Bvr mwanza inaanza kwa vioja

Bvr mwanza inaanza kwa vioja

Joined
Jan 2, 2015
Posts
53
Reaction score
23
Ikiwa mkoa wa mwanza unajiandaa kuanza zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa mfumo wa bvr baadhi ya wilaya maandalizi yanafanywa katika hali inayotiashaka.jana na leo nimepita katika wilaya za misungwi na kwimba,nimeshangaa kuona maandalizi ya zoezi hili yanavyoendelea bila wananchi kuwekwa wazi kwa mambo ya msingi yanayotakiwa kujulikana wazi.kwa mfano katika maeneo niliyopita wananchi hata hawajui wataandikishwa lini ilihali katika halmashauri maandalizi yanaendelea kwa kasi.leo lipo jambo lililoshangaza wengi kwa wale waliolifahamu katika wilaya ya kwimba,nalo si lingine bali ni la tangazo la kazi ya uandikishaji la bvr kit operator na mwandikishaji msaidizi lililobandikwa leo lenye dedline ya kesho.yaani watu walifanyie kazi ndani ya masaa 24 tu na tangazo liko makuu ya wilaya tu.mchakato huu unatia shaka kwa wale wanaoona mbali.iweje suala lenye maslahi kwa taifa zima liende kwa utaratibu wa kimyakimya huku suala la hamasa vikiachiwa vyama vya siasa vinavyofanya kwa maslahi yao ya vyama?
 
Ha ha ha chanjo za mbwa tunatangaziwa mpaka masikio yanaziba ila tukio Kama hili ni kimya kimya tu ahsante watawala
 
Ha ha ha chanjo za mbwa tunatangaziwa mpaka masikio yanaziba ila tukio Kama hili ni kimya kimya tu ahsante watawala

Kweli kabisa.leo katika wilaya hiyo ya kwimba kunachanjo ya minyoo na kichocho jamii imetangaziwa wiki nzima tena kwa gari la matangazo na makaratasi yamebandikwa kila kona.jamii yote inatambua hilo.lakini ukiuliza wanaandikishwa lini hawajui.serikali sijui ina ajenda gani na zoezi hili
 
Ndg hii serikali ina lake jambo maana maeneo mengi BVR inapelekwa kimya kimya,chamsingi wananchi wakajiandikishe kwa wingi ili kuwapa aibu tume ya lubuva na ccm
 
Mbona kulikuwa hadi na ratibu humo jf , sasa kimya unamaanisha nin
 
Kweli kabisa.leo katika wilaya hiyo ya kwimba kunachanjo ya minyoo na kichocho jamii imetangaziwa wiki nzima tena kwa gari la matangazo na makaratasi yamebandikwa kila kona.jamii yote inatambua hilo.lakini ukiuliza wanaandikishwa lini hawajui.serikali sijui ina ajenda gani na zoezi hili

Hizo chanjo zina deadline?
 
Tukio liko Mwanza leo dunia nzima wanalijuwa halafu unasema halitangazwi?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Tukio liko Mwanza leo dunia nzima wanalijuwa halafu unasema halitangazwi?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Hebu jitahidi kukusanya akili zako vizuri kama kijana mtanzania mzalendo ambaye nchi hii leo iko mikononi mwako ujiulize unaweza kutoa tangazo la nafasi ya kazi kwa masaa 24 katika kazi yenye tija kama hii.jaribu kidogo kutoka nje ya box la chama ulimo upate fikra yakinifu
 
Wataneng'eneka weee lakini October itafika tu.. Wasijidanganye hata hao wachache watawachinja tu..

CCM mwisho October!!
 
Back
Top Bottom