Bw. Lowassa, A Bitter Pill to Swallow | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bw. Lowassa, A Bitter Pill to Swallow

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kijakazi, Sep 2, 2012.

 1. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Baada ya kumsikiliza Bw. Lowasa (Waziri mkuu aliyepita) kwenye kipindi cha dakika 45 ITV kwa makini sana ninaweza kusema kwamba sijawahi tangu ufwatiliaji wangu wa siasa za hapa kwetu kusikia kiongozi akiongea mambo ambayo yamenigusa kama Bw. Lowasa.

  Kwangu mimi ameonekana kama mtu anayeelewa ni nini hasa tatizo letu na kwa nini hatutoki hapa tulipo kwa mfano moja ya vitu alivyonigusa ni pale kwenye Mafuta, anasema kwamba ni lazima tununue mafuta kwa wingi PALE AMBAPO BEI YA MAFUTA INAPOKUWA CHINI (soko la Dunia) ili kuweza kufidia kwa wakati inapopanda, hiyo kwangu mimi ni reasoning ya hali ya juu na ninalazimika kusema sijawahi kusikia kiongozi wa Tz akiweza kuongea na kutoa reasoning kama hiyo, kingine ni kuhusu uwiano wa ukuaji wa Uchumi na mabadilko ya maisha ya mwananchi wa kawaida (trickle down effect) ameweza kuelezea nini kifanyike ili ukuaji wa uchumi uweze kumfikia mwananchi wa chini, hakuna kiongozi wa Tanzania niliwahi kumsikia akiongelea nini kifanyike kutatua matatizo wote wengine nawasikia ni kulialia tu na kulalamika bila kutoa au kushauri nini kifanyike!

  Hivyo kwangu mimi pamoja na kusikia yote kuhusu huyu Bw. Lowasa ikiwemo tuhuma za mambo mbalimbali nafikiri ni mtu ambaye tukimtumia vizuri kwa njia yoyote ile, hata kwa usahuri tu, tunaweza kupata kitu!
   
 2. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  subiri waje magwanda hapa waanze kukuita fisadi.
   
 3. mchumia tumbo

  mchumia tumbo JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 1,368
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Alikuwa wapi kufanya hayo alipokuwa waziri mkuu?
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Uzuri wa mtu unapimwa kwa hotuba?
   
 5. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  linganisha lowassa alivyokuwa waziri mkuu na huyu mtoto wa mkulima au sumaye
   
 6. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135


  Hilo swali lingine, lakini nafikiri kama kumbukumbu yangu iko sahihi hakuwa Waziri Mkuu kwa muda mrefu kuweza kufanya mambo mengi anyway simtetei, ila kwangu hata mimi nilikuwa pia na maoni tofauti kuhusu huyu bwana kutokana na ninayoyasikia kuhusu yeye na kwa bahati mbaya sikuwahi kumsikia akiongea mpaka nilipokuja kumsikia hivi karibuni na naweza kusema imenibadilisha kiasi fulani mtazamo wangu juu yake!

  Nimeongolea tu yale niliyoyasikia akiyasema na kulinganisha na yale wanayoyasema viongozi wengine wengi wanapopewa nafasi ya kueleza ni nini kifanyike katika nchi!   
 7. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Balabala mlefu haikosi kona, mwanamke mzuri hakosi kasoro. Alishayasema yote marehemu Dr Remmy Ongala. Huwezi kusema mtu huyu ni mbaya 100% au mzuri 100% Binadamu tafsiri yake ndio hiyo.
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  We ni kijakazi wa Lowassa no doubt

  Eti mafuta
  wakati nchi ina gesi ambayo ni nishati mbadala?
  tunaweza tumia gesi na kupunguza kabisa kununua mafuta kwa kiwango kikubwa

  na je mbona Zambia wananunua kupitia bandari ya Dar lakini bei zipo chini?

  South Africa je?

  inflation je?

  dollarization je?

