Bye bye Jacob Zuma, times up, Wazungu wanakuondoa!

Bye bye Jacob Zuma, times up, Wazungu wanakuondoa!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,838
Mzungu hawezi kukubali kupoteza Afrika hata siku moja na wewe J.Zuma unajaribu kumyang'anya Mzungu tonge mdomoni kwa kuanza kujitoa ICC, sasa Mzungu ana hit back, na maandamamo yameshaanza na ninavyosikia baadhi ya heavy weights wa ANC wameshanunuliwa na sasa hawakutaki, kaa mkao wa kula muda umefika!

Nitakukumbuka Zuma kwa matukio ya ushujaa umeanzisha kampeni za kuondoa masanamu yote ya Kizungu, umeingia mkataba ya kujenga Nuclear power plant ambapo itaipatia AK Nishati ya uhakika, Wazungu hawataki hili, pole sana najua ndugu zako house niggas watakugeuka na kuwa upande wa Mzungu kama kawaida yao!

Amandla!!!

Afrika ni mtoto wa Muzungu!

President-answers-questions-in-parliament.jpg
 
Kuna muda tunawapa wazungu dhambi ambazo ni unjustifiable.
J. Zuma as a leader anayo mapungufu yake, of which the people of South Africa wanayo haki ya kudai masuala kupitia maandamano.

Has he been very clean kiasi kwamba hapaswi kupingwa na wananchi?
 
Ulichoandika hakina ukweli kamili.sidhani kama unazijua vizuri siasa za Ak.aliyeanzisha mpango wa kuzing'oa sanamu za wazungu si zuma bali ni kijana wa upinzani wa EFF.na hao unaowasema wamenunuliwa hakuna ukweli hapo.kwasababu kashachokwa na wenzake.na sababu kuu ni kwamba amehusika katika wizi wa pesa nyingi za uma.hata huo ujenzi wa nuclear kashachota pesa nyingi na baadhi ya wachumi wanahis gharama ya ujenz imezidishwa kwasababu ya rushwa iliyojaa ktk serikali ya Zuma
 
Hauwezi kuelewa mambo kama haya wewe endelea kuangalia DW, BBC,CNN &Co. watakupa picha ya Afrika yako unayoitegemea ktk kwao!
Usirukeruke, hebu weka sababu za wanachama baadhi wa ANC kuandamana. Tuanzie hapo ili kujua nafasi ya hao unao waita 'WAZUNGU'.
 
mbona hii habari imekaakishabiki hebu eleza kwa utulivu tukuelewe
 
Kuna sababu gan ya msingi kujitoa ICC kma cio udikiteta uchwara
Sababu wanazotoa ni za kijinga sana maana Hakuna kiongozi yoyote wa kiafrica aliwahi kukamatwa na kuonewa na ICC wote wanakamatwa kwa taratibu za kimahakama kesi zinaendeshwa kwa wazi na haki na hukumu zinatolewa asiyeridhika bado anapewa haki ya kukataa rufaa. Viongozi wazungu baadhi walishafikishwa huko pia kama Slobodan milisovich na wengine. Kama wapo ambao wanapebdelea viongozi wa Africa walitakiwa kukusanya ushahidi na kuuwasilisha ICC Ili wakamatwe. Kujitoa ni kuhalalisha uhalifu wa kivita ambao kwa Africa umekithiri sana. Inashangaza kwa nn Al bashir wa Sudan hakamatwi na viongozi wa kiafrica na kupelekwa the Hague?
 
Mleta thread anapotosha, sijui ni kwa maslahi gani. Recently South Africa inakabiliwa na kudorora kwa uchumi na ufisadi kuongeza. Ila moto zaidi ndani ya ANC ni kitendo cha chama kufanya vibaya katika uchaguzi mdogo uliopita.

Suala la ufisadi kubwa ni lile la Zuma na family ya kitajiri ya Gupta. Suala hili liliibuliwa na Waziri wa uchumi (ANC member) na taasisi ya kupambana na masula ya rushwa ilitoa ripoti iliyomtia Zuma hatiani.
Family ya Gupta imekuwa na ushawishi mkubwa sana katika uteuzi wa Mawaziri wa baraza la South Africa. Just to mention this one scandal, kuna nyingi ikiwemo ile ya ujenzi wa makazi yake ya 'anasa'.

Wazungu wanaingiaje hapa?
 
Mbona nasikia maandamano yameanzishwa na mMatumbi mwenzetu,tuangalie tusije kuwa kama waarabu wanatifuana gari likiwaka wanaanza kumlaum mzungu!
 
Sababu wanazotoa ni za kijinga sana maana Hakuna kiongozi yoyote wa kiafrica aliwahi kukamatwa na kuonewa na ICC wote wanakamatwa kwa taratibu za kimahakama kesi zinaendeshwa kwa wazi na haki na hukumu zinatolewa asiyeridhika bado anapewa haki ya kukataa rufaa. Viongozi wazungu baadhi walishafikishwa huko pia kama Slobodan milisovich na wengine. Kama wapo ambao wanapebdelea viongozi wa Africa walitakiwa kukusanya ushahidi na kuuwasilisha ICC Ili wakamatwe. Kujitoa ni kuhalalisha uhalifu wa kivita ambao kwa Africa umekithiri sana. Inashangaza kwa nn Al bashir wa Sudan hakamatwi na viongozi wa kiafrica na kupelekwa the Hague?
You have spoken my mind.
Wazungu kutofikishwa ICC it doesn't mean makosa wanayo tenda viongozi wa Africa hayapaswi kuhukumiwa ICC . Uhuru and Rutto are Africans na tumeona haki inatendeka.
 
Ulichoandika hakina ukweli kamili.sidhani kama unazijua vizuri siasa za Ak.aliyeanzisha mpango wa kuzing'oa sanamu za wazungu si zuma bali ni kijana wa upinzani wa EFF.na hao unaowasema wamenunuliwa hakuna ukweli hapo.kwasababu kashachokwa na wenzake.na sababu kuu ni kwamba amehusika katika wizi wa pesa nyingi za uma.hata huo ujenzi wa nuclear kashachota pesa nyingi na baadhi ya wachumi wanahis gharama ya ujenz imezidishwa kwasababu ya rushwa iliyojaa ktk serikali ya Zuma
Mi naumia sehemu moja tu
kwanin bara la afrika wanaogombea urais wote ni maskini na akitoka ni tajiri
lakin marekani anaegombea urais ni mtu tajiri na akitoka ameongeza utajiri wa nchi yake na si kuupunguza....
 
You have spoken my mind.
Wazungu kutofikishwa ICC it doesn't mean makosa wanayo tenda viongozi wa Africa hayapaswi kuhukumiwa ICC . Uhuru and Rutto are Africans na tumeona haki inatendeka.
That is true
 
Mtoa mada hamnazo umemjaa wivu waachie nchi yao Africa kusini wapiganie wanachokiamini na maslahi ya nchi yao wewe baki na nchi yako tajiri wananchi masikini lakini wanasiasa ni matajiri
 
Back
Top Bottom