C language au Python?

Upo vzr Mama
 
MK254,
Najifunza python sasa hivi nipo midway
Huko mwanzo nilikatishwa tamaa sana kwamba programming Tanzania hailipi nitakufa njaa bure
Nikasema potelea pote umenipa moyo sana Mkuu
 
Ulijifunza mwenyewe au ulipita shule mkuu?

Programming nimepiga darasa mwenyewe, ila kwa mbinde, ukiweza bora ufanye digri ya software engineering kabisa, kisha baada ya digri ujiongeze ongeze maana digri haitoshi, ila ikishindikana pambana mwenyewe kama chizi mbona mambo yataenda tu.
Ukiwa vizuri wateja watakutafuta badala uwatafute, kazi zako zitajitangaza.
 
Nafanya CS/SE chuo, lakini ujuzi mwingi napata mtandaoni zaidi ya darasani.
Nime devote muda wangu mwingi kujifunza mwenyewe badala ya kukomaa na ma slides .
 
mkuu tukianzia hapa kwa kushare baadhi ya sites ambazo programmers hujadiliana mambo yanayowahusu.

Kuna mdau amekutajia Nairaland, ni nzuri sana ile maana jamaa wanajadili programming kwenye level zetu za Kiafrika, tafuta sites za Kiafrika Afrika, yaani issues kama za Kibongo kabisa.
 
Nafanya CS/SE chuo, lakini ujuzi mwingi napata mtandaoni zaidi ya darasani.
Nime devote muda wangu mwingi kujifunza mwenyewe badala ya kukomaa na ma slides .

Yeah hii muhimu sana kupambana mwenyewe, chuo husaidia sana kupunguza makali na pia kukupa elimu ya principles kiundani zaidi, ila lazima uongeze juhudi zako za pembeni ndio ufaulu kufanya kitu.

Wakati naajiri, kuna vijana hunijia na CV zimesheheni vyeti vya kutisha, ila mtu ukimwambia aandike a very simple application from scratch, hana lolote kabisa, ukimhoji kuhusu mradi wowote aliowahi kufanikisha sehemu yoyote,

anataja inventory management aliyotumia kama school project, na keshasahau mambo mengi kuihusu hajawahi hata kuicheck wala kuiongeza features zozote tangu atoke chuo, hana utashi wowote kwenye programming.

Maana mtu mwenye utashi, hata akiwa nje bila kazi baada ya chuo ataendelea kujiongeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…