  Lowass was a mistake then.he is a scandal now,he will be a disaster tomorrow .....mark my words
   
 9. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hadithi kama hizi zinanikumbusha babu yangu mmoja huko kijijini alikuwa na nyumba yake ambayo alikuwa anaipenda sana! Hivyo alikuwa akipata wasaa wa kuifanyia matengenezo kama ni kupaka rangi, kurekebisha paa linalovuja au kioo kilichopasuka alikuwa na kawaida ya (baada ya matengenezo) anapanda baiskeli yake mpaka kwenye mwinuko ulio mbali kidogo na nyumba yake ili kuangalia nyumba inafananaje baada ya marekebisho.

  Hyuo alikuwa babu, kwa wakati wake alikuwa sahihi na ilikuwa atakachokiona huko kama kina hitaji marekebisho zaidi alikuwa hamuulizi mtu ila kuendeleza kile alichoamini kitafanya nyumba iwe bora zaidi!

  Nikirudi kwenye mada, inanishangaza kidogo kuhusu viongozi wa kitanzania. Mtu mkubwa na muhimu kama waziri mkuu hatakiwa kuwa analalamika kwenye vyombo vya habari kwamba mambo hayaendi sawa. Kwani tunaamini kwa sheria zetu yeye bado ni mtumishi wa umma kwa maana ya pensheni, kuna ubaya gani mawazo hayo mazuri aliyonayo akawaeleza safu ya uongozi iliyopo madarakania sasa?

  Kwa anachokifanya wananchi wanashawishika kuona kwamba mambo hayaendi sawa, na hii si salama sana kwa maisha ya taifa hili, uongozi kama timu lengo ni ushindi na mtu anayetaka ushindi wa peke yake ingawa yuko ndani ya timu kwa vyovyote vile atakuwa na matatizo.

  CCM hiyo hiyo hakuna vikao vya chama mkaelezana hizo ngojera badala ya kuwababaisha wananchi? Acheni hizo!
   
 10. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Kwanza haikuwa Hotuba, yalikuwa maswali na majibu nafikiri kuna tofauti, pili nafikikiri wote kwa namna moja au nyingine tunakuwa influenced na yale mtu anayoyasema kama ni ya ukweli au si ya kweli hiko ni kitu kingine, lakini cha muhimu ni uwezo wa mtu wa kuelezea na kutambua tatizo, hiyo pekee yake kwangu ni perfomance kubwa tu, ukilinganisha na viongozi wengine niliopata kuwasikia wakijibu maswali wanapoulizwa!
   
 11. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hiyo mbona hata wakulima wa mpunga Kilombero wanajua! Kuna muujiza gani kwenye hilo???
   
 12. mangusha kitoi

  mangusha kitoi Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 25, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni heri kuwa na "mtuhumiwa" mwenye uwezo wa kufanyq haya hapa chini kuliko kuwa na mtu "asiyechafuka" lakini goigoi.
  -mwenye maamuzi
  -mwenye kujua tatizo letu
  -mwenye solutions za matatizo yetu
  -mwenye uwezo wa kujenga hoja
  -mwenye udhubutu
  Bila hivyo nchi itakuwa na viongozi wasafi wanaojua kuomba maji ila hali wamezungukwa na mito na maziwa
   
 13. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ngoja wafuasi wa zitto wakusikie umesema hivyo...utapewa mitusi mpaka basi..... Ulichosema ni kweli huyu bwana akichukua nchi tutafika mbali sana lakini tuna bendera fuata upepo wengi tu humu saivi kila mtu anamtaka Zitto...jamani tumechoka watu wa kuuza sura ikulu tunataka rais mwenye uwezo wa kutoa maamuzi magumu ya nchi ili nchi isonge mbele...
   
