Kina mama wengi chanzo cha watoto kutowathamini kina baba, Hawatimizi jukumu lao la msingi kuwakumbusha watoto baba ni kiongozi na nahodha wa family

G Tank

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
2,297
8,776
Kama ilivyo kawaida, Watoto wengi wanakuwa upande wa mama kwajili ya huruma aliyoumbiwa kwa asili, Kitu hiki kimekuwa kikiwapa wanawake nguvu na influence kubwa sana juu ya watoto, Lakini wanasahau kwa maksudi kabisa jukumu lao muhimu la kuwakumbusha watoto "Muwe karibu yangu na mdeke mnavyotaka lakini tupo chini ya uongozi, Dira na juhudi za baba yenu".

Ni maneno mazito sana kwa mwanaume kuyatamka kwa watoto wake kwasababu kwa asili mdomo wa mwanaume ni mlango mgumu kufunguka manyanyaso ya utafutaji wa rizki ya kutunza familia hata kwenye kuonyesha mapenzi ya familia wao humtumia zaidi mama na watoto wanajua ni mama kwasababu mama yupo kimya.

Ni kwa maksudi kabisa hiki kitu wanakisahau, Heshima ya baba inaanza kupungua taratibu kadri watoto wanavyozidi kuwa wakubwa, Miwshowe baba huonekana kama mtu ambaye uwepo wake si chochote
 
Kaa na wanao vizuri wakiwa wadogo. Fanya nao homework ikiwezekana, wapigie hadithi za hapa na pale, Furahi nao, huzunika yao, nenda nao uwanjani kutazama soka au burudani yoyote. Wanapokua sekondari wasiliana nao mara kwa mara, watembelee wakiwa chuo halafu uone kama uzeeni wataona uwepo wako si lolote si chochote.
 
Na hapa ndio wababa wanafeli. Naimba kila siku, uzeeni wanaume wengi hawana wakulia nao sababu ya madude wanayofanyia wake zao na kutokuwa karibu na watoto, watoto hawaoni baba akimpenda mama. Hawaoni kama alikuwa na mchango wowote kwenye malezi hata kama alikuwa anavuja damu na jasho kuwahudumia. Haitoshi, pendeni wake zenu watoto waone. Kwenye kauli ya mwisho unaenda umezungukwa na watoto wako, faraja iliyoje!
 
Ndio maana wanaume tunashauriwa tuwekeze kwaajili yetu tunapozeeka.
Au rahisi zaidi ishi na wake zenu kwa upendo, watoto wenu waone wakiwa bado wadogo.

Wananume wengi wanakumbuka wake zao wakipata majanga ya kiafya mf. Kiarusi/figo kufeli/ajali nk. Wakati ujana wake/kipindi ana nguvu alikuwa busy na wanawake nje.

Huyo mwanamke wa kukuhudumia kwa upendo unamtoa wapi? Atakuhudumia kwa kipimo cha ulivyomtendea ukiwa mzima, na watoto si walikuwa wanaona? Basi na wao wanakuja kukuona kama jamaa na ndugu na sio baba, hawana mzigo juu yako

Wababa wanateseka sana makamo fulani lakini ni mavuno ya walichopanda kwa wake na watoto wao kipindi bado wana nguvu.
 
Na hapa ndio wababa wanafeli. Naimba kila siku, uzeeni wanaume wengi hawana wakulia nao sababu ya madude wanayofanyia wake zao na kutokuwa karibu na watoto, watoto hawaoni baba akimpenda mama. Hawaoni kama alikuwa na mchango wowote kwenye malezi hata kama alikuwa anavuja damu na jasho kuwahudumia. Haitoshi, pendeni wake zenu watoto waone. Kwenye kauli ya mwisho unaenda umezungukwa na watoto wako, faraja iliyoje!
Ni sawa lakini kama baba anavuja jasho na damu kuhudumia mama wakati unachukua credit usisahau wajibu wako wa kuhakikisha watoto hawana image mbaya kwa baba yao. Ukisimama na mume wako watoto watasimama naye hata kama alikuwa na mapungufu.
 
Kaa na wanao vizuri wakiwa wadogo. Fanya nao homework ikiwezekana, wapigie hadithi za hapa na pale, Furahi nao, huzunika yao, nenda nao uwanjani kutazama soka au burudani yoyote. Wanapokua sekondari wasiliana nao mara kwa mara, watembelee wakiwa chuo halafu uone kama uzeeni wataona uwepo wako si lolote si chochote.
Nakazia
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Watoto wanaokaa na masingle mother Huwa wanajazwa maujinga ambayo huathiri maisha yao
 
Au rahisi zaidi ishi na wake zenu kwa upendo, watoto wenu wasione wakiwa bado wadogo.

Wananume wengi wanakumbuka wake zao wakipata majanga ya kiafya mf. Kiarusi/figo kufeli/ajali nk. Wakati ujana wake/kipindi ana nguvu alikuwa busy na wanawake nje.

Huyo mwanamke wa kukuhudumia kwa upendo unamtoa wapi? Atakuhudumia kwa kipimo cha ulivyomtendea ukiwa mzima, na watoto si walikuwa wanaona? Basi na wao wanakuja kukuona kama jamaa na ndugu na sio baba, hawana mzigo juu yako

Wababa wanateseka sana makamo fulani lakini ni mavuno ya walichopanda kwa wake na watoto wao kipindi bado wana nguvu.
Ukiachana na hayo yote ila wanawake ni wabinafsi sana..,hata ufanyie nn.
 
Wanaume tusijisahaulishe, mbwa anamkumbuka anayemlisha sio anayenunua chakula. Men spend time with your kids. Sio ukitokea tu watoto wote wanakimbia. Cheka na watoto wako, acha wakufurahie, kula nao chakula cha jioni. Ukiweza toka nao out waletee watoto wako zawadi ikitoka kazini hata pipi za mia mia. Spend time with your kids.
 
We tenda nafasi yako watoto watajionea wenyewe kuwa we ni kiongozi na nahodha na vyeo vyote unavyotaka, hata ukitaka wakuone amiri jeshi.

.....ukiona unaomba sana kuheshimiwa jitathmini.
 
chagua mama bora kwa watoto wako,kama mama huwa hakuvalue kama kichwa cha familia unataka watoto wafanyeje.
 
Wanaume tulishakubaliana hela zozote utakazo mpa mke wako ( mama ya watoto wako) toa mbele ya watoto wako wakiona . Watoto wajue kabisa hii ni baba katoa kampa mama na mama akatupa sisi.

Nb. Hii kuonyesha upendo kwa mwanamke wako sishauri . Wanawake hawahitaji kupendwa wanapenda mikiki mikiki hawataki utulivu kabisa.hapa mtumie akili wanaume wezangu shauri yenu. Wewe jifanye una mpenda mkeo watoto waone ndiyo uone moto mkeo atakao kua ana kuwashia mbele ya watoto wako huku akiwaambia wanao wewe ni bepari na hela unazotoa niza freemason
 
Back
Top Bottom