C language au Python?

Man ivi unajua pillars za almost every programming language zinatoka kwenye C yani ukisoma C itakua ni rahisi kwako kusoma programming language mpya.
Ni muhimu mkuu lakini si lazima, nafikiri kwa sababu ni lugha na sio framework.
 
Namie nilianzaga hivi hivi...
Mdogo mdogo alhamdulillah kwa sasa niko vizuri.

Nilianza na C, nikaja Java. Then nikageukia web development (HTML, CSS, JavaScript, PHP).
Kisha nikaja Python (japo nilikosa project za kuifanyia nikaachana nayo).

Katika language zote, ilonitesa ikachukua muda wangu ni JavaScript aisee!
 
mama uko vizuri
 
kwan JavaScript ina nn?...wewe ni kama mtu wa ngap akizungumzia jinsi alivyochukua mda kuisoma JavaScript.

me nlianza na c++,sasa hiv naihangaikia java ndio nije JavaScript

 
Piga mzigo wa Python kisha mengine yafuate, haswa kwa beginner Python ni rahisi na ni multi-purpose, yaani ina uwezo wa kufanya mambo mengi bila kuwa na ulazima wa kuchanganya lugha kadhaa.

Huwa najutia kwa kutochukua muda wangu kujifunza Python kipindi nilikua naanza anza programming, leo nimezongwa na miradi yaani fursa ya nikae na kujifunza Python nimekosa kabisa, lakini nimeweza kuona wataalam wanavyoitumia kufanya mengi.

Japo umesema nia yako ni Android apps, then hapo nenda kwa Kotlin na Java.

Hatimaye shukia kwenye (Javascript/HTML/CSS)
 

kama umezaliwa makete mtaa kuzalisha maindi na unataka kujua programming basi fanya yafatayo:-
1-kaa chumbani soma sana kuzidi hata daktari.
2-kichwa chako kiwe chepesi hata ukiambia x-y usiwe mzito kuchanganua.
3-hakikisha unapesa hipo mfukoni au mpo vizuri kwenu maana inakula mda sana.
4-pombe,marafiki,mademu,mdaa hivi vote si muhimu kwako.
5-kuwa na akili ya kujiongeza maana hakuna hata mmoja aliye weza kusema mimi hapa nimemaliza lugha .ndio maana kila siku lugha inakuwa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
chizcom,
Hii ndio sababu programmers wengi ni walevi kupindukia, maana mtu unajinyima na kupitia magumu hata miaka miwili, ile siku unafunguka na kuwa na uwezo wa kuandika code za kueleweka na kupata miradi unajikuta umeingia kwenye pombe kujilipa kule kujinyima kote.

Mimi niliacha pombe baada ya kujiachia sana ikaniharibu, ila ilikua yaani mwendo wa raha tu, mteja ananipa mradi ambao kwao umeshindikana, mwenyewe nikikagua naona issue ndogo sana, naukeshea kisha nikipokeza mradi napokea kama milioni mbili za Kitanzania, hapo moja kwa moja naenda kwenye bar, mwendo wa mishkaki, beer, mademu siku inaisha. Ni maisha ya hovyoo sana usipojipanga.

Nilifanya maamuzi magumu sana kuyaacha.
 
MK254, mkuu, am total new to the game. Na ni asubuhi ya leo nimekata shauri nakuamua nianze kujifunza PYTHON. Mkuu unaoshauri wewote kwangu before cjachoma mafuta.
 
mkuu, am total new to the game. Na ni asubuhi ya leo nimekata shauri nakuamua nianze kujifunza PYTHON. Mkuu unaoshauri wewote kwangu before cjachoma mafuta.

Kwanza fahamu kuijua lugha yoyote hautaishia kuchoma mafuta, iwe Python, Java au C, lugha utakayoichagua na kujitosa humo kwa nguvu zote, siku ukija kutoka hautajutia.

Lakini ushauri wangu, usikate tamaa, utakutana na magumu, utatamaushwa, kuna kipindi utajikuta mwezi unaisha haujapatia chochote na hauoni ukipiga hatua, ila ndivyo ilivyo kwa programming, hali huwa ngumu mwanzo mwanzo, mwaka wa kwanza lazima ukubali kujitolea, ujinyime vyote, marafiki na kila kitu, jifungie pambana, tafuta vitabu vya PDF onlines, videos, tembelea mitandao ya wataalam wanakojadili haya mambo.

Hatua kwa hatua hakikisha kila somo unalielewa kwa undani, rudia mara hata kumi, fanya mazoezi kwa kila kitu ikiwezekana hakikisha unaandika code mwenyewe bila copy pasting, ukisoma tutorial, usi-copy kilichoandikwa huko, wewe kisome uelewe kisha andika mwenyewe version yako ya code.

Nakutakia kila la heri, na kukutia moyo kwa herufi kubwa naandika kwamba PROGRAMMING INALIPA, HASWA KWA NCHI ZETU HIZI HAMNA USHINDANI MKALI, UKIWA VIZURI PROGRAMMING UTAPIGA HELA YAKO KAMA UMETULIA KWAKO NYUMBANI BILA PRESSURE.
 
Sidhani kama ana haja ya kusoma haya yote unless yuko darasani.

Mleta mada angalia unataka kufanya nini then uchague language ya kusoma.

Kama unataka kutengeneza androis apps kwanini ujichoshe na C au python?

Jali muda soma language kulingana na mahitaji sio usome kama uko darasani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…