Bustani ya Eden ilikuwa Tanzania?

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
871
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Dr Leakey na mkewe wanabainisha kuwa fuvu la mtu wa kale duniani lilikuwa Olduvai Gorge huko Arusha.

Kwa utafiti huu tunaweza kujiuliza maswali kama:

Je, ni nani huyo mtu wa kale zaidi ya Adam?

Kama hakuna wa kale kumzidi Adam je, hilo haliwezi kuwa fuvu la Adam?

Kama ndivyo basi ni dhahiri kuwa bustani ya Eden ilikuwa Arusha.

Naomba kuwasilisha.
 
Inamaana hata huangaliagi hata National Geographic Channel? Mbona inafahamika Ngorongoro crater ndiyo Eden yenyewe?

th
th

pic_13.jpg

NgorongoroPanorama.jpg
 
Huu uzi uliwekwa hapa 5/9/2011

Source: Radio France Internationale.

Juzi wakati nasikiliza hii radio, kulikuwa na mama mmoja anahojiwa. Huyu mama anaitwa Chaiba Kombo ni Mwandishi wa Vitabu na Mdau mkubwa wa Sanaa za hapa Tanzania. Kwa hapa Tz sio maarufu sana ila nje ya mipaka kachukua tuzo nyingi za uandishi wa vitabu vya kijadi.

Sasa wakati anahojiwa alieleza kwamba research zake alizozifanya licha tu ya kuonyesha kwamba mifupa ya kale imegunduliwa hapa tanzania(Olduvai Gorge), ni kwamba wale watu wa zamani waliokufa kwenye gharika la Nuhu(kizazi kile kiliteketea kwa maji), mifupa yao watu hao ipo hapa tanzania na ana ushahidi huo.

Akaenda mbali zaidi akasema Bustani ya Eden walipokaa wazazi wa mwanzo Adam na Eva pia ilikuwapo hapa Tanzania. Research yake kajaribu kuipeleka Chuo kikuu cha Dar UDSM, lakini mawazo yake waliyapuuza na hawakumpa ushirikiano. Kwahiyo anafanya kazi na wattu wa Mataifa sasahivi.

Vp wadau kuna details zozote kwa mwenye kulijua hili?
 
Huu uzi uliwekwa hapa 5/9/2011

Source: Radio France Internatinale.

Mara nyingi ni nadharia tu na hadithi flani flani zenye mtiririko na mpanhilio wa kuleta intellectual bullying tu ili kukidhi agenda fulani.

Kuna fuvu la mtu wa kale zaidi limevumbuliwa Georgia, pia SA wana fuvu la kale zaidi. Baada ya gharika, vitu na watu walisombwa na gharika ile kutoka umbali mrefu! Kama kuna mabaki ya kina Nuhu hapa Tanzania, it means walisombwa na gharika toka mbali huko wakaja kutulizwa hapa!?

Nadharia ya Bustani ya Eden kuwa Tanzania haiishii pale Ngorongoro tu! Kuna hifadhi iko lake Nyasa huko. Ni hifadhi yenye maua mengi na ya aina tofauti kuliko sehemu nyongine, mito yake, uoto, milima na mabonde, etc..

Historia imefichwa sana, haipo wazi. Labda "Ufahamu" ndio tunda lenyewe la katikati!.
 
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Dr Leakey na mkewe wanabainisha kuwa fuvu la mtu wa kale duniani lilikuwa Olduvai Gorge huko Arusha.

Kwa utafiti huu tunaweza kujiuliza maswali kama:

Je, ni nani huyo mtu wa kale zaidi ya Adam?

Kama hakuna wa kale kumzidi Adam je, hilo haliwezi kuwa fuvu la Adam?

Kama ndivyo basi ni dhahiri kuwa bustani ya Eden ilikuwa Arusha.

Naomba kuwasilisha.
Changamoto iliyopo ni kufahamu hasa Adam aliumbwa mwaka gani na alikuwa na umbo na mwonekano gani muda huo. Fuvu la liliovumbuliwa katika Bonde la Olduvai lina umri wa miaka milioni 1.7. Aidha, kuna nyayo katika eneo la Laetili zenye umri wa miaka milioni 3.6. Kwa hiyo unaweza kuona kuwa Binadamu wamekuwepo katika ardhi ya Tanzania kwa muda mrefu, muhimu hapa ni kwamba huyu ni "Bianadamu wa Kale" sio "Binadamu wa Kwanza", hakuna anayefahamu kama ndiye wa kwanza, kinachofahamika ni kwamba ni wa kale.
 
Bustani ya Eden ipo katika nchi ya Iraq. kuna mito mitatu inapita ktk hiyo bustani. mojawapo wa mito hiyo ni mto Tigris.
 
Mkuu Mrigariga nadhan historia yako unayosemea inaanzia toka binadamu wa kale alipoanza kustaarabika! Sisi tunaangazia kuhusu kuumbwa ua mwanzo wa ubinadamu
 
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Dr Leakey na mkewe wanabainisha kuwa fuvu la mtu wa kale duniani lilikuwa Olduvai Gorge huko Arusha.

Kwa utafiti huu tunaweza kujiuliza maswali kama:

Je, ni nani huyo mtu wa kale zaidi ya Adam?

Kama hakuna wa kale kumzidi Adam je, hilo haliwezi kuwa fuvu la Adam?

Kama ndivyo basi ni dhahiri kuwa bustani ya Eden ilikuwa Arusha.

Naomba kuwasilisha.
Lakini pia mkuu..kweni unaamini mtu wa kwanza kuwepo duniani ni huyo Adam??kama je habari ilianzia kwa Adam tu na kumbe kuliwahi kua na watu wengine duniani?
 
Hadithi za abunuasi katika ubora wake.

Ni ubunuasi kabisa, ukisoma biblia mwanzo sura ya pili inaonyesha ramani ilpokuwepo bustani ya edeni. Kuna mito minne ilipita hapo bustanini ili kuimwagilia, mito hiyo inatajwa kwa majina. Kuna MTO frati, hidekeli, pishoni na gihoni. Je mito hiyo kwa majina yake IPO ngorongoro? Kiuhalisia bustani ya edeni MTU akisema ilikuwa maeneo ya Iraki atakuwa hayupo mbali na ukweli ikiwa utaangalia ramani kwa kuangalia hiyo mito
 
Mleta mada unatakiwa uwe upande mmoja tu.

Masuala ya Dr.Leakey na fuvu la mtu wa kale zaidi Olduvai George ni masuala ya kisayansi.
Na masuala ya Adam na Hawa au bustani ya Eden hayo ni masuala ya kiimani na ni vigum kuyathibitisha kisayansi na aghalabu fact mbili hizo hazichangamani.
 
Ni ubunuasi kabisa, ukisoma biblia mwanzo sura ya pili inaonyesha ramani ilpokuwepo bustani ya edeni. Kuna mito minne ilipita hapo bustanini ili kuimwagilia, mito hiyo inatajwa kwa majina. Kuna MTO frati, hidekeli, pishoni na gihoni. Je mito hiyo kwa majina yake IPO ngorongoro? Kiuhalisia bustani ya edeni MTU akisema ilikuwa maeneo ya Iraki atakuwa hayupo mbali na ukweli ikiwa utaangalia ramani kwa kuangalia hiyo mito
Hapo ndipo unapowaona hawa watu wana leta hadithi za kusadikika kutoka kisiwa cha kusadikika
 
Eden tafsiri yake kamili ni uwepo wa Mungu,,kwa hyo endeleeen kubishanaaaa mpka mchoke
 
Back
Top Bottom