Bwana Mungu Nashangaa Kabisa

kweli mungu ni mwema jamni tumwimbie tumsifu tumsujudie na tusema kweli tumebarikiwa
amani kwenu wote wan JF
i like the song. naule wa sioshwi dhambi zangu bila....damu yake yesu
 
Roho yangu naikumbie, Jinsi wewe ulivyo mkuu.

Mzee white hair anaupendaga sana huu wimbo, kwenye fund-raising za makanisa huwa anauimbaga mwenyewe
 
Kwa wale wapenzi wa TP OK Jazz na ile miziki ya Don P. yaani Mayoni Mayaula, watakumbuka kuwa hii ndiyo sauti ya jamaa aliyeimba zile nyimbo nzuri sana ndani ya hiyo Album. Jamaa alitamba pia kwenye wimbo wa Maya wa OK Jazz, wimbo ambao miaka kadhaa nyuma wameupiga tena kwa Kiswahili. Jamaa anmkubali ingawa simuelewi anaimba nini ila sasa hivi ni muimbaji wa Gospel na Mhubiri Injili....... Carylito Lassa.


YESU NA RUMBA 🙂
 
Last edited by a moderator:
Oooh God,
Haleluyaaah!
Nina kushukuru Mungu kwa ajili ya ndugu huyu aliamua kukusifu wewe kwa tenzi katika uwanja huu, hakika si kwa akili yake ya kibinadamu wala kutaka kuonekana bali katika kukusifu Mungu wewe uliye hai. Baba ninamkabidhi ndugu huyu mikononi mwako na wote waliojumuika nae katika kukusifu katika matendo yako makuu. Baba ukaendelee kuwatumia katika huduma yako ee bwana, watu wote wakapate kukujua kuwa wewe ni Mungu na hakuna aliye zaidi yako. wewe ndiwe wa kwanza na wa mwisho wewe ni alpha na Omega baba nina nasema asante, kwa maana wema wako na fadhili zako ni mpya kila uchwao. Baba kupitia sifa hizi natangaza mpenyo kwa kila mwanajamii hii, natangaza kufunguliwa kwa kila msomaji, natangaza uponyaji kwa kila mojamoja katika jina la Yesu Kristu alieye hai, Baba watu wako wakaponywe kwenye ndoa zao, kazi zao, mashamba yao ooh Mungu wangu, Ninakutukuza kwa kuwe wewe ni mponyaji, wewe mtoaji wewe ni mwenye kubariki wewe mkuu. Baba nina kushukuru kwa kuwa utakwenda kutenda kadri ya mapenzi yako. Ninaomba na kushukuru na kukiri kupoea kwa Imani katika Jina Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Amen!!!!


Haleluya!!! wewe ndiwe Mungu mkuu!!!!!!
 
nimrudishie bwana nini kwa wema wake na fadhili dhake kwangu?......hakika wema na fadhili zitanifata,siku zote za maisha yangu,nami nitakaa nyumbani mwa bwana milele na milele
 
Ubarikiwe mtumishi wa Mungu, kila utakachoshika leo kiwe na Neema za Mungu, ubarikiwe ofisini,nyumbani wewe na ndugu zako wote, na hata mifugo yako, Mungu akusimamie kila pande,akukinge na maadui wabaya katika jina la Yesu baba aliye juu Amen <br />
<br />
 
jamni kwa yesu kuna raha sana
nishike mkon mungu wangu eeh ........
usiniache bwana ,
mungu awabarikia sana kweli ninafarijika kuona jf tunamtukuza mungu kwa njia ya ki pekee
amani kwenu wote siku ya leo na zote zijazo

swali: wapi nitapata tshrt za JF anayejua ani PM
 

amina mpendwa!!!

Mungu akubariki sana
 
Bwana Mungu wewe ndiye Mungu pekee unaestahili kuabudiwa. Sifa na utukufu wako vimetamalaki kila mahali..
Baba,
ninaomba nguvu zako na uweza wako vikaibariki Jamii forum, ili ipate kudumu na ikafanyike kuwa ni mahali salama kwa watu wako kujifunza na kujipatia maarifa mbalimbali. Ni katika jina la Yesu kristu ninaomba haya nakushukuru, Amen.
 
Waoh.... Leo watu wamekuw free hadi raha.. Hakika Mungu Baba ni Baba .. Hakuna aloponda hata mmoja.. Muanzisha wimbo UBARIKIWE UTOKAPO, UBARIKIWE UINGIAPO..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…