Buswelu, Baba H mchumba huyu hapa....!

DMussa

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
1,310
296
Nimekumbana na hii huko kwa Michuzi....
Wenye Masters hebu changamkieni 0.5 wa Kijerumani!!

aluta continyua


Kaka Michuzi,

Kwa jina naitwa Jovinata Kileo. Natokea mkoa wa Kilimanjaro. Nina miaka 28, niko single, sina mtoto, na wala sijawahi kuolewa. Baba ni Mchaga ila Mama Mjerumani. Mimi ni mtoto wa pili katika familia. ninaye Kaka ambaye ameshaoa na anaishi zake Afrika Kusini. Mama ni marehemu ila baba anaishi Moshi

Elimu ya msingi nimesomea Moshi, na baadae kujiunga na shule ya International School of Tanganyika, Kabla ya kuendelea na masomo ya Juu Afrika kusini. Nilipata shaada ya kwanza ya biashara na hatimaye ya pili ya maswala ya utawala mwaka 2005.


Kwa sasa nafanya kazi katika shirika la kuhudumia wakimbizi lililopo Juba Sudan. Ingawa ninaweza kusema kwamba nimejaliwa kazi nzuri, na maisha mazuri, ninaona upungufu Fulani maishani mwangu, kwani kila mwanamke inabidi awe na familia yake, na Muda unavyozidi kwenda, naona uzee unaninyemelea bila matumaini ya kumpata mchumba.

Nilishauriwa kwenda kwa waganga wa kienyeji ili nipata usaidizi, lakini haijasaidia. Niliyempata akawa balaa, tapeli wa kutupwa. Mmoja wa vigogo nchini aliniahidi uchumba matokeo yake nikaja kugundua ningekua mke wa tatu. Sikuwa tayari kuwa mke wa tatu. na waliokuwa wakinishauri mambo ya waganga ndo kabisa wamezalishwa na kutelekezwa.


Namtafuta kijana mcha Mungu ambaye tutakuwa pamoja. Kutokana na familia yangu kuwa ya kidini sana (walutheri) nitafurahi sana kumpata Mkristo wa aina hoyote, na pia mcha Mungu.

Manka alipoweka maombi yake ya kutafuta mchumba, wengi walimuona kama vile kichaa. Ila, katika dunia ya sasa na hali ya sasa, inambidi mwanamke atafute vigezo kwa mwanamme.Sitaki kumparamia mpiga tungi wa siku mbili tatu, wala sitaki mlevi wa ngono. Namtafuta mume ambaye atakuwa baba watoto wangu. Sitafuti makuu, namtafuta mwanamme msomi lazima hawe na masters na hawe na umri chini ya miaka 35 na ambaye hajawahi kuoa.

Mzungu marufuku, wala mtu uchanganyiko sitaki. Asiwe mlevi, au mtumiaji wa kileo cha aina yoyote. Lazima hawe na kazi, Lazima awe na roho safi , mwenye fadhila na mpenda watu atakayenipenda kwa moyo wake wote.


Ulipoiweka picha ya bwana John Mashaka mara ya kwanza, niliguswa sana, ila kwa vile sikuwa na uhakika , nilishindwa na la kufanya ili niweze kuwasiliana naye; Nilikuomba contacts na email zake lakini ukanibania. Nilipokuomba namba za Mshikaji toka Ukraine pia ulinibania, wakati alibainisha wazi kwamba naye ni single nikashindwa kukuelewa.


Ulipoibandika picha ya Mashaka hapo jana, sikuwa na budi kuchunguza zaidi ili kufahamu hali yake ya ndoa. Inshallah, hajaoa. Sitaki kujua saizi yake ya viatu, sitaki kujua ana hela ngapi au magari mangapi, simtaki kwa vile yupo Marekani . Sitaki maisha yake mazuri, ninachohitaji ni roho yake safi. Naomba kwa hisani ya mbingu unipe namna ya kuwasiliana naye ili tujuane.

Ukiona kuna ugumu, basi niunganishe na yeyote mwenye wasifu wake. Nipo Tayari kununua tiketi na hela zangu na kwenda kukutana naye popote pale alipo.

