Busara za Mzee

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,305
8,655
Katika Uchina ya kale (Acient China) aliishi mzee mmoja mwenye busara sana, umaarufu wake ulivuka mipaka ya falme jirani na maeneo mengine mengi.

Watu walitoka maeneo ya mbali kuja kupata busara za mzee huyu. Alikuwa mshauri wa watawala, watu mashuhuri pamoja na watu wote.

Mtu yeyote mwenye swali gumu alikuja kuuliza au kutatua tatizo lake au hata kupata busara. Basi kuna huyu jamaa muuza duka alimtuma mwane akajipatie busara kwa mzee huyu, ilitakiwa akajifunze siri ya kuwa na furaha maishani.

Kijana yule alitembea kwa siku 40 msituni mpaka alipoikuta jumba kubwa la kifahari anamoishi mzee huyu mwenye busara.

Alipofika badala ya kukuta mtu yule peke yake alikuta kundi kubwa la watu, wengine wakitoka na wengine wakiingia, mziki mzuri mlaini ulikuwa ukipigwa na vyakula vitamu mno vilikuwa vikiandaliwa sehemu hiyo!. Ilibidi asubiri masaa mawili kuonana na mzee huyu kwani alikuwa anafanya mazungumzo na watu wengine.

Baada ya muda mzee yule akamsikiliza yule kijana amueleze shida yake, kijana akamueleza kwamba anataka siri ya kuwa na maisha ya furaha, mzee akamwambia kwa sasa sina muda njoo baada ya masaa mawili.

Lakini akamwambia kabla hujaondoka “Chukua kijiko hichi chenye matone mawili ya mafuta, kisha zunguka nyumba yangu yote na urudi mafuta yakiwa hayamwagika”.

Kijana akapanda na kushuka ngazi nyingi huku akimanika na kijiko kuhakikisha mafuta hayamwagiki, baada ya masaa mawili akarudi.

Mzee akamwambia sawa, je umeona urembo unaoninginia kwenye nyumba yangu? Umeona bustani nzuri iliyomchukua miaka 10 mtaalamu wa bustani kuitengeneza? Umeona maktaba nzuri iliyopangika kiustadi?

Kijana akakiri kwamba hajaona yote hayo, alizingatia sana mafuta yasimwagike. Kisha mzee akamwambia basi rudi upya kaangalie mambo yote hayo kwa maana “Huwezi kumuamini mtu kama huijui nyumba yake”. Kijana akarudi upya na kijiko chake chenye matone ya mafuta, akaangalia urembo wote wa lile jumba, milima mizuri ya maeneo hayo, marumaru ya kutosha, michoro iliyochorwa kiustadi na wachoraji mahiri pamoja na bustani nzuri.

Baada ya kurudi kwa mzee akamueleza kila kitu, lakini mzee akamuuliza yako wapi matone yangu ya mafuta niliyokuachia? Kijana kuangalia kweli hakuna mafuta!

Kisha mzee akamwambia sikiliza mwanangu, siri ya kuwa na maisha yenye furaha ni kuona uzuri na maajabu ya ulimwengu bila kusahau matone ya mafuta kwenye kijiko!

Ni tumaini langu umepata somo!

FB_IMG_1595323394043.jpg
 
furaha haipatikani kwa style hiyo aache ujinga huyo mzee

bustani tu miaka 10 au miti ya mbao
 
Back
Top Bottom