bweni laungua moto lugoba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

bweni laungua moto lugoba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Sep 2, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ule utamaduni wa watanzania kutovumiliana na kuvunja sheria unaendelea tena usiku huu ambako wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugoba wilayani chalinze mkoa wa pwani wamefanya fujo na kuchoma bweni moja , mpaka sasa hivi haieleweki ni nini haswa chanzo cha fujo hizo mpaka kufikia kuchoma bweni hilo La wasichana moto pamoja na kufanya fujo zingine .

  Pamoja na hayo kuna habari kwamba baadhi ya wasichana wamezimia kutokana na mshituko walioupata katika matukio yanayoendelea shuleni humo pamoja na fujo za hapa na pale .

  Mpaka ninapoandika saa hizi walimu pamoja na baadhi ya wanafunzi wamefungiwa katika vyumba wengine wazimiwa simu zao za viganja pamoja na njia zingine za mawasiliano .

  Hakuna polisi wala wanausalama wowote waliofika katika eneo la tukio mpaka sasa hivi wengi wa wanafunzi hao wamelala chini kungoja huduma ya kwanza .
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Here we go.... Shy at it again!
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Sep 3, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Kabla ya tukio hilo mwalimu mkuu wa shule hiyo alibadilishwa hiyo ilikuwa ni miezi 3 iliyopita ndipo walipoanza kupata vipeperushi vya vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana wakitishia kuuwa walimu na kuchoma shule ndipo jana hiyo usiku shuguli hiyo ikatendeka ,haieleweki haswa kisa ni kuhamishwa yule mwalimu au kulikuwa kuna matatizo mengine zaidi shuleni hapo

  leo hii asubuhi ndugu na wazazi wengi wa wanafunzi wale wamefika shuleni hapo pamoja na wanafunzi huku mtiani wa mock kwa kidato cha 6 ukiwa unaendelea naamini vyombo husika watapatia jawabu lake na kuieleza jamii nini haswa kinaendelea katika shule ile .

  Ikumbukwe pia pale kulikuwa na mradi wa ict huu mradi haijulikani umeishia wapi na mafanikio yake yalikuwa ni nini kwa wakazi wa kijiji hicho na tanzania kwa ujumla mradi huo umekufa kimya kimya
   
 4. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  Zamani enzi za Nyerere matukio kama haya yalikuwa nadra sana, ni kutokana na msimamo wa serikali kusimamia maadili ya Mtanzania. Siku hizi serikali badala ya kusimamia maadili ya Mtanzani ya kumuadabisha mtoto mbele ya mkubwa, imevamia maadili ya Ulaya na Marekani ambapo Kumchapa mtoto hata kama wewe ni mzazi mtoto ana haki ya kukupeleka mbele ya sheria. Sasa haya ndo yametufikisha hapa tulipofikia. Fujo zinazidi sana kisa Haki Elimu. Tujikosoe Watanzania, tunajenga taifa la namna gani na la raia wa aina gani? Serikali ikae na wadau wajadili kuendesha elimu kulingana na Mazingira, tabia, maadili na mifumo ya kitanzania na si kuiga mambo ya kimagharibi.
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Polisi wanasemaje? Mkuu wa Mkoa anasemaje?
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  I am skeptical, Shy on the ring.....

   
Loading...