 14. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Kuhusu Gesi, hayo nafikiri ni mambo ya baadae na yanahitaji pesa, nafikiri alikuwa anaongelea kuhusu sasa hivi nini kifanyike kuondokana au kupunguza kupanda kwa bei ya mafuta, kuhusu hizo nchi nyingine labda wao wanafanya hivyo wananunua kwa wingi Mafuta labda ndio maana bei ziko chini kumbuka hapa kwetu wanapitisha na wanakonunulia ni kwingine!

  kuhusu Dollarization, kama uliangalia kipindi chote aliliongelea hilo na pia kupendekeza nini kifanyike na akatoa mpaka mfano wa Afrika Kusini na Misri ambapo hauwezi kuruhusiwa tu kutumia dollar hovyo hovyo bila kuchajiwa na Serikali akapendekeza nini kifanyike!

  kuhusu kama yeye ni disaster au sio, hilo sijui mimi nimekuwa tu impressed na jinsi alivyokuwa anajibu maswali na kuelezea nini kifanyike kuboresha na huo uwezo bado sijauna kwa kiongozi mwingine na hivyo tu!

   
 15. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Inawezekana lakini mimi binafsi siajawahi kumsikia kiongozi akijaribu kuchambua na kuelezea tatizo ni nini na nini kifanyike na ukiyapima yako ndani ya uwezo wetu, na sio kuongelea kwamba sijui watanzania tunadharaulika kwa maana hatuji kuvaa suti vitu kama hivyo!
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kijakazi,
  Tatizo la Tanzania siyo kukosa viongozi wenye kujua solutions. Kinachokosekana ni political will ya kuyashughulikia matatizo kwa wakati.
   
 17. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,710
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Ndugu hatufanyi comparison ya mbovu kwa mbovu ili kutafuta ipi afadhali,Lowasa alikuwepo serikarini na hatukuona jema la kumnasibisha nalo iweje sasa?
   
 18. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135

  Nimesikia kwamba mradi wa maji kutoka Ziwa Viktoria kwenda Shinyanga mpaka Kahama ni moja kati ya Miradi aliyoisimamia yeye Bw. Lowasa sina uhakika na hilo lakini kama lina ukweli wowote basi ni bonge la Plus kwake kwani nimefika huko na kuona jinsi ule mradi ulivyowakomboa watu wa kule!
   
 19. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Eliah G Kamwela says thanks for this very useful post
   
 20. Karikenye

  Karikenye JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi EL aliposema UCHUMI wetu unapaa wewe ulikuwa Tanzania au wapi? Sifa moja ya watanzania wengi sio wafuatiliaji wa mambo consistently na siyo watunza kumbukumbu wa mtiririko wa visa au matukio yanayohusu siasa, uchumi au hata watu!! wanasahau haraka sana, hivi wewe Lowassa mpaka JK (Baba wa Taifa) anamkataa kwamba siyp presidential material ulikuwa wapi?

  Kinachowatesa NYINYIEM kwa sasa ni kukataa mambo ambayo kambarage aliyasimamia kwa kucha na vidole, ndicho kinachowamaliza NYINYIEM.... stay tuned...
  Kwangu mimi ameonekana kama mtu anayeelewa ni nini hasa tatizo letu na kwa nini hatutoki hapa tulipo kwa mfano moja ya vitu alivyonigusa ni pale kwenye Mafuta, anasema kwamba ni lazima tununue mafuta kwa wingi PALE AMBAPO BEI YA MAFUTA INAPOKUWA CHINI (soko la Dunia) ili kuweza kufidia kwa wakati inapopanda, hiyo kwangu mimi ni reasoning ya hali ya juu na ninalazimika kusema sijawahi kusikia kiongozi wa Tz akiweza kuongea na kutoa reasoning kama hiyo, kingine ni kuhusu uwiano wa ukuaji wa Uchumi na mabadilko ya maisha ya mwananchi wa kawaida (trickle down effect) ameweza kuelezea nini kifanyike ili ukuaji wa uchumi uweze kumfikia mwananchi wa chini, hakuna kiongozi wa Tanzania niliwahi kumsikia akiongelea nini kifanyike kutatua matatizo wote wengine nawasikia ni kulialia tu na kulalamika bila kutoa au kushauri nini kifanyike!

  Hivyo kwangu mimi pamoja na kusikia yote kuhusu huyu Bw. Lowasa ikiwemo tuhuma za mambo mbalimbali nafikiri ni mtu ambaye tukimtumia vizuri kwa njia yoyote ile, hata kwa usahuri tu, tunaweza kupata kitu!
   
Loading...