Butiku: Yaliyotokea Oktoba 29 yametuachia doa la aibu, majirani wanasikitika pamoja na sisi

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema kuwa katika siku za hivi karibuni Tanzania imepitia kipindi kigumu kilichosababisha taifa kutetereka, lakini halikuanguka.

Akizungumza leo Januari 22, 2026 wakati wa kufungua mkutano wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere na Wazee, Butiku amesema tangu Oktoba 29, 2025 kumekuwapo hali ya sintofahamu iliyoacha doa la aibu kwa Watanzania, jambo ambalo limewafanya hata majirani na marafiki wa nje ya nchi kushangaa.

“Siku chache zilizopita tulipata tatizo na kidogo tukatetereka. Sitaki kurudia, mnakifahamu. Tangu tarehe Oktoba 29 (mwaka jana) tunatembea kidogo tuna aibu,” amesema Butiku.

Mzee Butiku, ameeleza hali hiyo haijaumiza Watanzania pekee, bali hata marafiki na majirani wa nchi wameonesha masikitiko na mshangao.

“Hii aibu si yetu peke yetu. Wanaotufahamu ndani na nje ya nchi wanasikitika Hawakutegemea kuona Tanzania ikiwa hivi,” amesema.

Amesisitiza kuwa taifa linapaswa kujitafakari, kurejea misingi ya uadilifu, umoja na maadili yaliyoasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere ili kurejesha heshima ya nchi.

Huyu si alisema anapenda utawala wa kijeshijeshi, sasa anazuga nini hapa?
 
Huyu mzee ni mhuni, halafu ni bonge la "sycophant." Nothing less, nothing more.
 
Back
Top Bottom