nimetumia hiyo "if statement" ili kubainisha array index zinazobeba values zinazofanana.

kama mleta mada utakuwa na swali basi waweza uliza ili upate maelezo zaidi.

msakhara
 
Back
Top Bottom