Business Plan ni nini?Ina umuhimu gani?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,490
5,525
Business Plan katika biashara ni kama ramani ya nyumba.
Unapotaka kujenga Biashara ni sawa na unapotaka kujenga nyumba au unapotaka kwenda mahali fulani ni muhimu sana uwe na ramani.Business Plan ni kama ramani ya Biashara yako.
Business Plan inaweza kuwa fupi yenye kurasa moja au inaweza kuwa ndefu yenye kurasa 1000 ila kazi yake ni ile ile kukupa Ramani.
Unapoandaa business plan lazima ujiulize maswali yafuatayo:
  1. Je business plan hii ni kwa ajili ya nani?Yangu mwenyewe,ya wawekezaji,ya kuombea mkopo,ya wafanyakazi wangu au ya nani?
  2. Je Hii plan ni ya muda gani,Miezi mitatu?sita? mwaka? miaka mitatu?au mingapi?
  3. Je ni bidhaa au huduma gani ambayo ni ya msingi katika business plan yako?Je ina bidhaa/huduma za ziada ambazo unaweza ongezea?Je kuna bidhaa au huduma ambazo unazihitaji ili uweze kutoa bidhaa au huduma hizo?
  4. Je Wateja wako ni wakina nani(Walipo,Umri wao,Kipato chao na jinsi wanavyopata huduma au bidhaa hiyo wakati huu)
  5. Je suppliers wako ni wakina nani(Walipo,bei zao,na jinsi wanavyotoa huduma zao kwa sasa
  6. Je washindani wako ni wakina nani(Walipo,bei zao na jinsi wanavyotoa huduma zao kwa sasa
  7. Je utaleta ushindani katika eneo gani(Bei,ubora,upekee au ubunifu wa nyongeza?)
  8. Je unao uwezo wa kuisimamia baishara yako(Skills,Wafanyakazi,ujuzi etc)
  9. Je biashara yako inahitaji gharama kiasi gani ili iweze kujiendesha?
  10. Je Ni mauzo kiasi gani yakuwezesha kujiendesha kibiashara?
  11. Je ni mauzo kiasi gani yatakupa faida
Hayao ni baadhi ya maswali ambayo ni lazima business plan ijibu na yatajibiwa wakati unapoandaa business plan yako.

Kwa msaada katika kuandaa na kusimami business plan yako tuwasiliane kwa Email masokot@yahoo.com au SIMU namba 0710323060

Karibuni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom