Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUFUTA RANGI WALIZOPAMBA ENEO HILO NA OFISI YA SERIKALI YA MTAA .
Wafanyabiashara wa Mitumba eneo la Kinondoni Manyanya ( kituo cha kuelekea kariakoo ) wamepatwa na kile kinachoitwa " Matumizi ya Nguvu ya Watawala kwenda kwa wananchi wenye mitazamo ya Upinzani nchini " baada ya kupewa 'Onyo' kutokana na kuonekana kulipamba eneo hilo kwa bustani, na kisha kutia nakshi kwa rangi za bluu, nyekundu, na nyeupe kwenye vijinguzo vilivyopo eneo hilo, ambazo rangi hizo zinahusishwa na rangi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ), na kisha kuweka bango lenye picha ya aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho Edward Lowassa.
Waandishi wetu walifanikiwa kuipata barua ya wito kwa wafanyabiashara hao kutoka ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kinondoni Mjini ambapo eneo hilo lipo ndani ya mtaa huo, ikimtaka mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo alinayefahamika kwa jina la Keneddy, kufika mara moja kwa ajili ya kupata taarifa za mwongozo kuhusu eneo hilo, na mara baada ya kufika alitakiwa kuhakikisha anazifuta rangi hizo mara moja.
Licha ya eneo hilo kuonekana ni la kuvutia kufuatiwa kutunzwa vizuri kwa bustani yake na wafanyabiashara hao, rangi zilizopakwa eneo hilo zimeonesha kuwakera baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi ( CCM ) na kuamua kuitumia Ofisi ya Serikali ya Mtaa huo ili kushinikiza wafanyabiashara hao kufuta rangi hizo mara moja .
My take: Nafikiri diwani wa Kata hiyo Mh. Mustafa Muro, ( ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji ya Jiji ) pamoja na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob, wanatakiwa kutoa mwongozo juu ya nani anapaswa kufanya nini katika maeneo ya hifadhi ya barabara, ili kila mtu atambue wajibu wake juu ya maeneo hiyo.
Mashuve Aron, Edward Simbey, Lilanga Maganga, Steven Andrew Mmbogo, Allan Kashoro, Steve Mwakyoma, Rose Moshi Makey, Erick Mosha, Fenian Meena, Hatibu Makumuli, Zuberi Makumuli, Maneno Ramadhani, Stibah Gasto, Mazoya Souza Dé.