C.N.N habari za kibaguzi..

Don Calvino

Senior Member
Mar 3, 2012
113
29
Kumekuwa na habari nyingi muhimu za dunia ya tatu (3rd world countries), ila utakuta C.N.N na vituo vingine vya habari vinaona za kwao kwenye habari za kimataifa ni muhimu kuliko hata kuonyesha na kuweka za Africa.Mfano mlipuko wa Kenya juzi sijauona kuongelewa hata kwenye tovuti yao ya cnn.com
 
Ndio maana uwa siifagilii CNN na ni mara chache kuiangalia kwani uwa hawatoi uzito hata kidogo kwa habari zinazohusu Africa. Sio kama BBC ambao coverage yao kwa mambo ya Africa in nzuri kabisa!!!

Tiba
 
Al jazeera wana ubora katika usawa wa habari,ukiangalia pia ni kama hawafagilii news za U.S, maana wamelenga nchi za kiarabu,asia n.k.Na huko ndipo kwenye news za kusisimua..
Ndio maana uwa siifagilii CNN na ni mara chache kuiangalia kwani uwa hawatoi uzito hata kidogo kwa habari zinazohusu Africa. Sio kama BBC ambao coverage yao kwa mambo ya Africa in nzuri kabisa!!!

Tiba
 
Kila chombo habari kina sera zake na malengo ya mmiliki. Kinachotakiwa ni vyombo vyetu vya habari vizidi kujiimarisha na kuwa na wawakilishi sehemu mbalimbali katika Africa, EA au ko kote duniani ili kuondokana na utegemezi wa kupata habari toka vyombo vingine ambavyo vina mlengo fulani.

Pole Don Calvino, lakini habari si ndio umeshazipata au lazima ziandikwe na CNN ndio uamini?
 
CNN ipo kwa ajili ya propaganda za kimarekani, na haiko kama unavyodhani kukuletea habari za ulimwenguni.
 
Kila chombo habari kina sera zake na malengo ya mmiliki. Kinachotakiwa ni vyombo vyetu vya habari vizidi kujiimarisha na kuwa na wawakilishi sehemu mbalimbali katika Africa, EA au ko kote duniani ili kuondokana na utegemezi wa kupata habari toka vyombo vingine ambavyo vina mlengo fulani.

Pole Don Calvino, lakini habari si ndio umeshazipata au lazima ziandikwe na CNN ndio uamini?
..................mtafiti, anaripoti matokeo !
 
Kumekuwa na habari nyingi muhimu za dunia ya tatu (3rd world countries), ila utakuta C.N.N na vituo vingine vya habari vinaona za kwao kwenye habari za kimataifa ni muhimu kuliko hata kuonyesha na kuweka za Africa.Mfano mlipuko wa Kenya juzi sijauona kuongelewa hata kwenye tovuti yao ya cnn.com
Hivi hata huu mkuano wa AfDB unaoendelea Arusha wanaufanyoa coverage?
 
Utegemezi utegemezi utegemezi si mzuri. Hakuna mtu aliyemzuia mwafrika/nchi za Afrika kuanzisha chombo chake cha habari na kuweka wawakilishi dunia yote ambao watafanyia coverage vitu wanavyotaka waafrika. Yupo?
 
Inatia uvivu hata kuchangia yaaani.......aliyekwambia vyombo vya habari huwa ni kwa ajili ya faida ya jamii ni nani?????

Tafuta kitu inaitwa "Critical theory/ theorists" then specify the role of media ndo utajua falsafa behind media mkuu angalia hata ya hapa nyumbani tu kwa kuanzia angalia magazeti yanayohusiana na vyama vya siasa utaanza kupata mwanga then tafuta hiyo maneno hapo juu

Pole kwa kuchelewa kujua uhalisia.......mkuu Pasco@ please complement knowledge.......
 
Hivi hata huu mkuano wa AfDB unaoendelea Arusha wanaufanyoa coverage?

Media zetu za hapa hazijaifanyia ndio mnataka CNN wawafanyie, embu niambie kama hapa JF kuna Post ya huo Mkutano. Jitambueni ndo mtatambuliwa na wao wanalipa kodi jamani
 
Back
Top Bottom