BUTIAMA: Mfanyabiashara Charles Magesa (31) auawa na kutumbukizwa kisimani

WIMBI la kuuawa na kisha miili kutupwa kwenye visima vya maji wilayani Butiama limezidi kuongezeka baada ya mfanyabiashara mmoja, mkazi wa Kijiji cha Busirime, kata ya Butuguri wilayani Butiama mkoani Mara, Charles Magesa (31) kukutwa mwili wake ukiwa unaelea ndani ya maji katika kisima kilichopo kando ya nyumba moja ya kulala wageni iliyopo katika Kijiji cha Isaba kata ya Buruma, Butiama.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo la kusikitisha, baba mzazi wa Charles, Alphonce Magesa, alisema kijana wake aliondoka nyumbani Machi 20, mwaka huu, majira ya saa 2.00 usiku na kwenda Isaba Senta akiwa katika matembezi yake ya kawaida ya kila siku.

Mzee Magesa alidai kuwa, kijana huyo hakurudi siku hiyo nyumbani kama ilivyokuwa kawaida yake na kesho yake ndipo alipopata taarifa kuwa kijana huyo siku hiyo, majira ya saa 7.00 usiku akiwa kwenye baa moja hapo Isaba, alivamiwa na kundi la watu wanne na kuanza kupigana nao.

Baba huyo alifafanua kwamba, baada ya kupata taarifa hizo za kijana wake kuonekana akipigana na kwa kuwa alikuwa hajaonekana nyumbani, aliingiwa na hofu akaichukua familia yake na kuanza kumtafuta maeneo tofauti kijijini hapo bila mafanikio.

Alieleza kuwa, alfajiri ya Machi 22, walimtafuta hasa jirani na eneo alilokuwa akipigana na walipofika karibu na nyumba moja ya kulala wageni ambayo haina jina ambayo pia ina baa ambayo Charles na hao watu walikuwa wakipata vinywaji, walishtuka kukuta mwili wa mpendwa wao ukielea ndani ya maji kisimani huku upande mmoja wa sehemu ya kichwa ukiwa na jeraha kubwa linaloashiria kuwa marehemu alipigwa kwenye ugomvi huo na kitu kizito hadi kupoteza uhai.

Tukio hilo ni la pili kutokea wilayani Butiama kwa kipindi cha wiki moja, ambapo katika tukio la kwanza lililotokea Machi 13, mwaka huu, mwili wa mkazi mmoja wa Kijiji cha Nyakiswa, Kata ya Kyanyari, Jerald Manyama (44) ulikutwa pia ukielea ndani ya maji kisimani kijijini hapo ambapo pia ilidaiwa kuwa naye alionekana akiwa baa kabla ya kukutwa na mauti.

Polisi wilayani Butiama wamethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba wanamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Isaba, miongoni mwa watuhumiwa wanne wanaosadikiwa kutekeleza mauaji hayo ambao walionekana wakipigana na marehemu kwenye baa hiyo.

Polisi wamesema chanzo cha ugomvi uliosababisha kuuawa kwa Charles bado hakijafahamika, uchunguzi unaendelea.Marehemu Charles alizikwa Machi 22, mwaka huu kijijini kwao, Busirime na ameacha mtoto mmoja.

Chanzo: GP

View attachment 727479
Hiki ndiyo Kisima alichotumbukizwa
Busirime

Saba saba
Tonyo
Irimba
Nyamika
Kiabakari

Ngoja niende hapo msibani
 
Kisima au shimo lenye maji. R I P kwa mfanyabiashara kama ugomvi sio Demu muuza bar basi Ni kulewa kupitiliza
 
Back
Top Bottom