Au kama atakuja Tanzania mwaka huu, naomba unijulishe ni lini ili nikutane naye bwana Mashaka kwa ajili ya maongezi ya kawaida. Ukininyima contacts, zake, basi naomba uchapishe conctacts zangu ili kaka yeyote wa kitanzania mwenye hizo sifa anitafute kupitia
jovinatakileo@yahoo.com


WAKO MTIIFU


Jovin-Grusdin- KILEO
http://issamichuzi.blogspot.com/

Yangu macho.... naona vijana kila siku mnatangaza kusaka wachumba, maombi yenu yanasikilizwa now play your part!!!!
 
Mkubwa kwangu...vigezo vyake vinanizidi sana umo ndani patakuwa hapakaliki..ntaanza kufundishwa wakati mie natafuta pesa tu shule ya upili imenitosha.

Beer sasa ndio kila week end...na jumapili baada ya kanisa...mchanganyiko huyu dada yetu hajasema.

Wengine tumechanganyikana kati ya msukuma na mhaya apo anasemaje?Ametumia neno gumu sana la (ulevi wa ngono) sijui alikuwa ana maana gani labda angesema ulevi wa mapenzi yaani hata nikimkuta anapika namwambia mama check room kama then namfata...hiyo ni balaaa...

Umri kanizidi one year..na ile formula ya kitanzania ya kuona sijui kama mnaijua..

Ukitaka kuoa chukua nusu ya umri wako ongeza saba...ndio unapata mke.Thats because ya maumbile ya dada zetu wanakuwa haraka sana so anaweza kukuzeekea ndani..ukasema hajijari kumbe ndio maumbile..so inabidi umchukue mdogo kwako ili akiwa anakuwa atakukuta katika ukuaji.

Regards

Buswellu
 
Ametumia neno gumu sana la (ulevi wa ngono) sijui alikuwa ana maana gani labda angesema ulevi wa mapenzi yaani hata nikimkuta anapika namwambia mama check room kama then namfata...hiyo ni balaaa...

Umri kanizidi one year..na ile formula ya kitanzania ya kuona sijui kama mnaijua..

Ukitaka kuoa chukua nusu ya umri wako ongeza saba...ndio unapata mke.Thats because ya maumbile ya dada zetu wanakuwa haraka sana so anaweza kukuzeekea ndani..ukasema hajijari kumbe ndio maumbile..so inabidi umchukue mdogo kwako ili akiwa anakuwa atakukuta katika ukuaji.

Regards

Buswellu

hahahahaha umefurahisha sana na hiyo formula nikifikiria kuowa sasa hivi mkuu nitakuwa na under 14 hahahahaha Buswelu balaaa
 
Yaani mimi nimepasi vyoooote....ila kwenye 'ulevi wa ngono' nimefeli vibaya sana yaani hakuna matumaini. Yaani nimelewa hadi vibega juu kama nime-overdose gongo. Sasa sijui atakuwa tayari kunipa practical counselling?

Halafu hivi Masters dili? Sijui za online zinakubalika?
 
Yaani mimi nimepasi vyoooote....ila kwenye 'ulevi wa ngono' nimefeli vibaya sana yaani hakuna matumaini. Yaani nimelewa hadi vibega juu kama nime-overdose gongo. Sasa sijui atakuwa tayari kunipa practical counselling?

Halafu hivi Masters dili? Sijui za online zinakubalika?

Wewe dogo, demu kesha mmind jamaa mmoja anaitwa Mashaka halafu kuna jamaa mmoja mtaalam wa IT yupo kwa Haki-Ngowi blog kesha unganishiwa tayari, links hizi hapa: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=11700.... hapo dogo huna hoja - anza moja!! lol
 
Kwa tanzania hiyo hata kwa sasa wanataka kuibadili bado kwa life cycle ya tanzania mtoto wa miaka 15 ni mdogo sana kwa kuwa kwenye ndoa.

Ila hiyo yangu hapo juu wala nilikuwa siijui mpaka mzee alipo nistua akaniambia kuwa tumia hiyo ni nzuri sana.

My point of view naona its fine.
What do you reckon LazyDog?

Good afternoon.
Buswelu
 
Muuuu, kuna kazi hapo huyo Mashaka aliyemaindiwa ajitayarishe kupewa mashariti mengine baada ya ndoa. Kwania mashariti kabla ya ndoa ni issue je mkianza kuonana kama kaka na dada si ndio isuue zinakuwa kubwa zaidi????????????
 
Niiliisoma kwa michuzi hii

Watu waliponda mbaya......em wanaume walioserious na wenye sifa izo

Mstirini jaman.....mke ndio huyooooo
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom